Search This Blog

Tuesday, October 18, 2011

UEFA YASEMA ROONEY ANAWEZA KUPUNGUZIWA ADHABU IKIWA...................




Shirikisho la soka barani ulaya limethibitisha kwamba Miodrag Dzudovic anaweza kusaidia kupunguzwa kwa adhabu ya Wayne Rooney ikiwa mchezaji huyo kutoka Serbia ataamua kumtetea mshambuliaji wa England.


Rooney alitolewa nje kwa kumchezea rafu ya makusudi Dzudovic katika mchezo ku-qulify kucheza EURO 2012 na baadae kupelekea mchezaji huyo kupewa adhabu ya kufungiwa mechi 3 za mashindano ya timu za taifa barani ulaya, hali iliyomaanisha mshambuliaji huyo wa Man United atakosa mechi zote za makundi katika EURO 2012.


Dzudovic anaamini adhabu aliyopewa Rooney ni ya kikatili kufaninisha na kosa lake na msemaji wa UEFA amesema: Ofcourse, imewahi kutokea huko nyuma ambapo mlalamikaji akaongea kumtetea mtu aliyemfanyia madhambi na kufungiwa, lakini hatuwezi kutoa siri za hearings.Hatuna kinyongo na chochote juu suala la Dzudovich kumtetea Rooney, na uhakika kila mtu angependa kusikia sapoti ya namna hiyo.”


FA ya Uingereza bado inafikiria kukata rufaa.Wana siku 3 kabla ya kupokea ripoti nzima ya UEFA, ambayo wanategea kuipata baadae wiki hii, kuamua kukata rufaa ama vipi , lakini taarifa zinasema wanaweza kuacha kufanya hivyo kuhofia kuongezeka kwa adhabu hiyo ikiwa watashindwa.


Lakini wataamua kukata rufaa mchezaji aliyefanyiwa madhambi na Baba Kai, Dzudovic yupo tayari kusaidia. Alisema: “Sidhani kama ilikuwa sawa(adhabu). Hakuwa katika usawa wa akiakili wakati anafanya vile, hakudhamiria kuniumiza, na aliniomba msamaha mara baada tu ya kufanya tukio lile.”



1 comment:

  1. HATA MIMI SIJAIPENDA HIYO ADHABU NI KUBWA SANA KULINGANA NA 2KIO LENYEWE. MIMI KAMA SHABIKI WA ENGLAND NA UNITED SIYO FEA KABISA KWA ROONEY. WACHEZAJI WE2 WAMEKUWA WAKI2MIKA KAMA MIFANO WANAPOFANYA KOSA. WHY? PAMOJA NA HAYO KAKA MCHANGO WAKO NI MKUBWA SANA KATIKA SOCCER LA TZ, GOOD JOB.

    ReplyDelete