Rekodi ya kushinda mechi 11 ya mabingwa wa Nigeria, Enyimba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa CAF ilifutwa juzi baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Wydad Casablanca ya Morocco.
Wenyeji Wydad alifunga bao hilo pekee kupitia mchezaji wake wa akiba Pascal Angan aliyeingia na kuwapa ushindi huo mwembamba vigogo hao Morocco kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali kabla ya kurudiana Oktoba 16 huko mjini Aba.
Kama ilivyokuwa katika mchezo wao dhidi ya Raja Casablanca kwenye hatua ya makundi, Enyimba waliingia uwanjani kwa kucheza kwa kujiami kuanzia mwanzo hadi mwisho shukrani kwa kipa Paul Godwin aliyefanya kazi kubwa ya kuokoa hatari zote kwenye Uwanja wa Mohamed V jijini Casablanca.
Wydad walifanya mashambulizi kuanzia mwanzo wa mchezo na walikosa bao dakika ya 16, wakati mshambuliaji wao Mcongo, Fabrice Ondama alipofunga goli hilo lakini mwamuzi alikataa kwa madai mfungaji alisukuma beki wa Enyimba, Valentine Nwaebili.
Kipa Godwin aliziba pengo la kipa namba moja Chijoke Ejiogu, ndiye aliyekuwa sababu ya mabingwa hao wa Nigeria kufunga goli moja kwa kuokoa hatari zote.
Enyimba walikuwa kwenye hatari wakati wote wa mchezo huo nchini Morocco na dakika ya tisa beki Markson Ojobo aliokoa mpira karibu na mstari wa goli baada ya kipa Godwin kupitwa.
Mshambuliaji Uche Kalu alikuwa mbele peke yake alifika goli kwa Wydad dakika 26 na kupiga shuti la kwanza golini mwa wapinzani wao.
Katika muda huo Wydad walishaweka rekodi ya kupiga kona 14 wakati Enyimba wakiwa hawajapata hata moja hali iliyowafanya mabingwa hao mara mbili wa kombe hilo kuwa kwenye wakati ngumu.
Nahodha Chiedozie Johnson na Rasheed Olabiyi walipata kadi za njano katika kipindi cha kwanza wakati Wydada wakifanya mashambulizi ya nguvu kusaka goli.
Kipindi cha pili, Chinedu Udoji alipewa kadi ya njano na mwamuzi kwa mchezo mbaya. Kipa Godwin alikuwa na bahati ya kutolewa nje katika muda wa majeruhi wakati alipoupiga mpira nje akiwa na kadi ya njano tayari.
Search This Blog
Monday, October 3, 2011
WYDAD WAVUNJA REKODI YA ENYIMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment