Search This Blog

Monday, September 12, 2011

Kocha Azam alia na Bocco,


Olaba- Yanga wanakipa mzuri sana
KOCHA mkuu wa Mtibwa Sugar Tom Olaba, amesifu kiwango alichokionyesha kipa namba moja wa Yanga Yaw Berko kwenye mchezo dhidi ya timu hiyo kuwa anaweza kutetea nafasi yake ya golikipa bora msimu huu. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Olaba alisema kiwango cha Berko kimekuwa kikikuwa kila siku hususani kwenye mchezo dhidi yao uliochezwa wiki iliyopita ambapo aliokoa mashuti mengi na kama si ubora wake wangeondoka na ushindi mkubwa. “ Yanga wanakipa mzuri sana kama uliona mechi tuliocheza nao hakika Berko ndio alitunyima ushindi wa dhahiri kama si uimara wake langoni leo tungekuwa tunaongoza kwenye msimamo wa ligi. “Nafikiri ni kutokana na kujiamini zaidi langoni mwake na uzoefu pia unachangia kiangalia ndo kwanza ametoka kwenye mashindano makubwa ya Kagame ni mzuri zaidi,” alisema olaba. Mtibwa mpaka sasa imejikusanyia pointi inane katika nafasi ya tatu imefungwa mechi moja imeshinda mbili na sare mbili.

Basena atoa onyo Simba SC
KOCHA mkuu wa Simba, Moses Basena amesema kuwa hasikitii uamuzi wake alioutoa kwenye mechi ya Azam FC, wa kumchezesha kiungo wake mshambuliaji, Shija Mkina. Katika mechi hiyo, Mkina alicheza dakika 12 pekee akitokea benchi akiingia badala ya Amri Kiemba kabla ya kutolewa na Basena nafasi yake kuchukuliwa na kiungo mshambuliaji, Uhuru Selemani . Basena alisema, kama kocha anaamini maamuzi yake na ataendelea kuyafanya hadi atakapoihama klabu hiyo kongwe yenye maskani yake Kariakoo. Kocha huyo raia wa Uganda alisema, alimuingiza Mkina kwa ajili ya kuiongezea nguvu timu badala yake alikuwa akicheza tofauti ya maelekezo aliyompa kabla ya kuingia uwanjani. “Kama kocha nafanya kwa manufaa ya kabla na siyo kumfuraisha mtu mmoja pekee, hicho ndicho kilichonileta Simba siyo kingine na hayo ni maamuzi yangu pale ninapoona mchezaji tofauti na maelekezo. “Kama kocha nitaendelea na mfumo huo pale mchezaji anapocheza tofauti na maelekezo hadi nitapoondoka Simba, Mkina mechi na Azam ilimshinda kutokana na kushindwa kuendana na kasi mchezo huo,” alisema Basena.

Kocha Azam alia na Bocco
KOCHA mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amelalamikia nafasi za wazi alizozipata mshambuliaji wake, John Bocco timu hiyo ilipovaana na Simba SC. Mechi hiyo ilichezwa jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mchezo huo uliokuwa na upinzani uliomalizika kwa sare ya kutofungana mabao timu hizo zilicheza kwa kushambuliana kila wakati. Hall alisema, katika mechi hiyo kama Bocco angekuwa makini ndani ya uwanja anaamini mechi hiyo isingemalizika kwa sare badala yake ushindi mnono na kukwea kileleni kwenye msimu wa ligi. Kocha huyo alisema, ana kibarua kigumu cha kuboresha safu yake ushambuliaji ili iweze kupata ushindi kwenye mechi zijazo za ligi kuu inayoendelea kwenye viwanja tofauti. “Ninasikitika kukosa pointi kwenye mechi yetu na Simba kutokana na nafasi za wazi alizozipata Bocco ambazo kama angezitumia vyema ninaamini matokeo yasingemalizika hivyo,” alisema Hall.

No comments:

Post a Comment