Search This Blog

Tuesday, August 23, 2011

BARCLAYS PREMIER LEAGUE KWENYE NAMBA


2 – Ushindi wa Newcastle United wa 1 – 0 dhidi ya Sunderland unamaanisha kuwa wamefanikiwa kupata clean sheets katika michezo yao miwili ya ufunguzi wa EPL kwa mara ya kwanza.


5 – Ushindi wa Manchester City wa 3 -2 dhidi ya Bolton Wanderers unaamanisha kuwa matajiri hao wa EPL wameshinda mechi 5 mfululizo za premier league kwa mara ya pili katika historia ya klabu hiyo.


7 – Namba ya magoli waliyofunga Man City katika zao mbili za ufunguzi.


11 – Ushindi wa 2-0 wa Liverpool dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates ndio ulikuwa ushindi wao wa kwanza nyumbani kwa Gunners ndani ya kipindi cha miaka 11 tangu washinde 1-0 mwaka 2000.


19 – Namba ya michezo ambayo Sunderland wameshindwa kuwa na clean sheet dhidi ya majirani zao Newcastle United.


100 – Mechi waliyofungwa Everton 1-0 dhidi ya QPR ilikuwa mechi ya 100 kwa Everton kufungwa nyumbani katika premier league.


1988 – Goli la Shane Long kwa West Brom dhidi ya Chelsea lilikuwa la kwanza kwa kufungwa na mchezaji wa timu hiyo tangu mwaka 1988 katika premier league.


5663 – Ushindi wa 1-0 wa QPR dhidi ya Everton ulikuwa ndio wa ushindi kwanza wa premier league katika siku 5663, kutokea 16, February 1996.



No comments:

Post a Comment