Wesley Sneijder amekiri kuwa kweli yupo sokoni kwa kuwa klabu yake inahitaji pesa lakini atauzwa kwa fedha inayoeleweka na nzuri.
Sneijder ambaye amekuwa akihusishwa kwa nguvu sana kujiunga na Manchester United katika kipindi hiki cha usajili, kabla ya jana gazeti moja nchini Italy kuripoti kuwa Man City nao wanamtaka mchezaji huyo.
Akiongea na Voetball International Sneijder alisema: “Ninavyofahamu ni kuwa Inter wanahitaji pesa na kwamba mimi nipo sokoni, kama ofa nzuri ikitokea.Nina siku tano za mapumziko baada ya game ya kirafiki na England – Jumatano.Nategemea hatma yangu itajulikana ndani kipindi hiki,” alisema mdachi huyo.
Mchezaji huyo wa zamani wa Ajax na Real Madrid pia aliongelea kuhusu tetesi za usajili wake kwenda either Man United au City alisema: “Naweza kusema kwa kifupi tu kuhusu Manchester United na City.Sijaongea na timu yoyote kati klabu hizo mbili, hivyo siwezi sina mengi ya kusema kuhusu hatma yangu kwa sasa.”
No comments:
Post a Comment