Search This Blog

Wednesday, September 14, 2011

SABABU 10: KWANINI REAL MADRID WAMESHINDWA KUCHUKUA CHAMPIONS LEAGUE KWA MIAKA 10


Real Madrid ni moja klabu kubwa na tajiri duniani, iliyo na historia kubwa ndani na nje ya mipaka ya Spain.Real Madrid ndio klabu yenye historia ya kuchukua mara nyingi kombe la klabu bingwa ya ulaya, wakiwa wamelishika kwa mara tisa.

Pamoja na historia kubwa iliyonayo kwenye Champions league, lakini katika miaka ya karibuni timu hiyo imekuwa na hali ngumu sana inapokuja suala la kushinda ubingwa wa ulaya, mara ya mwisho kwa klabu hiyo kuchukua ubingwa wa ulaya ilikuwa pale jijini Glasgow-Scotland mwaka 2002, walipoifunga Bayern Leverkusen, shukrani kwa bao la Zinedine Zidane.

Msimu huu wa 2011-12 ni msimu wa 10 tangu mabingwa hawa wa mara tisa kuligusa kombe hilo, lakini ni kwanini imewachukua muda mrefu Madrid kuweza kuwa washindani tena?

SABABU 10

FROLENTINO PEREZ & MAGALACTICOS

Florentino Perez aliingia madarakani kwa mara kwanza Santiago Bernabeu mwaka 2000, na kwa haraka alifanya usajili ulioleta mtafaruku mkubwa katika historia ya klabu hiyo, baada ya kipenzi cha Barcelona Luis Figo alipohama Catalunya na kuwa Galactico wa kwanza.

Madrid waliingia katika millennia mpya wakiwa sera mpya ya usajili ya kutumia fedha nyingi.

Falsafa ya Perez ya kuwavutia wachezaji wenye vipaji na kuwaweka pamoja na chipukizi wa klabu ilileta mafaniko ya haraka mwaka 2002 kwenye Champions league, lakini baadae ikapelekea kuanza kwa ubinafsi miongoni mwa mastaa wa klabu hivyo kuiacha klabu ikiwa haina umoja.Uwepo wa wachezaji mastaa kama David Beckham, Ronaldo de Lima, Micheal Owen, Zinedine Zidane, Luis Figo, ulileta mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wachezaji kati yao na wachezaji wengine wa kawaida na waliokulia ndani ya klabu ile.

As a result , haikuonekana kama kuna timu inayojengwa katika uongozi wa kwanza wa Perez, zaidi ya kuonekana kama ni story ya mfanyabiashara mwenye nguvu akiwakusanya wachezaji kwa namna yoyote aliyotaka.Je experience aliyoipata imempa fundisho? Hapana mwaka 2009 alipochaguliwa tena alifanya kufuru kwa kutumia zaidi ya €250 million kukusanya Magalacticos, lakini mpaka sasa hajapata faida.

KUONDOKA KWA VICENTE DEL BOSQUE

Mafanikio ya hivi karibuni ya Vicente Del Bosque kwenye Kombe la Dunia yame-highlight uwezo wake kama kocha, na kwenye uongozi wake pekee ndio Madrid ilionekana kufanya kazi kwa umoja na mafanikio.

Nini kilichomfanya aondoke kipindi cha kiangazi mwaka 2003, pamoja na kushinda makombe mawili ya ulaya in 2000’s, kombe ambalo Madrid wanalithamini na kulipenda kutokana na historia yake lakini bado Perez hakuridhika.

Inawezekana kutokupenda kupelekwa pelekwa kwa Del Bosque kulileta kutokuelewana na uongozi wa Perez na hatimaye akaondoka Bernabeu.

KUMRUHUSU CLAUDE MAKELELE AONDOKE

Katika miaka ya hivi karibuni kwenye soka, Claude Makelele anatajwa kama kiungo bora wa ulinzi kuwahi kutokea duniani.

Madrid wakiwa chini ya Del Bosque, Makelele alikuwa na msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho haswa kipindi timu inapoenda mbele kushambulia, mfaransa alikuwa kama cover katika counter attacks, timu ilipopoteza mpira wachezaji wenzake wakiwa wanarudi kuchukua nafasi zao, Makelele alikuwa ameshafika mbele ya ukuta wa mabeki wan ne, tayari kupokonya mpira na kupeleka mbele.

Majukumu yake ndani ya uwanja yaliisadia Madrid kuwa wagumu zaidi nyuma, na tatizo pekee alilokuwa nalo ni nidhamu mbovu.Alipoondoka kwenda Chelsea in 2003, alijitengenezea legacy for himself, na alifanya kila kitu @ Stamford Bridge na kama angeendelea kuwepo Bernabeu angeisaidia sana Madrid.

UKAME WA MABEKI KIKOSINI

Florentino Perez alikuwa hataki kabisa kununua mabeki katika awamu ya kwanza ya uongozi, akisema kwamba kufanya hivyo kutawafanya waonekane “wadhaifu”.Kutoka kuondoka kwa Madrid;s Legend Fernando Hierro in 2003, wengi waliletwa lakini kwa bahati mbaya hawakufikia standard iliyohitajiwa.

Francisco Pavon, Raul Bravo, Ivan Helguera(ambaye hakupenda kucheza kama beki wa kati), hata Raul Albiol na Ezequiel Garay, wote walipewa majukumu na wakashindwa.Ingawa Perez alimsajili Walter Samuel kutoka Roma in 2004, lakini alipatwa na mkosi na hakucheza vizuri.

Hata baada ya Fabio Cannavaro na Pepe kununuliwa, ni wakati huu tu ndio ukuta wa Madrid unaonekana upo stable na ume-settle.Imewachukua muda mrefu kufikia mafanikio haya.

