Vincent Kompany anatarajiwa kutangazwa kuwa nahodha mpya wa Manchester City hata kama Carlos Tevez atabaki in Eastlands club.
Kompany ambaye alikuwa akishika nafasi ya unahodha kipindi Tevez alipokuwa amekosekana katika baadhi ya mechi msimu uliopita ndani kikosi cha Man City, na sasa ikiwa ni baada ya wiki moja kupita tangu Tevez awasilishe ombi la kutaka kuondoka vyanzo vya habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema Vincent Kompany anapewa nafasi kubwa ya kupewa kitambaa cha unahodha.
Tevez alipewa uongozi baada ya Kolo Toure, mwanzoni mwa msimu uliopita katika hali ya kuhakikisha mchezaji wa raia wa Argentina anabaki ndani ya City of Manchester.
Lakini, kipindi Tevez akiwa kiongozi mzuri uwanjani, kugombana kwake na kocha Roberto Mancini, kuomba kuondoka mara mbili kumemfanya asiaminike mbele ya mashabiki wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment