Klabu ya Palermo ya Italia imesema kuwa ndani ya siku 10 zijazo kiungo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Argentina na klabu hiyo Javier Pastore atakuwa ameuzwa kwa moja ya vilabu vikubwa barani ulaya kwa dili linalokaribia kufikia £40million.
Kwa mujibu wa klabu hiyo ya Italia Javier Pastore mwenye umri wa miaka 22 ambaye amekuwa akizivutia klabu kubwa barani Europa anatarajiwa kurudi Italia siku chache zijazo akitokea kushiriki katika michuano ya Copa America.
Akiongea na press raisi wa Palermo Maurizio Zamparini alisema:"Jana, Niliongea na klabu kubwa ya ulaya na wamesema wapo tayari kulipa kati ya £39m-£43 kwa ajili ya Pastore.Mpaka hapa tulipofikia, naamini tutakamilisha uhamisho wa Javier ndani ya siku 10 zijazo."
Klabu ambazo zimekuwa zikitajwa kumtaka Pastore ni Manchester United, Man City, Real Madrid, Barcelona , Chelsea na Inter Milan, huku mchezaji mwenyewe akiwahi kunukuliwa akisema angependa kuendelea kubaki Italia.
No comments:
Post a Comment