MAKOCHA WA AINA YA “NDIO MZEE”

Baada ya Del Bosque kuondoka, Madrid walianza kutafuta mrithi wake, ambaye angekuwa mtu tofauti na kocha aliyepita kwa kutopingana na sera na Boss(Perez)

Alianza Carlos Quieroz aliyewasili kutoka Manchester United lakini akadumu kwa msimu mmoja kabla ya kufukuzwa.Miaka miwili ya mbele msururu wa makocha wakaja Santiago bernabeu, Antonio Comacho aliyedumu kwa mwezi tu, Mariano Garcia Ramon aliondoka katika Christmas ya 2004, na mbrazil Vanderlei Luxemburgo akidumu kwa miezi 12.

Hali ilizidi kuwa mbaya chini ya Juan Ramon Lopez, ambaye aliweka rekodi kutokushinda mechi nyingi zaidi akifuata nyayo za Jupp Heynckes in 1996-97, alifukuzwa mwaka 2006.

Awamu ya pili ya Perez baada ya kurudi madarakani mwaka 2009, Manuel Pellegrin alipewa timu, na akiwa anaheshimika japo sio sana, watu wengi bado walimuona kama ni mmoja kati wa makocha ya aina ya “ndiyo mzee”, baadae alitimuliwa na nafasi yake ikachukuliwa na Jose Mourinho.

MKOSI WA HATUA YA 16 BORA

Kwa klabu iliyokuwa na rekodi bora kwenye Champions league, kushindwa kwao kuendelea baada ya hatua ya 16 bora kwa miaka 6 mfulululizo pamoja na kuwa wachezaji wengi wenye vipaji vikubwa, unabaki kuwa mkosi.

Kikosi cha Mourinho kilimaliza mkosi huo msimu uliopita kwa kuwatoa Lyon, na hatimaye kutolewa na Barcelona kwenye nusu fainali, lakini miaka ya mkosi bado iliwaandama sana :Juventus, Arsenal, Bayern Munich, Roma, Liverpool na Lyon wote walihusika kupeleka msiba kwa wahispania hao kutokea mwaka 2004 mpaka 2010.

SAMUEL ETO’O

Kama kuna mchezaji Real Madrid wanajuta kumuuza basi ni Samuel Eto’o.

Samuel Eto’o alijiunga na Real Madrid in 1997, lakini hakuweza kujiunga na kikosi cha wakubwa na hatimaye baada ya kuhangaika klabu tofauti na hatimaye mwaka 2004 alihamia Barcelona ambapo alipata mafanikio makubwa akiisaidia timu hiyo kushinda makombe kadhaa yakiwemo mawili ya klabu bingwa ya ulaya na kuwaacha Madrididistas waki-wonder nini Mcameroon angewafanyia kama asingeondoka klabuni kwao.

BARCELONA

Kwa takribani miaka 6 Real Madrid wamekuwa wakikimbiza kivuli Barcelona wakiteswa ulaya na nyumbani.

Barcelona walikuwa wameshinda ubingwa mmoja tu wa ulaya wakati Madrid wakibeba ubingwa wa ulaya kwa mara ya tisa @ hampden Park in 2002, lakini tangu kipindi hicho, the Catalan giants wameibuka kuwa mtawala wa Spain.

Kwa miaka yote hiyo ni msimu uliopita pekee ambao Madrid walionyesha kidogo upinzani katika UCL semi-finals.Timu hizi mbili za Hispania zilikuwa zinatajwa kama ndio vilabu vyenye nguvu zaidi ulaya, na kama isingekuwa Barca na mchawi wao Muargentina, Madrid wangekuwa na nafasi kubwa ya kubeba kombe lao walilolimisi kwa takribani miaka 10.

UKIBURI NA KUJIONA NDANI YA KLABU

Mafanikio, utajiri na umaarufu katika ulimwengu wa soka ulileta hali ya kujiona na ukiburi mbele ya timu nyingine.Kuwasili kwa wachezaji wenye majina makubwa , waliokuwa wakilipwa mishahara mikubwa kuliko kulileta situation ya kujiamini kwa kupitiliza huku wakiamini medali za ubingwa zitakuja kwa haraka.

Mfano mzuri ni katika sakata la Fernando Morientes aliachwa aende kwa mkopo Monaco in 2003 bila masharti yoyote kuwekwa kwenye mkataba kama vile kumzuia Morientes kucheza dhidi ya Madrid in Europe ikiwa timu hizo mbili zikikutana.Mwisho wa siku walijutia ukiburi wao na kujiona baada ya Morientes kuwafunga mara mbili katika robo fainali na kuwaacha Wafaransa hao wakiendelea mbele na kufika mpaka fainali ya UCL in 2004.

UTAWALA WA DRESSING ROOM

Japokuwa kulikuwepo masupastar wengi kutoka nje ya Spain, lakini mashujaa wazawa kama vile Raul na Guti walibaki kuwa vipenzi vya Madridistas, na watu wote walikuwa wanatambua nguvu walio nayo ndani ya maamuzi ya klabu.

Raul alikuwa kalishika sikio la kila raisi wa klabu aliyekuja na kuondoka, hivyo aliweza hata ku-influence sera za timu uwanjani, hali iliyopelekea makocha kutengwa na kutokuwa na sauti ndani ya klabu, ndio maana wachezaji hao ndio walikuwa wa kwanza kuondoka mara tu Mourinho alipochukua madaraka alipowasili Santiago Bernebeau in 2010.

1 comment:

  1. Poa kaka sina ubisha kwa uchambuz wako
    karıbu
    www.gshayo.blogspot.comPoa kaka sina ubisha kwa uchambuz wako
    karıbu
    www.gshayo.blogspot.com

    ReplyDelete