JE, ushawahi kusikia msemo wa kisoka uitwao “Sexy Football”, ama kwa Kiswahili soka lenye mvuto wa kimapenzi? Sasa BLOG yako inakukutanisha na mwanzilishi wa soka laini lenye mvuto, soka ambalo limetumiwa vyema na mabingwa wapya wa kombe la dunia Hispania, kujibebea ndoo za Ulaya na dunia kwa ujumla. Hapa namzumgumzia si mwingine bali muholanzi Ruud Gullit.
hapa ilikuwa ni baada ya mazungumzo marefu na Gullit ( kulia ) pamoja na Steve Mcmanaman.
Lakini mara nyingi umekuwa ukitamka kuwa hakuna mahala umewahi kufurahia kuishi katika maisha yako ya kisoka zaidi ya jijini London. Ni kwa sababu gani?
Sitokuja kusahau maisha ya London na katika klabu ya Chelsea kwa ujumla kwani kwanza kocha Glenn Hoddle, alikuwa akinisikiliza na kunichezesha nafasi niliyoizoea, pia nilipata sapoti kubwa sana toka kwa wachezaji wenzagu kina Mark Hughes na Dan Petrescu.
Hebu tuambie kuhusu staili hii ya uchezaji wa “total football” ama kama unavopenda kuiita “sexy Football”
Mimi nilikuwa mchezaji wa aina yake kwani nilikuwa na uwezo wa kucheza nafasi nyingi niwapo uwanjani. Niliweza kucheza kama beki wa kati, beki wa pembeni kiungo mkabaji, kiungo mshambuliaji na hata straika. Niliweza kufanya hivi sababu nilikuwa na spidi, nguvu na uwezo mkubwa hewani. Sasa staili hii ya uchezaji wangu ndio iliyowafanya makocha kuanza kuiga katika timu zao.
Ruud Gullit akiwa na Glenn Hoddle enzi hizo anachezea Chelsea.
Historia yako kama kocha imejaa milima na mabonde toka enzi za Chelsea, lakini tuko na mshawasha sana wa kujua kilichotokea Marekani na LA Galaxy?
Unajua soka la kimarekani liko tofauti kidogo tukianza ma masuala yao ya kuweka viwango vya mishahara na sheria za uhamisho na usajili wa wachezaji. Mimi nilifika pale mwaka 2007 na malengo na mipango yangu ya kuifikisha mbali LA Galaxy. Ila kulikuwa na wafitini ambao walidhani mimi nimeletwa pale na Beckham na wala sikustahili hivyo walinipikia jungu hadi ikasababisha niondoke.
Vipi kuhusu Celestine Babayaro?
Celestine alikuja Galaxy kwa maombi yangu. Celestine alikuwa mchezaji mzuri sana na mwenye kipaji lakini alikuwa akiandamwa na matatizo mengi sana nje ya uwanja hivyo ilimuwia vigumu kuwa makini pale klabuni, ilibidi tu aondoke.
Sasa turudi kwenye “Sexy Football” unadhani staili hii ndio iliyowaangusha waholanzi katika fainali ya kombe la dunia 2010?
Siwalaumu vijana waliocheza mwaka huu, siwalaumu hata kidogo. Timu ya Uholanzi mwaka huu tofauti na miaka mingine haikuwa ikicheza soka lake la siku zote la kushambulia. Mwaka huu kocha alifanya kitu sahihi kwa kuwafundisha vijana wake kucheza soka chafu ili mradi ushindi. Kilichowaangusha ni kuwa Wahispania walikuwa makini zaidi; ni hicho tu.
Nini kifanyike Waholanzi waache kuishia kufungwa tu katika fainali kila wakati?
Kwanza napenda kumpongeza kocha Bert Van Marwijk, ametengeneza timu nzuri sana yenye vijana kama kina Van Persie, Robben, Elia na wengineo. Vijana hawa ambao tayari wana uzoefu wa mashindano makubwa ndio watakaojenga timu ya kesho ambayo itakuwa tayari imekwishajifunza toka katika fainali ya mwaka huu. Yanahitajika mabadiliko kidogo tu Uholanzi ni timu nzuri tayari.
Unaenjoy kuwa mchambuzi wa soka zaidi ya kucheza?
Nishakuwa mzee sasa hivi hata danadana kumi sifikishi (anacheka). Nafurahia kila mara sababu inanipa nafasi ya kutumia utaalamu wangu wa ukocha kuchambua mechi na kuwapa burudani wapenzi wa soka. Pia inanifanya nisafiri sana na kukutana na watu wengi tofauti kama nilivyokutana na wewe hapa Sauzi.
Ulifikiria nini kutoa ule wimbo uliokamata chati za muziki mwaka 1988?
Kipindi kile kulikuwa na vitendo vingi sana vya ubaguzi wa rangi na ukandamizaji wa watu weusi. Hata mimi mweneywe ilikwishanikumba uwanjani nikiwa nachezea Feyernoord wakati huo tulikuwa katika mechi dhidi ya ST Mirren. Mashabiki walinizomea sababu ya rangi yangu. Hii iliniuma sana. Nililia sana siku ile. Ikichangiwa na vitu kama kufungwa kwa Mandela n.k niliona ni wakati mzuri wa kutoa wimbo wa kupinga vitendo hivi.
Kwa kumalizia mzee nasikia una watoto sita ni kweli?
Yes! Nina watoto sita niwapendao kuliko chochote hapa duniani. Wa kwanza anaitwa Felicity na mdogo wake Charmayne hawa nilizaa na Yvonne de Vries. Wa tatu anaitwa Quincy na wa nne Sheyenne hawa wana mama yao pia aitwaye Cristina Pensa. Mke wangu wa sasa anaitwa Estelle Cruyff ambaye kama jina linavyoonesha ni mpwa wa Johan Cruyff. Huyu tumezaa nae watoto wawili pia Maxim na Joelle. Maxim nimekuja naye hapa Sauzi yuko hapo nje anacheza.
Shukrani sana Ruud Dil Gullit
Asante nawe pia, karibu Holland siku moja.
No comments:
Post a Comment