Defence yao inaweza kuchukua sifa katika uongozi huu wa timu yao, wameruhusu mabao matano tu kwenye mechi 7, ni rekodi ya kuvutia, tena ukizingatia matatizo ya majeruhi kwenye safu ya ulinzi tena kipindi hiki ambacho viraka kama John O’shea na Wes Brown wakiwa wameondoka kwenda Sunderland.
Pamoja na rekodi nzuri kwenye safu ya ulinzi, United msimu huu ndio timu iliyopigiwa mashuti mengi kuliko timu yoyote kwenye ligi, wakipigia mashuti 97 langoni mwao katika michezo 7.
TAKWIMU
Kwenye graph hapo juu takwimu zinaonyesha United wame-concede shots 13 au zaidi katika kila mchezo.Mchezo dhidi ya Stoke City ndio mchezo pekee ambao United hawakuruhusu shots nyingi.
Pia kwenye graph nyingine hapo chini inaonyesha katika michezo saba, United wameruhusu mashuti mengi langoni mwao kuliko waliyopiga.
MAHALI YALIPOPIGWA MASHUTI
KWANINI?
Turudi kwenye swali-kwanini? Kupitia ushahidi wa takwimu unaonyeshwa hapo juu, kwanini United wameruhusu kupigiwa mashuti kutoka kwenye umbali mrefu? Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kuwa majibu kwanini United wamepigiwa sana mashuti mengi langoni mwao.
1: FIKRA ZA DAVID DE GEA KUWA NA UDHAIFU KWA MIPIRA YA MBALI?
Baada ya kufungwa bao la mbali na Edin Dzeko katika mechi ya ngao ya hisani, watu wengi walianza kuhoji udhaifu wa De Gea katika kuzuia mipira ya mbali.Kupitia system ya Opta takwimu zinaonyesha De Gea alikuwa na rekodi mbovu katika kuzuia mashuti ya mbali msimu uliopita katika La Liga.
Je ni kweli De Gea ni mdhaifu kwa mipira ya mbali? Katika kesi hii sio rahisi kupata jibu sahihi ukizingatia kipindi kifupi alichocheza, lakini la kuzingatiwa ni kwamba wapinzani wanafikiri De Gea ana udhaifu huo, na ndio maana wamekuwa wakijaribu kumtungua kutokea umbali wa 20+ yards.Hitimisho ni kwamba Da Gea bado hajafungwa goli nje ya box katika premier league.
2: MAJERUHI KWENYE ULINZI
Rio Ferdinand na Nemanja Vidic wote wamekuwa majeruhi, Chris Smalling na baadae Antonio Valencia wamekuwa wakichezeshwa katika nafasi beki wa kulia.United defence wame-cope vizuri na hali hii ya majeruhi, lakini swali ni kwamba je wameweza kujenga partnership nzuri kwenye ukuta wao, particularly wakati beki wa kati mmoja anapoenda mbele mwingine anakuja na ku-cover, kama goli la Fernando Torres @Old Trafford lilivyoonesha.Ferdinand na Vidic wamekuwa na wakitengeneza partnership nzuri ya namna hiyo tofauti na Phil Jones na Evans.
3: HAKUNA KIUNGO MZURI MZUIAJI
Kuna utata whether Micheal Carrick ni kiungo mzuiaji au sio, lakini ni mzuri zaidi ya wote wawili Anderson na Tom Claverley katika uzuiaji, Ferguson amekuwa akipenda midfield partnership katika msimu huu.Mtindo wa kuvutia wa 4-4-2 wa United msimu uliopita ndio ulikuwa chanzo cha mchezo mzuri wa United msimu uliopita kupitia viungo Micheal Carrick, Paul Scholes, Fletcher, na Anderson ambao Ferguson alipenda kuwatumia kama two passer na two runners kwa pamoja.
Cleverley ni kiungo mzuri sana, akicheza zaidi kwa mtindo wa kushambulia zaidi kuliko kiungo yeyote aliyetajwa hapo juu, na kumtumia yeye na Anderson kunaacha gap kubwa katika midfield na defence.Carrick, akiwa yupo mbali na kuwa mtu mzuri kufanya tackling, lakini bado kuna wengine wanm-favour yeye kucheza katika nafasi, yupo vizuri katika kufanya tracking and intercepting.United wanaweza kuwa bora bila yeye, lakini katika uzuiaji sio wagumu kabisa.
4: ROONEY HAFANYI KAZI KUBWA?
Kama Stewart Robson alivyosema hivi karibuni, Rooney akiwa katika form nzuri kama true namba 10 amekuwa akimbii sana bila kuwa na mpira.Alikuwa anafanya kazi kubwa kipindi wakati akicheza pembeni kipindi United ilipokuwa dominated na Cristiano Ronaldo na alifanya kazi kubwa zaidi alipokuwa anatumika kama mshambuliaji pekee.Sasa, mfano mzuri wa aina yake ya mchezo kuwa madhara ilikuwa katika fainali ya Champions league dhidi ya Barca, matatizo ya safu ya kiungo cha United yalianzia kutokana na aina hii mchezo, Rooney akiwa hashuki sana kuja kukaba na ku-cover, matokeo yake viungo walikuwa wakifanya kazi kubwa mbele kwenye pitch, na wakiacha gap kubwa nyuma yao.
Sababu nyinginezo.
Performance ya katika kombe la ngao ya hisani ilionyesha utofauti mkubwa kutoka kwa United ya msimu uliopita.In 2010/11walikuwa well defined na organized vizuri.Sasa, wanacheza zaidi wakiwa katika mtindo wa free-flowing and flexible, matokeo yake wanakuwa wanashambulia zaidi kwa pamoja katika ushirikiano mzuri lakini wakiachia nafasi zaidi kwa wapinzani katika midfield.Katika mtindo wa uchezaji wa sasa wachezaji kama Ashley Young na Nani watakuwa favoured kuliko Ji sung Park na Antonio Valencia wachezaji ambao ni wazuri katika kucheza kwa nidhamu kubwa ya ukabaji.
HITIMISHO
Sifa ya De Gea ya kuwa mbovu kwa mipira ya mbali inaonekana wazi kuchangia, na kama Rooney ataendelea kucheza mchezo wa kutokushuka chini, then Cleverley na Anderson watakuja kuwa exposed na timu yoyote nzuri kubwa kama Real Madrid au Barca katika stages za mbele msimu huu.
Tatizo la majeruhi kwa United halionekani kuchangia sana , Evans, Jones na Smalling wanaonekana kucheza vizuri sana.
ila nadhani mpaka sasa De Gea kashawa prove wrong watu wengi sana. so far anafanya vizuri sana!!!
ReplyDelete