AMIN BAKHRESSA MWENYE SHATI JEUSI.
Nimejaribu kuangalia ligi ambazo zilikua zinashirikisha mabingwa wa mikoa katika vituo mbali mbali lakini nimeshtushwa kuona kwamba mwaka huu mkoa wa kinondoni haukua na timu ambayo ingeuwakilisha katika ligi ya kituo ili kuweza kupata timu ambazo zingekwenda daraja la kwanza kama ilivyo kwa Cosmo na Sifa Politani hii ni kutokana na ukiritimba ambao DRFA imeuleta kwa kuandaa ligi ya kanda ya Dar es salaam.
Sasa nabaki najiuliza hii ligi ya kanda ina faida gani wakati Kinondoni, Ilala, na Temeke tayari zinatambulika kimikoa zaidi ya wilaya katika mpira wa miguu na kwa kuthibitisha hilo tumeona katika michuano mbalimbali ya kitaifa hakuna mkoa unaoitwa Dar es salaam sasa hivi bali tuna mikoa kama hiyo nilioitaja hapo awali yaani ya KINONDONI, ILALA, na TEMEKE. Ukiangalia michuano ya Taifa Cup na Copa Cocacola je uhai wa Dar es salaam kimpira upo wapi? Na kama ingekua ipo mbona hatuioni pindi timu zinazotoka Dar es salaam zikishiriki michuano mbalimbali nje ya Dar es salaam? Nimekua kiongozi wa mpira katika ngazi ya wilaya mpaka ya Taifa nikiwa na Timu ya Villa Squad ya Dar es salaam katika ligi tofauti na sijawahi kupata ushirikiano wowote kutoka DRFA zaidi ya kusikia fitna na majungu ambacho chombo hiki kinaleta katika mpira wa Tanzania kwanza Management hawana zaidi ya Amini Bakhressa
Kwa kuthibitisha hili nyaraka mbalimbali za chama hiki hazikai ofisini zaidi ya kukaa ndani ya buti la gari la Bakhressa unapotoka nje utagundua kwamba viongozi wa vyama mbalimbali husika utawaona jinsi wanavyotoa maximum support kwa timu zinazotoka katika mikoa yao husika tofauti na DRFA ambayo hujikita zaidi pindi timu zinapopanda daraja na kukuta fomu za mapato zikiandika asilimia Fulani zinakwenda katika chama hiki ambacho hakina msaada wowote na timu husika.
Hebu tuiangalie Management ya DRFA na majukumu yake ni yapi in depth analysis kwangu mimi sioni zaidi ya kuzorotesha kama hivi Kinondoni haikutoa team katika ligi ya kituo na nikizidi kuangalia kwa umakini zaidi nimegundua haina management team zaidi ya mtu mmoja ambae ni Amini Bakhressa sasa sijui labda tuweke mjadala na kuitizama kwa sababu tunataka kulikomboa soka la Tanzania na kama tutaendelea kukumbatia vyombo au watu kwa maslahi yao hatutopiga hatua kwa sababu kuna mambo mengi ya kufanya zaidi kuliko kurundika vyama hewa ambavyo havina majukumu yoyote ndani ya soka la Tanzania.
Mdau wa blog IDDI GODIGODI.
No comments:
Post a Comment