Search This Blog

Friday, September 16, 2011

CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA VS AC MILAN MATCH RPORT


Barcelona 2-2 Milan:

September 13, 2011

http://i1231.photobucket.com/albums/ee512/zonal_marking/barca-milan.jpg

Timu zilizoanza

Milan walifunga kwenye dakika ya kwanza ya mchezo na kwenye dakika ya mwisho katika mchezo uliotawaliwa na Barcelona kwa asilimia kubwa ya mchezo.

Timu ya Pep Guardiola iliwatumia Sergio Busquets na Javier Mascherano kama mabeki wa kati na Seydou Keita alicheza kama kiungo mkabaji na Barcelona ilitumia mfumo wa 4-3-3.

Kocha wa Ac Milan Maximiliano Allegri alimkosa Zlatan Ibrahimovic na hii ilimaanisha kuwa Alexandre Pato alianza kama mshambuliaji pekee akisaidiwa na Antonio Cassano nyuma yake . Antonio Nocerino na Gianluca Zambrotta pia walianza .

Mchezo huu ni mgumu sana kuuelezea , swali la kujiuliza ni hili , ni vipi mbinu za Milan zilifanikiwa kwenye mchezo huu? Kuna baadhi ya mbinu zilionekana kufanya kazi , mfano ni wembamba wa uwanja kwa jinsi walivyopanga wachezaji kujaribu kudhibiti njia za Barca kupenyeza mipira, mfumo wa Milan kwa jumla,pamoja na kujaribu kuwaadhibu Barca kwa jinsi walivyokosa kasi kwenye upande wa mabeki, hivi vyote vilifanya kazi, lakini Barcelona wangeweza kuua mchezo kama si uzembe wao wenyewe . Guardiola alikuwa anatumia mbinu zake za siku zote , ukiacha mabeki wa kati ambao wamekuwa tatizo kwa Barca hivi karibuni mbinu za Milan zilifanya kazi kwa kiasi Fulani.

Vitu vilivyofanikiwa kwa upande wa Milan

1 Mfumo kwa ujumla

Timu za Italia zimekuwa zikigharimiwa na kucheza kwa kukosa wachezaji wa pembeni haswa kwenye ligi ya mabingwa.Timu ya mwisho kuondoka na pointi tatu kwenye uwanja wa Nou Camp ilikuwa Hercules ambao walishinda msimu uliopita kwa mabao 2-0 kwenye ligi ya Hispania . Hercules walitumia mfumo wa 4-4-2 ya mtindo wa Diamond na Milan walijaribu kufanya kitu kama hiki ili kushindana na viungo wa Barcelona ambao wanamiliki mpira kwa kiasi kikubwa .Mabeki wa Milan walicheza vizuri wakijitahidi kujenga ukuta ambao ulionekana kuwabana wachezaji wa Barcelona, viungo watatu waliosimama mbele ya mabeki walifanya kazi yao vizuri kwa kuweka ukuta wa ziada mbele ya mabeki wa Ac Milan huku kiungo ambaye alifanya kazi ya ubunifu nyuma ya Cassano na Pato Kevin Prince Boateng na baadae Clarence Seerdorf walicheza kwenye eneo ambalo alisimama Seydou Keita . Tatizo kubwa ambalo liliwakumba Barca kwa kumchezesha Keita mbele ya mabeki kama kiungo mkabaji ni kwamba wachezaji wa Barca walishindwa kwenda kwa Keita kuchukua mipira na hali hii iliwapa uhuru Boateng na Seerdorf.

2.Kumdhibiti Messi.

