Baada ya wadau wengi wa soka kushangazwa na kuhoji uamuzi wake, kocha wa Simba, Moses Basena amesema alifikia uamuzi wa kumtoa kiungo wake Shija Mkina katika mechi dhidi ya Azam FC ili kuepuka hatari ya kupewa kadi nyekundu.Mechi baina ya Simba na Azam ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na timu hizo kutoka suluhu.
Katika mchezo huo, Basena alifanya mabadiliko mara mbili ndani ya dakika 10 baada ya kumtoa Mkina ambaye awali alikuwa ameingia kuchukua nafasi ya Amri Kiemba na kumwingia Uhuru Selemani.
Akizungumza jana, Basena alisema kuwa, endapo angemwacha Mkina aendelee kucheza katika mechi hiyo, kulikuwa na uwezekano mkubwa winga huyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa vile tayari alikuwa amepoteza umakini kutokana na kuchezewa rafu mara mbili ambazo mwamuzi hakuziona hivyo ingeweza kuwa hatari kwao.
"Kipindi cha kwanza, Amri Kiemba nilimpanga kama kiungo wa upande wa kulia, lakini alikuwa akicheza zaidi katikati kwa vile nilitaka kuubana uwanja.
"Kipindi cha pili nilipoamua kushambulia zaidi, nilimwingiza Mkina ili atanue uwanja na tuongeze mashambulizi, lakini kilichotokea ni kwamba kuna rafu kama mbili hivi alifanyiwa na mwamuzi hakuwa amezona hali ambayo ilisababisha atoke mchezoni
"Kama angeendelea kubaki uwanjani kuna uwezekano mkubwa angepewa kadi nyekundu, jambo ambalo lingekuwa na athari kwetu na kwa mchezaji binafsi," alisema Basena.
Search This Blog
Tuesday, September 13, 2011
BASENA AJITETEA JUU YA SUALA LA SHIJA MKINA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment