Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu ya TP Mazembe leo amefanya maajabu makubwa katika historia ya soka la nchini Congo baada ya kufunga magoli 6 kati ya 13 yaliyowekwa kimiani na TP dhidi ya FC Police katika michuano ya ligi ya jimbo la Katanga.
Mbwana Samata amekuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kufunga idadi hiyo ya magoli katika mechi moja hivyo kuweka rekodi ndani ya klabu yake.Magoli mengine katika mechi hiyo iliyoisha kwa TP Mazembe kushinda ugenini kwa mabao 13-1 yalifungwa na Wachezaji, Lusadisu (3 ), Kanteng, Traore ( 2 ) na Mabele.
Ngoja atutoe tongotongo wabongo. Huyu dogo atacheza Ulaya. Mungu Ibariki Tanzania. Mungu mbariki Mbwana Samatta.
ReplyDeletehongera mbwana samata,, kaza buti baba usiridhike kabisaaa tupo pamaoja.................................
ReplyDeleteMbwana Samatta anatuwakilisha vyema, kikubwa aongeze juhudi na amuombe sana Mungu aonekane ktk ulimwengu wa soka wa nchi zilizoendelea na pia Mungu amuepushe dhidi ya janga la kuwa majeruhi na atunze damu ktk kipindi hiki cha ujana wake. Tupo pamoja naye!
ReplyDeletekaka anaejua anajua tuu bravo Samatta kaza kama upo mechi za mchangani!!!!
ReplyDeleteHooooolla
ReplyDeletekaka mbwana namwona ulaya shortly
ReplyDeleteNa bado tu.. Kijana anani impress balaa!! Shukrani za dhati ziende kwa Klabu ya SIMBA waliotoa fursa kwa kijana wetu kwenda kusakata 'gozi' huko DRC. Kamua baba kamua babaaa... kamua baba usitumie hiriziii!!!
ReplyDeleteDogo, ww ndo pro wa kuigwa. Kaza buti usiridhike na hapo ulipofikia, ww ni wakucheza Europe nasi Afrika.
ReplyDelete