Search This Blog

Monday, August 8, 2011

WEPESI WA VIJANA WA ‘BABU UNAWEZA KUREJESHA ENZI ZA SAFU YA USHAMBULIAJI YA UNITED 2008.

Mechi za ngao ya jamii siku zote huonekana kuwa mechi za kukamilisha kama si kuanzisha ratiba, kimsingi zinaonekana kukosa mvuto na wengi huziona kama zinaboa sana . Hiyo imekuwa tofauti mwaka huu ambapo Man united wakiwa wameshakufa kipindi cha kwanza walifufuka na kuondoka na ushindi kwa bao safi la dakika ya 90 la Luis Nani na kushinda 3-2.

Sir Alex Fergusson alifanya mabadiliko mwanzoni mwa kipindi cha pili . Itakuwa rahisi sana kusema kuwa alifanya ujanja ambao umeipa United ushindi mwishoni . Kiukweli United hawakushinda kwa sababu ya mabadiliko kwani walitawala mchezo wao dhidi ya City tangu mwanzoni na hata pamoja na ukweli kuwa United walikuwa nyuma kwa mabao mawili kufikia mapumziko , ni dhahiri kuwa walicheza vyema na tofauti ni kuwa City walitumia vyema nafasi mbili walizozipata kinyume na United ambao hawakautumia na kama wangezitumia zao basi wangekuwa vifua mbele kwenye nusu ya kwanza ya mchezo.


Mechi ya ngao ya jamii kwa kuwa ni fungua pazia ya ligi kuu nchini England huwa ni mechi ya kuonyesha wachezaji waliosajiliwa watafanya nini kwenye timu zao mpya lakini cha kushangaza ni kwamba wachezaji wote wa Man City walioanza walikuwepo kwenye timu hiyo msimu uliopita na Roberto Mancini hakukibadilisha kikosi chake , kilikuwa vile vile kama kilivyokuwa msimu uliopita.


United kwa upande wao walikuwa timu tofauti kabisa na ile ya msimu uliopita hususani kile kilichotawanywa na Bracelona kwenye fainali ya klabu bingwa ya ulaya na Barcelona . United waliingia na kipa mpya David De Gea ( ambaye alikuwa topic ya mazungumzo kwenye kipindi cha kwanza ) lakini kivutio kilikuwa jinsi wepesi wa mawasiliano uwanjani waliokuwa nao wachezaji wane wa upande wa mbele .

Kwenye kipigo ilichokipata United mikononi mwa Barca wengi walikuwa wepesi kuainisha tofauti za timu hizi mbili ( United na Barca) na kwa hili wengi wakatoa maoni jinsi United inavyopaswa kutumia dirisha la usajili kufanya marekebisho ili kujaribu kuwafikia Barcelona . Kuna chembechembe za ukweli kwenye hili . Kwa mfano United lazima wafanyie marekebisho jinsi wanavyokaa na mpira kwa muda mrefu , ila ikumbukwe kuwa wakijaribu kuwaiga Barcelona hawataweza kuwafikia .


Barcelona wanatamba kuwa na wachezaji bora wa tatu ulimwenguni na pia kikosi ambacho kimetengenzwa kwa muda mrefu . Hivyo kwa timu itakayotaka kuwa kama Barca ni lazima iwe na mpango halisi na wa ukweli na pia wenye tofauti na si kuwaiga ( barca) moja kwa moja .

United wanaonekana kuwa na upekee na watafanya vyema kama wakirudi na kuchungulia kikosi cha mwaka 2008 ambacho kiliweza kutwaa ubingwa wa Ulaya na kikosi cha msimu uliofuata ambacho kilijitahidi kushindana na Barcelona . Kikubwa kwenye vikosi hivyo (2008-2009) ni wepesi wa mawasiliano baina ya wachezaji wa upande wa mbele Wayne Rooney , Cristiano Ronaldo na Carlos Tevez.

Haya yote yalibadilika baada ya kuondoka kwa Tevez na Ronaldo na japo wabadala wao Valencia,Owen,Hernandez na Berbatov wote ni watu wenye uwezo mkubwa sana tu ila wanakosa uwezo wa kuwa na mitazamo tofauti ya uchezaji kama wenzao ( ronaldo-tevez) na uwepo wao ulimaanisha kuwa United walikuwa wanatabirika sana na hata walipoukosa ubingwa wa ligi kuu ya England mwaka 2009/10 wengi waliamini kuwa ni kwa sababu ya kukosa sfau ya ushambuliaji kama iliyokuwepo msimu mmoja uliopita

Usajili wa Ashley Young ni muhimu sana kwa kuwa ana uwezo wa kucheza kwenye winga zote mbili na hata nyuma ya mshambuliaji nafasi ambayo hata kocha wake wa zamani Gerard Houlier anaamini kuwa ndio bora kwake . Zaidi ya hapo Danny Welbeck ana uwezo wa kucheza winga zote na kati pia kitu ambacho kijana mwenzie Tom Cleverly ana uwezo wa kukifanya kwa ufanisi pia japo yeye ni mchezaji tofauti kabisa .


