Vinara wa Ligi Kuu Simba pamoja na kuongoza kwa pointi 18, pia wanaongoza kwa utovu wa nidhamu sambamba na Villa Squad wakiwa na jumla ya kadi 20.
Msimu huu umeonekana kushamiri kwa matukio ya utovu wa nidhamu kulingana na kadi ambazo zimeshatolewa na waamuzi wa ligi mpaka sasa, ambapo tayari zimetolewa kadi 223, huku kadi nyekundu zikiwa 15 na njano 208.
Simba, Villa Squad, Kagera Sugar na Toto African zimeibuka vinara kwa kadi nyekundu na njano.
Villa imeibuka kinara wa kadi za njano baada ya kumiliki kadi hizo 20, Simba 19 na Toto African 18 huku ikiwa kadi 208 zimeshatolewa na waamuzi wa ligi hiyo kwa michezo 55 iliyochezwa sawa na uwiano wa kadi tatu kila mechi.
Kagera Sugar imeibuka kinara wa kadi nyekundu baada ya kumiliki kadi hizo tatu kati 15 zilizotolewa na waamuzi kwa michezo yake minane iliyocheza.Katika michezo hiyo 55 ya Ligi Kuu bara jumla ya mabao 108 yamepachikwa kimiani sawa na uwiano mabao mawili katika kila mchezo.
Washambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Moro Utd na John Boko wa Azam FC wanaongoza kwa kuzifumania nyavu baada ya kila mmoja kuifungia timu yake mabao matano kwa michezo minane waliyoshuka dimbani.
Hata hivyo, timu zilizopanda Ligi Kuu bara msimu huu, Moro Utd na Villa Squad zinaongoza kwa kufungwa mabao mengi, Moro imeruhusu mabao 15 kuingia kwenye wavu wake na kufunga 12, wakati Villa imefungwa 13 na kufunga matano katika michezo minane iliyocheza kwenye ligi hiyo.
Search This Blog
Thursday, September 29, 2011
SIMBA WAONGOZA LIGI NA NIDHAMU MBOVU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment