Blog yako namba 1 ya michezo leo itakuletea mtiririko wa matukio yote yatakayotokea kwenye mchezo wa mwisho wa kutafuta nafasi ya kushiriki AFCON 2013, kati ya Tanzania dhidi ya Morocco moja kwa moja kutoka nchini Morocco.
KIKOSI CHA TANZANIA.
Kocha Jan Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 11 ambao wataanza kwenye mechi ya leo dhidi ya Morocco. Mechi hiyo inaanza saa 1.30 usiku kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania ni saa 4.30 usiku na itachezwa Grand Stadium hapa Marrakech. Poulsen atatumia mfumo wa 4-4-1-1 huku akimweka Mbwana Samata kuwa mshambuliaji wa mwisho na nyuma yake akicheza Abdi Kassim.Katika kikosi cha kwanza amewaanzisha wachezaji wote wa kulipwa wanaocheza nje ya Tanzania ambao anao hapa. Amewataka wachezaji kuwa focussed na mchezo, kujituma na kila mmoja kutekeleza wajibu wake uwanjani ili ushindi uweze kupatikana. Baada ya kutoa game plan yake, Poulsen aliwaonesha wachezaji CD ya mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya Morocco ambapo tulifungwa bao 1-0.
Kupitia CD hiyo aliwaeleza wachezaji upungufu uliojitokeza na pia wachezaji hatari wa Morocco wanaotakiwa kuangaliwa kutokana na uzuri wao wanapokuwa uwanjani. Amewakumbusha mabeki kuwa mshambuliaji Chamakh Marouane (Arsenal, Uingereza) kuwa ni mzuri kwa mipira ya vichwa, hivyo kutomuacha kuruka peke yake katika mipira hiyo.
Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Idrisa Rajab, Juma Nyoso, Aggrey Morris, Shabani Nditi, Mohamed Rajab, Henry Joseph (Captain), Mbwana Samata, Abdi Kassim na Dan Mrwanda. Subs: Shabani Dihile, Nassoro Cholo, John Bocco, Ramadhan Chombo, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Jabir Aziz.
Aisee wadau game ndo inataka kuanza uwanja umejaa kweli kweli :
ndo wimbo wa taifa unaimbwa so wote tuimbe..
nyimbo za mataifa yote zimemalizika muda wowote mpambano utaanza...
Tanzania wamevaa jezi ya blue na na bukta nyeusi wakati morocco wamevaa jezi nyeupe na bukta nyeusi,
DK 1: GOAL KICK KUELEKEA GOLI LA MOROCCO
DK 2: ADEL TAALABT ANAKOSA BAO LA WAZI
DK 4: MOROCCO WANAKOSA TENA BAO LA WAZI
DK 8: POSSESION BADO IPO KWA MOROCCO
DK 14: MOROCCO ALMANUSURA WAFUNGE KICHWA CHA CHAMAKH KIMEGONGA MWAMBA,MPIRA UKARUDI NDANI LIKAPIGWA SHUTI JUMA KASEJA AKADAKA..
DK 20: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO !!!MAROUNE CHAMAKH ANAIPATIA MOROCCO BAO LA KUONGOZA..
DK 24: KONA YA IDDRISSA RAJAB INADAKWA NA KIPA WA MOROCCO.
DK 25: ADEL TAARABT ANAMFINYA JUMA NYOSO SHHUTI LAKE LINAPAA SENTIMITA CHACHE..
dk 38: morocco bado inaongoza bao 1:0 wakti huo huo JUMA KASEJA ANAOKOA BAO LA WAZI..
DK 40: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!! ABDI KASSIM BABI ANAISAWAZISHIA TANZANIA
DK: 42 JUMA KASEJA ANAOKOA BAO LA WAZI SHUTI LA ADEL TARAABT
DK 44: JUMA KASEJA AMELALA CHINI NAONA ANAPULIZIWA DAWA KWENYE KISIGINO
DK 45: SAIVI NI MAPUMZIKO MATOKEO BADO NI BAO MOJA KWA MOJA
ALGERA 2:0 AFRICA YA KATI - HT
DK: STARS WANAFANYA MABADILIKO ANAINGIA SAID NASSOR CHOLLO
TANGIA KIPINDI CHA PILI KIMEANZA MCHEZO UNAONEKANA KU-BALANCE NAFIKILI MOROCCO WAMEPATA MATOKEO YA AFRIKA YA KATI KUWA NYUMA KWA ALGERIA,MATOKEO AMBAYO YANAWAPA NAFASI YA KUFUZU HATA KWA SARE YA LEO..