Siku zote utakapocheza dhidi ya Messi ukae ukijua kuwa lazima yeye ang’ae mwisho wa siku na ukishindwa kumhimili hakuna atakayekulaumu kwa sababu kila mtu anajua uwezo wake na sio mabeki wengi wameweza kumzuia kwa mafanikio . Milan mwanzoni mwa mchezo kuanzia dakika waliyopata bao mpaka kwenye dakika ya 30 waliweza kummudu na kumzuia kwa kiasi fulani, Alesandro Nesta alimkaba na Messi na alihakikisha kuwa alimkera . Haikuwa lengo au mbinu ya Milan kumkaba Messi yeye kama yeye au peke yake . Waliweka nidhamu yao ya ukabaji kama kawaida yao ila kila alipopata mpira walihakikisha kuna watu wawili au zaidi wamemzunguka ,kilichomzuia messi kufanya vitu vyake mwanzoni ni viungo watatu wa Milan waliokuwa wamesimama mbele ya mabeki ambao uwepo wao ulimnyima Messi nafasi ya kurudi hadi katikati ya uwanja kufuata mipira kama anavyofanya siku zote. Barca walicheza sana mbele ya wachezaji nane waliokuwa mbele ya goli na nyuma ya mpira na ndio maana mchezo ulikuwa mgumu kwa Barca mwanzoni . Lakini ndio kama ilivyosemwa awali kwamba utamkaba Messi unavyotaka lakini mwishowe lazima atakudhuru na ndio kilichotokea kwani mwishowe alitengeneza bao lililofungwa na Pedro.

3.Kumhimili Dani Alves

Hasara mojawapo ya kuchezesha mfumo wa 4-3-1-2 dhidi ya timu kama Barcelona au timu nyingine yoyote ile ni ukweli kuwa unawapa uhuru mkubwa sana mabeki wa pembeni . Ila Milan walitumia mfumo huu na hawakupata tabu kwani waliridhika na kuwapa uhuru mabeki wa pembeni wa Barcelona . Alves alikuwa akipambana na Gianluca Zambrotta na Pedro alikuwa akiingia mpaka katikati ya uwanja , Dani Alves hakuwa anakimbia pembeni sana na Zambrotta alikuwa anamruhusu aingie ndani sana kwa kuwa ndio upande ulipo mguu wake wenye nguvu mguu wa kulia japo anatumia miguu yote miwili na upande huo ndio upande ambao Dani Alves hautumii sana na kwa sababu hii Barcelona walijikuta wakipunguza uwanja wao wenyewe huku wakishindwa kutanua uwanja.

4 Pressing ya Milan.

Milan mwanzoni walikuwa wameridhika na kukaa kwenye nusu yao ya uwanja na kuwaachia Barcelona waje , walikuwa wameridhika kukaba na kuutafuta mpira ulioko kwenye himaya ya Barcelona . Kwenye dakika ya 50 walilazimika kutoka pangoni baada ya kufungwa bao la pili . Hapa Allegri hakuona faida ya kukaa nyuma tena na akabadili mfumo na kuwaelekeza wachezaji wake kutoka na kushambulia . Bado Barcelona waliendelea kutawala mchezo kwenye kipindi hiki ila kiu ya Milan ya kujaribu kuchukua mipira miguuni mwa wachezaji wa Barcelona ilionekana wazi. Hakuna haja ya kuendelea kubaki nyuma ukiwa umefungwa katika hali ya kawaida.

5.Kuanzisha mchezo kutoka nyuma .

Kama ilivyoonekana kwenye bao la mapema la Pato , Milan wangefaidika kwa kutumia wachezaji wenye kasi dhidi ya wa Barcelona ambao hawana kasi hasa mabeki wa kati.

Kikosi cha Guardiola kwa kawaida huwa kinacheza kwa kukaba kuanzia sehemu ya juu ya uwanja lakini Sergio Busquets na Mascherano walionekana kuwa wangelazimika kurudi nyuma kulinda lango lao. Hivyo tangu mwanzoni mwa kipindi cha pili ilionekana wazi kuwa Christian Abbiati , Nesta na Thiago Silva walikuwa wakianzisha mipira kuanzia langoni mwao na si kupiga mipira mirefu ili kuwatamanisha wachezaji watatu wa mbele wa Barca wafuate mipira toka kwao (kina Nesta) ili kutengeneza nafasi nyuma yao.

