Kiungo nyota wa zamani wa ‘Majogoo wa jiji’ Liverpool, Steve McManaman amefanya mahojiano na BLOG hii na kuchagua kikosi cha wachezaji 11 bora ambao yeye binafsi ameona kuwa ni bora kwa muda wote katika historia ya timu hiyo. McManaman ana nafasi ya kuchagua kikosi hicho kutokana na kuwa ni mmoja wa wachezaji wakali waliowahi kucheza kwa mafanikio pale Anfield katika miaka ya 1990.
Kwa mujibu wa McManaman, golikipa huyu ni bora zaidi ya wote waliopo na waliopita katika timu hiyo. Clemence alikuwa bora na alikuwa moja wa magolikipa imara na wagumu kufungika katika wakati wake wa uchezaji.
02: Phil Neal
Alikuwa ni beki bora wa pembeni katika historia ya Liverpool, akicheza kwa staili ya kupanda na kushuka, Phil hakika ni mmoja wa mashujaa wa kudumu katika moyo wa Steve McManaman.
03: Alan Kennedy
Alikuwa mzalishaji muhimu wa mabao ya Liverpool wakati akiwa mchezaji wa kikosi hicho. Ni beki bora zaidi wa upande wa kushoto katika historia ya timu hiyo.
04: Alan Hansen
Kwa sasa ni mmoja wa watangazaji wa BBC, lakini kwa walimwona Mscotish huyu hakika wanasema kuwa alikuwa ni beki bora. Alicheza mechi 620 na kufunga mabao 14 katika miaka yake 15 aliyoitumia Anfield.
05: Jamie Carragher
Mwamba wa safu ya ulinzi ya Liverpool wakati wanatwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2005. Ni mtoto hasa wa jiji la Liverpool. Kwa sasa amekuwa majeruhi mara kwa mara lakini anapokuwa ‘fiti’, Carragher huwa moto wa kuotea mbali kwa mabeki.
06: Graeme Souness
Hana umbo kubwa kama la Papa Bouba Diop, lakini kiungo huyu wa zamani wa England alikuwa mpambanaji na mara zote alikuwa ni mshindi. Kwa sasa ni mmoja wa makocha wenye kuheshimika katika England.
07: Steve Heighway
Alikuwa winga hatari wakati akivaa jezi ya Liverpool. Kwa kawaida Liverpool imekuwa timu ya ‘mahandsome boy’ pia hata kwa kiungo huyu alikuwa na sifa zote ya ‘umodel’. Alikuwa mzalishaji wa magoli mengi ya ‘the reds’.
08: Steven Gerrard
Mshindi wa taji la ligi ya mabingwa, Gerrard kwa sasa ndiye ‘Mr Liverpool’ wa ukweli. Kwa kutambua umuhimu wake, McManaman amemjumuisha kiungo huyu katika kikosi chake. Nadhani hata wewe msomaji usingepata tabu kumpanga kiungo huyu katika dimba la kati.
09: Kenny Dalglish
Kila mtu anayepita na kuchezea Liverpool hakika alikutana na jina la Dalglish. Mshambuliaji huyu wa zamani wa timu hiyo alikuwa ni hatari katika kupasia nyavu. Ndiye mchezaji mwenye mafanikio kuliko wote katika historia ya Liverpool.
10: Ian Rush
Mmoja wa wafungaji wakali ambao Dunia ilipata kuwashuhudia. Wengi wanaweza kumshangaa McManaman kwa kutowapanga Robie Fowler au Fernando Torres. Fowler alikuwa mfungaji asilia, lakini Rush alikuwa ni mfungaji aliyekamilika ambaye alitengeneza ‘kombinesheni’ya hatari na Kenny Daglish.
11: John Barnes
Kwa sasa huwa anachambua soka katika kituo cha television cha Super Sport ya Afrika ya Kusini. Barnes alikuwa anafunga magoli ya kuvutia na alikuwa mtengenezaji mzuri wa mabao pale Liverpool na alikuwa mtumiaji mzuri wa guu lake la kushoto.
No comments:
Post a Comment