DK 55: JUMA KASEJA ALIKUWA CHINI SASA AMEAMKA NA MCHEZO UNAENDELEA KAMA KAWAIDA..
DK 61: JUMA NYOSSO ANAPEWA KADI YA NJANO..
DK 65: MRISHO NGASSA ANAINGIA BADALA YA ATHUMAN MACHUPPA
DK 68: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!! ADEL TAARABT ANAIPATIA MOROCCO BAO LA PILI KWA FREE KICK ...
DK 80: AMETOKA MBWANA SAMATTA AMEINGIA JOHN BOCCO ,BADO MOROCCO INAONGOZA MABAO 2-1.
DK 88: CHAMAKH ANATOKA NA NAFASI YAKE INACHUKULIWA NA FETTAR
DK 89: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!! MOROCCO WANAPATA BAO LA TATU..
DK 90 : JUMA KASEJA ANAOKOA BAO HAPA
FULL TIME : MOROCCO 3-1 TANZANIA.
FULL TIME: Algeria 2-0 Central African Republic.
mechi imeanza?
ReplyDeleteKanyaga twnde kaka,TBC ambayo n television ya taifa hawana hata mpango,Hii nch bwana,hata shirika la nch linakosa uzalendo?
ReplyDeleteDUH HAL C NZUR,THE BOYZ NEED 2 CONCETRATE
ReplyDeletewapenda soka mkitaka kucheki live mechi ya stars tumieni link hii kwa wale wenye access na internethttp://www.justin.tv/ssouff.
ReplyDeleteBARAKA.
yes imeanza
ReplyDeleteBado kuna matumaini. Goli 1 c kitu saaana
ReplyDeleteChannel gani naweza kuona match?
ReplyDeleteMh! yashakuwa maji ya shingo tayari cjui kama 2taweza kuyaogelea.
ReplyDeleteimekula kwe2, ngoja nikalale tu
ReplyDelete1-1 naona vijana wanataka kulinda heshima ya nchi yetu. We need more goals boys
ReplyDeleteDu vijana wanajitahdi kwel labda 2tatoka.
ReplyDeleteShaffih umelala? Mbona hutupi update kwamba sasa ni halftime na tumesawazisha ni 1-1?
ReplyDeletehamna ktu hapo mpira uwanjani c mdomoni.
ReplyDeleteRoo kama 2melogwa..
ReplyDeleteMwenzenu nimemmiss Maximo!
ReplyDeletePoleni vijana karibuni nyumbani,kuteleza si kuanguka,kufungwa tumezoea, ushindi kwetu ni bahati mbaya karibuni stars.
ReplyDeleteNashukuru kwa kutupatia matokeo mwanzo mwisho lakini naomba uitathmini(uichambue) Kinagaubaga mechi hii mwanzo hadi mwisho kupitia Clouds fm,...its me Athumani S Mpoki wa ARUSHA.
ReplyDeleteNi matokeo ambayo kila mtu anayejuwa soka aliyategemea.Huo ndio ukweli tuache kudanganyana eti kwenye soka lolote linaweza kutokea.Soka sio mchezo wa bahati nasibu.Chama chetu cha soka kinastahili lawama hizi kwani kimeshindwa kubuni mfumo mzuri wa kututoa hapa.
ReplyDeleteNadhani pale TBC tangu alipoondoka Tido na Juma mambo yamerejea yaleyale ya mwaka 47!
ReplyDeleteHata hivyo kwa maandalizi ya stars kupitia kwa viongozi mpaka kocha kupitia kwa wachezaji matokeo yanaridhisha sana tena sana maana mpaka timu inaondo haijapata hata mechi moja ya maandalizi kujua baya na zuri tulitegemea matokeo tofauti na hayo{kocha kafanya kazi yake maridadi, wachezaji wajitahidi kututetea watanzania lakini imeshindikana nao wamefanya kazi yao ipasavyo, sasa ambao hawajanya kazi yao ni TFF
ReplyDeletebora tumetolewa labda tutajipanga vizuri na iwe fundisho.....
ReplyDelete