Search This Blog

Thursday, October 13, 2011

TEVEZ: MANCINI ANIOMBE RADHI


Carlos Tevez jana usiku ali-demand kuombwa radhi na kocha wake wa Manchester City Roberto Mancini.

Tevez, 27, amekasirika kwamba amebebeshwa mashtaka ya kukataa kucheza katika mechi dhidi ya Bayern Munich, na ikiwa leo adhabu yake ya kusimamishwa kwa wiki mbili inaisha, Carlitos yupo tayari kurejea kucheza katika ligi kuu ili kudhihirisha hakugoma kucheza dhidi ya The Bavaria.

Tevez anasema alikuwa radhi kuomba msamaha kwa kukataa ku-warm up ikiwa Mancini nae ataomba radhi kwa kusema uongo kuwa alikataa kucheza.

Tevez sasa anatarajiwa kuhojiwa na klabu on Monday.

Chanzo cha habari cha gazeti la ‘The Sun’ kilisema: “Tevez amekasirika.Anataka Mancini amuombe radhi kwa kusema uongo kuwa alikataa kucheza.

“Mambo yote yangekuwa yameisha kama wote wawili wangeomba radhi lakini City walikataa wazo hilo.”

Taarifa kutoka kambi ya Tevez zinasema kuwa Carlitos alikataa kupasha kwa sababu tayari alishafanya hivyo, lakini upande wa Man City wanaonekana wapo upande wa Mancini na leo uongozi wa klabu hiyo ulimzuia mshambuliaji huyo asiudhurie mazoezi ya asubuhi ya kikosi cha kwanza.

City wamedhamiria kumpiga faini ya £1.5milllion na kumfungia zaidi kwa wiki nne.

No comments:

Post a Comment