Manchester City wamempiga faini Carlos Tevez ya kumkata mshahara wa wiki 4 baada kupatikana hatia ya kufanya matendo yasiyoridhisha.
Carlitos pia ameonywa kutokana na tabia yake aliyoionyesha kwenye benchi wakati timu yake ikicheza na Bayern Munich in Champions league.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alienda kusikiliza shauri la mashtaka yake Ijumaa iliyopita, ameadhibiwa kwa kupewa adhabu ya wiki mbili ambayo kimsingi tayari ameshaitumikia.
Tevez alisimamishwa kwa wiki mbili wakati City wakiwa wanafanyia uchunguzi tuhuma za Mancini dhidi yake kwamba Muargentina huyo alikataa kuingia kama sub katika mchezo wao waliofungwa na Bayern Munich @Allianz Arena.
Tevez alipinga madai hayo akidai kulikuwa na kutokuelewana akisema alikataa kupasha tu kwa sababu haikuwa lazima kufanya kwakuwa tayari alishafanya hivyo kabla.
Tevez ana siku 14 za kuamua kukata rufaa au kutokata rufaa kwa bodi ya wakurugenzi wa City.
Kwa hivyo sasa Tevez yupo huru kuitumikia City ikiwa manager wake Mancini ataona anafaa kutumika katika kikosi chake, jambo ambalo linaonekana kuwa gumu.
No comments:
Post a Comment