Search This Blog

Tuesday, September 27, 2011

LIGI YA UINGEREZA KWENYE NAMBA


0: Fulham hawajawahi kuwafunga West Brom Albion katika Premier league wakiwa wamefungwa mechi 3 kati ya sita.

1: Mshambuliaji wa Chelsea Fernando Torres alipata kadi nyekundu ya kwanza katika soka la uingereza baada ya kutolewa katika mechi dhidi ya Swansea City.

1: James Milner alifunga bao la lake kwanza kwa Man City kwenye EPL na mara kwanza tangu ajiunge na timu hiyo.

2: Man City wamefunga wastani wa mabao mawili katika mechi zao 10 zilizopita.

3: Beki wa Wigan Athletic Steven Gohouri alikuwa mchezaji wa 3 ndani ya wiki kupewa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Gareth Bale.

5: Aston Villa hawajashinda hata mechi moja kati ya 5 za mwisho za EPL walizoenda kwenye uwanja wa nyumbani wa QPR Loftus Road.

6: Peter Crouch sasa ameweka rekodi ya kuzifungia klabu 6 za EPL baada ya kufanikiwa kufunga bao la kusawisha kwa Stoke City dhidi ya Manchester United.

7: Baada ya michezo 7, Stoke City walipata pointi yao kwanza katika EPL dhidi ya Manchester United.

8: Newcastle United waliifunga Blackburn Rovers kwa mara ya kwanza katika michezo nane iliyopita.

8: Goli la Didier Drogba dhidi ya Swansea City lilikuwa la kwanza kufunga katika uwanja wa Stamford Bridge tangu 2nd January 2011 walipotoka sare ya 3-3 na Aston Villa.

9: Beki wa Aston Villa Richard Dunne sasa amefunga magoli tisa ya kujifunga katika premier league baada ya kuwazadia goli QPR katika dk za mwisho.

10: Bolton Wanderers wamefungwa mechi zao za mwisho 10 katika ya 11 za EPL, na pia wamepoteza mechi zao 10 kati ya 13 walizoenda Emirates Stadium.

22: Manchester United sasa wamefunga magoli 22 katika mechi zao 6 za EPL, wakiifikia rekodi iliyowekwa na Newcastle United katika msimu wa 1994/95.

100: Robin Van Persie sasa ameifungia Arsenal mabao 100 tangua jiunge nayo baada ya ushindi wa Gunners wa 3-0 dhdi ya Bolton.

No comments:

Post a Comment