6 .Mabao ya wazi.

Milan walikuwa na vyanzo viwili vya wazi vya mabao(A) Kasi kupitia katikati na (b)mipira iliyokufa. Hivi vyote viwili vilifanya kazi kwani bao la kwanza Milan walifunga kwa kutumia kasi ya Pato na bao la pili lilifungwa kupitia kona .

Kilichoenda vibaya kwa Milan.

1.Kutoa faulo nyingi .

Timu yoyote inayomtumia Mark Van Bommel kwenye sehemu ya kiungo wa kukaba siku zote lazima itagawa faulo nyingi,wachezaji wa Milan walikuwa wanajitupa kupita kiasi wakidhani kuwa kucheza rafu ni mojawapo ya njia za kuwapunguza kasi Barcelona.Alesandro Nesta alicheza rafu za akili tofauti na wenzie hasa pale ambapo lango la Milan lilipokuwa hatarini lakini viungo waliokuwa mbele yake hawakufuata mfano wake , walikuwa wanacheza rafu zisizo na msingi na kiranja katika hilo alikuwa Mark Van Bommel na ndio maana alipewa kadi ya njano mapema kwennye dakika ya 18. Unapocheza dhidi ya Barcelona siku zote uko hatarini kupata kadi, sasa unapopata kadi ya njano kwenye dakika ya 18 halafu bado una muda mrefu wa kukimbizana na Xavi, Iniesta na Messi unategemea nini kama si kadi nyekundu. Hili liliigharimu Milan kwani baada ya kupewa kadi Van Bommel hakufanya ‘tackling’ nyingine yoyote kwa kuhofia kuonyeshwa kadi nyingine na hili liliidhuru timu yake.

2.Kuruhusu mashuti mengi.

Moja ya sifa nyingi za Xavi kama mchezaji si upigaji wa mashuti ya mbali, hizo ni sifa za kina Lampard na Steven Gerard, lakini cha ajabu ni kwamba Xavi alipiga mashuti matatu ya mbali kwenye mchezo huu, hii ni kwa sababu kulikuwa na nafasi ya kufanya hivyo ambayo ilitengenezwa na viungo wa Milan .

3.Hakukuwa na pasi za mwisho za uhakika(hasa pasi za kupitia katikati ya mabeki)

Barcelona walikuwa wadhaifu kwenye safu ya ulinzi hasa kwenye mashambulizi ya moja kwa moja lakini Milan hawakuwa na ujanja wa kupenyeza mipira katikati ya mabeki kwa kuwa wachezaji wa mbele hawakuwa wamejipanga vyema kufanya hivyo. Hakuna aliyejua jukumu alilopewa Antonia Cassano kwenye mchezo huu.Cassano alikuwa akicheza kama mshambuliaji anayeshuka mpaka chini , sawa lakini mchezaji huyu anapaswa kufanya nini au ana jukumu gani la kutimiza hasa pale ambapo timu yake haina mpira .Alichotakiwa kufanya Cassano ni kurudi ndani zaidi au kusogea pembeni kumvuta Mascherano atoke kwenye eneo lake na kuanzisha mashambulizi ya ghafla. Pengine Urby Emmanuelson angeweza kupangwa tangu mwanzoni kwa kuwa ana kasi na angeweza kuyapa mashambulizi ya Milan mlengo tofauti kidogo akitokea pembeni ya uwanja, hapa Barca wangejaribiwa zaidi kutokana na kukosa kasi kwenye timu yao.

4 .Uchovu

Cassano , Pato na Seerdorf mwisho wa siku walichoka na upande pekee wa Milan ambao haukuwa na wachezaji waliochoka ulikuwa upande wa kulia na ni kwa sababu Antonio Nocerini na Ignazio Abate walikuwa na uwezo wa kukimbizana na Barca na hata bao la kusawazisha kwa Milan lilipatikana baada ya ubishi wa Nocerino ambaye alilazimisha kona iliyozaa bao.

No comments:

Post a Comment