Makamu wa kwanza wa TFF, Athumani Nyamlani ( kushoto ),Raisi wa TFF,Leodegar Tenga ( katikati )
Wazo la kurudisha Ligi za Madaraja ya chini limenigusa sana. At least TFF wabaki na Ligi 2 (Ligi Kuu na 1st Division) halafu 2nd Division ndiyo ziwe Ligi za Mikoa, 3rd Division (Ligi za Wilaya) huku TFF ikitoa mwongozo wa uendeshaji wa ligi hizo za chini ili ziwe na ubora unaolingana.
Hapo angalau soka letu litakuwa na ‘structure’ kuliko lilivyo sasa, ni kama Kampuni iliyo na ‘Top Management’ (uongozi wa juu) tu bila ngazi za chini kujua nani supervisor na nani kibarua. Kampuni lazima itapoteza mwelekeo.
Ila napingana na issue ya kujaza timu Ligi Kuu, kwa kuwa inaweza kuleta timu nyingi zisizo na uwezo wa kucheza ligi kuu yenyewe. Tuliwahi kuwa na Ligi ya Timu 20 miaka ya 1990s kama sikosei, na kwa kumbukumbu yangu utamu wa Ligi uliisha katikati baada ya baadhi ya timu kutotokea uwanjani au kuuza mechi wapate hela ya kula.
Mapendekezo yangu ili wachezaji wapate mechi za kutosha, Ligi itengenezwe kwa mfumo huu:-
1. Ligi Kuu iwe na timu 14 (mechi 26 kwa msimu) au timu 16 (mechi 30 kwa msimu) pamoja na Mashindano ya Kombe la Mtoano la FA lenye kama raundi 4 za nyumbani na ugenini (approx. mechi 8 kwa timu zitakazofika fainali). Wenzetu Misri tunaowaheshimu wanatumia mfumo wa Ligi yenye timu 14, wakati South Afrika wana Ligi ya timu 16.
2. Ligi Kuu iwe na timu 10 lakini zikutane mara 4 kwa msimu (mechi 36 kwa msimu). Mfumo huu unatumiwa Scotland. Najua hawapo juu kisoka, lakini mfumo huu unasaidia kufanya Ligi iwe ya ‘Quality’ na ushindani mwanzo mpaka mwisho kwa vile timu kubwa zinakutana mara nyingi mpaka kuamua Bingwa.
Mimi kilio changu ni kuwa na Ligi ya ushindani yenye viwango na si kujaza timu ili mradi ziwe nyingi. Tunaweza kuanza kwa viwango rahisi ili kuvutia wadhamini na kuboresha soka kwa kuzitaka timu ziwe na bajeti za msimu za kueleweka, timu B na za vijana pamoja na kuwa na mipango ya muda mrefu ya viwanja vyao binafsi vyenye hadhi ya soka la ushindani.
Ni TFF ndiyo wa kwanza kufanyia kazi haya kwa kuweka msingi na si kusubiri serikali. Serikali ikiona mabadiliko, nina uhakika watakuwa tayari kutoa msaada ili wapate kura mbele ya wananchi.
Ni hayo tu.
structure nzima za ligi ni mbovu ndio maana tunakosa ligi inayosisimua.
ReplyDeleteTff wanatakiwa kuiangalia upya kuanzia ngazi ya chini, tusikimbilie kudai kuongeza timu ambazo zitashindwa kuleta msisimko. Na ningependa kuona ligi ya muungano inarejeshwa.
http://aboodmsuni.blogspot.comstructure nzima za ligi ni mbovu ndio maana tunakosa ligi inayosisimua.
Tff wanatakiwa kuiangalia upya kuanzia ngazi ya chini, tusikimbilie kudai kuongeza timu ambazo zitashindwa kuleta msisimko. Na ningependa kuona ligi ya muungano inarejeshwa.
http://aboodmsuni.blogspot.com