Uchezaji bora kabisa wa Luis Nani uliipa United matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya City . Kurejea kwa Valencia toka kitanda cha wodi ya majeruhi kulimondoa Nani kikosini pamoja na ukweli kuwa Nani alicheza vizuri sana msimu uliopita .

Hivyo mfumo ambao United iliutumia kwenye mechi kubwa msimu uliopita wa 4-4-1-1 kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita ulikuwa mfumo ambao umeundwa kiukweli lakini ufanisi wake ulionekana zaidi kwenye uwezo wa wachezaji wa kujipanga kwenye nafasi zao .


Valencia alicheza vizuri kwenye baadhi ya mechi –mfano ile dhidi ya Chelsea Old Trafford-lakini pale alipocheza vibaya kama ilivyokuwa kwenye fainali dhidi ya Barca aliifanya United ionekane kama timu ya upande mmoja iliyokosa mpango mbadala (plan b)


movement za wachezaji wanne wa mbele wa United .

Ilishangaza kidogo kuona kuwa Fergusson aliingia kwenye mchezo dhidi ya Man City akitumia mfumo wa 4-4-2 ambao ulionekana kuwa na wepesi kwa wachezaji wa United .Young na Nani wote wanaweza kucheza kwenye winga zote mbili . Young alianzia kushoto huku Nani akiwa upande wa kulia , ila wote walikuwa wakiingia ndani kwa haraka kushirikiana na washambuliaji wao .


Silaha kuu ilikuwa ‘positioning’ na ‘movement’ za wachezaji wawili wa mbele . Hakuna yoyote kati yao aliyekaa upande wa juu wa uwanja begani mwa mabeki wa mwisho . Welbeck alikuwa akirudi mpaka karibu na ‘midfield’ akijaribu kumvuruga De Jong, huku Rooney akicheza kama ‘namba 9 wa uongo’ .


Hivyo kwa haraka United walikuwa kama wanatumia 4-4-2 na walikuwa hawana washambuliaji halisi ‘kinafasi’, na badala yake Rooney na Welbeck walikuwa wakishirikiana na Young na Nani huku mabeki Kompany na Lescott wakihangaika ‘kukatiza’(intercept) pasi zao , mabeki hawa wanapokuwa wametolewa kwenye ‘position’ zao yoyote kati ya wachezaji wanne wa mbela wa United angewatoroka na kutengeneza chumba cha hatari nyuma yao.

United walifunga baada ya mapumziko na ilikuwa baada ya Tom Cleverly kuchukua nafasi ya Michael Carrick. Hii iliongeza movement za kijanja za Man united kwenye upande wa ushambuliaji japo wachezaji karibu watano wa United walikuwa wanaonekana kuongezeka kwenye nusu ya adui wakagti timu yao ikimiliki mpira .


Bao la pili lilikuwa matokeo ya ‘movement’ za hatari za Man United . Ni vigumu kuwafikiria United wakifunga bao kama lile wakitumia mfumo wa 4-4-1-1 kama walivyokuwa wakiutumia mwishoni mwa msimu uliopita .

Tayari watu wameliita bao lile ‘bao la kibarcelona’lakini huu ni mfano wa kivivu. Lile halikuwa bao la kibarcelona , ungeweza kulifananisha na mabao ambayo Arsenal ya katikati ya miaka ya 2000 ilikuwa ikiyafunga, mfano bao alilofunga Patrick Vieira katika mechi dhidi ya Liverpool. Kikosi kile cha Arsenal kilikuwa kinatumia 4-4-2 ambayo haina mshambuliaji halisi huku wakiwa na mawinga wawili wanaoingia ndani .

Goli hili linaweza kuwa mwanzo wa taswira ya enzi mpya kwa United . Japo si sahihi sana kuzungumzia zama au enzi mpya kwa United kwani ni miezi michache tu imepita toka mwezi mei United walipofungwa na Barcelona na hivyo huwezi kuita kinachotokea United Mapinduzi .


Ila ukweli ni kuwa kuna mabadiliko kwenye kikosi hiki na mabadiliko haya yataendelea kuonekana kwani unapokuwa na wachezaji ‘versatile’ yaani wenye mitazamo na uwezo wa kubadilika kuendana na mazingira tofauti kunakuwa na wepesi wa mawasiliano na hapo safu ya ushambuliaji inakuwa ya kutisha zaidi .

No comments:

Post a Comment