Viongozi hao wa vilabu wamesema sababu kuu ya kukataa kwenda kufanya mazungumzo na Tenga ni kwa sababu hawadhani kwamba kuna jipya lolote wataloambiwa ili kuweza kubadili msimamo wao wa ligi ya msimu ujao kuendeshwa na kampuni ya vilabu.
“Hatuoni kama kuna umuhimu wowote wa kufanya majadiliano juu ya suala hili, sisi sote tumeshaamua kwamba msimu ujao ligi itaendeshwa na kampuni ya vilabu vishiriki, TFF na Tenga wenyewe hawataki, wanataka kamati itakayoteuliwa na Tenga ndio iendeshe ligi. Tenga anataka tukae tujadili ajenda ipi? Sisi kwa pamoja tumeshaamua kwamba ligi ya msimu ujao itaendeshwa na kampuni yetu na huu uamuzi wetu wa mwisho,” alizungumza Geoffrey Nyange Kaburu ambaye ni mwenyekiti wa Kamati maalum ya kusimamia mchakato wa uanzishwaji wa Kampuni ya kusimamia ligi kuu kuanzia msimu ujao.
HILI LITAKUWA BONGE LA MUVI!!!!YYANI WE ACHA TU
ReplyDeleteHili kweli ni muvi,na sijui stelingi ni nani,yetu macho kaka, kazi njema Dauda, its Keny.
ReplyDeleteWakaze hivyohivyo na wala wasilegeze hata kidogo...
ReplyDeletewakati fulani kwa manufaa ya baadaye yafaa kufanya maamuzi magumu, kazi ya kujenga soka letu halitakiwi kutawaliwa zaidi na siasa tumechoka kuwa wasindikizaji kwenye safari ya soka,viongozi wa vilabu huu ni wakati wenu wa kuonyesha nia yenu ya dhati katika hili,wapenzi was soka tupo numa yenu!
ReplyDeleteWamezoea kuvibana vilabu hao TFF,Wawakazie hadi kieleweke.
ReplyDelete