Kocha mpya wa Yanga Mserbia, Kostadin Papic jana alianza rasmi kazi ya kuinoa timu hiyo kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.
Papic alisimamia mazoezi ya Yanga jioni yaliyofanyika Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya watani wao wa jadi, Simba utakaofanyika Jumamosi wiki ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Jana asubuhi Yanga ilifanya mazoezi katika uwanja huo yaliyosimamiwa na Mganda Sam Timbe, ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Yanga kabla ya jioni kuachia jukumu hilo kwa Papic.
“Tumemrudisha Papic, kama unavyoona ameanza rasmi kazi, masuala yanayohusu mkataba wake tutaeleza, lakini kwa sasa ndiyo kama unavyomuona,” alisema Ofisa Habari wa Yanga, Luios Sendeu jana.
Kuhusu mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Simba utakaofanyika Jumamosi ijayo, Sendeu alisema maandalizi yanaendelea na kuwa mahali ambapo wataweka kambi wataeleza wakati ukifika.
Search This Blog
Tuesday, October 25, 2011
PAPIC ACHUKUA MAJUKUMU RASMI YANGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment