Search This Blog

Monday, October 24, 2011

LIGI KUU YA ENGLAND KWENYE NAMBA - MAN UNITED WAFUNGWA NYUMBANI BAADA YA MECHI 26


0 - Bolton Wenderers ndio pekee ambayo katika zote za madaraja yote manne haijapata hata pointi katika uwanja wa nyumbani kufuatia kufungwa na Sunderland 2-0 @Reebok Stadium.


3 – Wolverhampton Wnaderers imekuwa ya tatu pekee ambazo zilipata pointi baada ya kutanguliwa kwa magoli mawili kwa bila.


3 – Danny Graham sasa amefunga magoli matatu mfululizo katika mechi za Barclays premier league kwa timu yake ya Swansea City.


4 – Rafael Van Der Vaart sasa amefunga katika mechi nne mfululizo katika mechi za ligi kwa Tottenham Hotspur.Magoli yake mawili dhidi ya Blackburn yanamaanisha amefunga magoli matano katika ya nane ya mwisho yaliyofungwa na Spurs.


5 – Tottenham Hotspur sasa wameshinda mechi zao tano za mwisho walizokutana na Blackburn, baada ya ushindi wa 2-1 @Ewood Park.

5 – Ushindi wa Everton wa 3-1 dhidi ya Fulham at Craven Cottage unamaanisha kwamba wameshinda mechi tano na kudroo moja katika michezo sita ya mwisho walizokutana na Fulham.

5 - Michezo mitano ya mwisho kati ya Aston Villa na West Bromwich Albion yote imeisha kwa matokeo ya 2-1, huku Villa wakishinda mara 3.

6 – Kufungwa goli 1-6 dhidi ya mahasimu wao Man City, ndio kilikuwa kipigo cha kwanza kwa Manchester United kuruhusu wavu wao kuguswa mara 6 wakiwa Old Trafford.

6 – Liverpool wameshindwa kuzuia wavu wao kuguswa katika mechi zao 6 wakiwa Anfield, matokeo mabaya kuwahi kutokea tangu mwaka 2003.

6 – Wigan Athletic sasa wamepoteza mechi zao 6 mfululizo za EPL, baada ya kufungwa bao 1-0 na Newcastle.

7 – Bolton Wanderers sasa wamepoteza zao saba za EPL wakiwa nyumbani.Matokeo mabaya zaidi tangu warudi premier league.

9 – Chelsea walipata kadi tisa – mbili nyekundu na saba za njano – katika kufungwa kwao na QPR kwa 1-0.

12 – Newcastle United hawajafungwa katika mechi 12 za premier league kwa mara ya kwanza tangu mwezi wa tatu mpaka wa nane mwaka 1997.

16 – QPR waliwafunga majirani zao Chelsea kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 16 na kuweka rekodi ya kushinda mechi ya kwanza wakiwa nyumbani tangu warejee katika epl.

26 – Manchester United wamefungwa nyumbani kwa mara ya kwanza ndani ya mechi 26, tangu walipofungwa na Chelsea in April 2010.Ushindi wa City wa 6-1 ulimaliza mbio za vijana wa Ferguson kushinda mechi 19 wakiwa OT.

33 – Manchester City wamefunga mabao 33 msimu huu na kuweka rekodi mpya kwa kufunga magoli mengi katika mechi tisa, wakiivunja rekodi ya Arsenal ya mabao 29 in 2004/05.

No comments:

Post a Comment