Chelsea chini ya Andre Villas Boas wamecheza michezo mitatu ambayo hadi sasa wamejikusanyia pointi 7. Kama unakumbuka Vizuri , msimu uliopita Sunderland ni moja ya timu zilizoitesa Chelsea msimu uliopita wakiwafunga The Blues bao 3-0 darajani Stamford Bridge.
Sunderland iliyoifunga Chelsea si sunderland hii iliyopo Leo kwani kipindi kile alikuwepo Danny Welbeck ambaye amerejea nyumbani United , alikuwepo Darren Bent ambaye ameuzwa Aston Villa , alikuwepo Nedum Onuoha ambaye naye kama Welbeck amerejea nyumbani Man City.
Kuondoka kwa wachezaji hao kumefagia njia ya kuingia kwa wachezaji kadhaa wakiwemo John O’shea na Wes Brown toka Man United , Nicklas Bendtner naye amekuja toka Arsenal na Sebastian Larson toka Birmingham City.
Kwa mchezo dhidi ya Chelsea Sunderland watamkosa John O’shea na hii inamaanisha kuwa beki Phil Bardsley atahama toka kushoto alikozoea na kuja kwenye nafasi ya beki wa kulia huku Kieran Richrdson akijaza nafasi yake kama beki wa kushoto na huenda atasaidiwa na Jack Colback huku Wes Brown akicheza katikati na Titus Bramble ambaye anakuja kuziba pengo la Anton Ferdinand aliyeuzwa QPR.
Kwa upande wa ushambuliaji Bruce huenda akamuanzisha Asamoah Gyan huku Stephane Sessegnon akisimama nyuma yake na Bendtner atakuwa benchi pamoja na kucheza vizuri katikati ya wiki akiwa na timu yake ya taifa na Anton Gadner na Seb Larson watacheza pembeni.
Kwa upande wa Chelsea bado Didier Drogba ataendelea kukosekana baada ya ajali aliyopata kwenye mchezo uliopita . Taarifa njema kwa mashabiki wa Chelsea ni kurejea kwa kipa Petr Cech ambaye amekosa takribani wiki tatu baada ya kuuumia goti .Boas pia atakuwa na David Luis ambaye atakuwa benchi baada ya kurudi baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Raul Meireles pia atakuwa benchi na inatarajiwa kuwa kuwa Juan Matta ataanza baada ya kucheza vizuri mara ya mwisho dhidi ya Norwich City .
Upande wa beki watakuwepo Nahodha John Terry ambaye atacheza pembeni ya Branislav Ivanovic huku Jose Bosingwa ambaye anaonekana kuzaliwa upya msimu huu akicheza upande wa beki ya kuli akisaidia kupandisha mashambulizi kwa upande huo huku Ashley Cole naye akifanya hivyo hivyo upande wa kushoto.
Safu ya kiungo itakuwa chini ya Ramires , Frank Lampard, na John Obi Mikel wakigawana majukumu ya kucheza kwenye injini ya chini kwa Ramires na Obi na injini ya juu ikiwa chini ya Lampard.
Andre Villas Boas atawatumia Florent Malouda , Juan Mata na Fernando Torres kweney safu ya ushambuliaji ambayo kwa vyovyote itafanya jitihada za hali na mali kumsaidia Fernando Torres afunge baada ya kufunga bao moja katika michezo 27 ya Chelsea .
Hadi sasa Sunderland wamefunga bao moja tu lililowekwa wavuni wakati msimu unaanza kwenye mechi dhidi ya Liverpool katika mchezo ulioisha kwa sare pale Anfield .
Sunderland wamekuwa wakicheza vibaya kwenye uwanja wao wa nyumbani tangu mwaka huu uanze ambapo wamevuna pointi 7 pale Stadium Of Light huku wakiwafunga Wigan 4-2 mara ya mwisho mwezi Aprili.
Hadi sasa Sunderland wameweza kuvuna kadi nane za njano huku Phil Bardsley akiwa mchezaji pekee aliyeonyeshwa kadi nyekundu na Chelsea wamepata kadi za njano 6 hadi sasa.
Sunderland waliifunga Chelsea 3-0 mara ya mwisho msimu uliopita huko Stamford Bridge lakini Chelsea nao walishinda huko Stadium Of Light kwa matokeo ya 4-2.
Mara ya mwisho kwa Chelsea kupata ushindi ugenini ilikuwa mwezi Aprili ambapo waliwafgunga West Brom 3-0 kwenye uwanja wa The Hawthorns.
Katika mara sita za mwisho walizocheza huko Stadium Of Light Chelsea wameweza kushinda mara zote huku mara pekee ambayo walishindwa kupata pointi zote tatu ikiwa mwaka 2001 wakati timu hizi zilipotoka sare ya bila kufungana .
No comments:
Post a Comment