Search This Blog

Thursday, November 17, 2011

CAPELLO: PHIL JONES ANANIKUMBUSHA FRANCO BARESI


Kocha wa England Fabio Capello ameonekana kuridhika sana na kiwango cha Phil Jones baada ya kumfananisha kinda huyo wa Manchester United na moja ya wachezaji bora wa muda wote Franco Baresi.

Jones alicheza mechi yake ya 3 kwa England katika nafasi 3 tofauti baada ya kucheza kama holding midfielder katika mechi dhidi ya Sweden katika uwanja wa Wembley.

Teeneger huyo ambaye anakiri kuwa nafasi yake halisi kiwanjani ni beki wa kati, alicheza mechi yake ya kwanza kama beki wa kulia in Montenengro mwezi uliopita kabla ya kucheza kiungo cha bele katika mechi dhidi ya Spain wiki iliyopita.

“Ni vigumu sana kupata mchezaji kama Phil Jones, vigumu sana,” alikaririwa Capello.

“Katika career yangu labda nimeshakutana na aina ya wachezaji wa namna hiyo wawili tu. Naongea kuhusu Franco Baresi akiwa Milan na Fernando Hierro at Real Madrid. Walikuwa wachezaji wazuri, ambao waliweza kucheza kama kiungo na vilevile kama beki wa kati.

“Phil anaweza kucheza katika sehemu tofauti na katika kiwango cha juu. Hii inaonyesha ana kipaji kikubwa sana.”

“Kitu kizuri kuhusu Jones anapopokea mpira anatulia na kucheza vizuri bila woga,” aliongeza Capello.

“Anatoa pasi nzuri na kuzuia vizuri sana, kumuona akicheza mbele ya ukuta wa nyuma katika mechi dhdi ya Sweden kilikuwa kitu muhimu sana kwangu, kwa sababu sasa kama Parker akiwa hayupo fiti, then ninaye mbadala wake, nae ni Jones.” Alimaliza Fabio Capello.

1 comment:

  1. Hello shaffih mimi nilikuwa nasemaje mkipata nafasi ktk miaka 50 hii ya uhuru mwende ccm kata 15 temeke mwisho mmuoji omary kapera (mwamba) ambaye pale ni mwenyekiti wa ccm nae atupe nzi zake za yanga na pan vile vile huyo jamaa hana tofauti na mbwiga
    wako
    Harambe

    ReplyDelete