Sekeseke la usajili wa kiungo Wesley Sneijder kutoka Inter Milan kuelekea Manchester United limechukua sura mpya baada ya taarifa za kampuni kubwa mavazi ya Nike kuingilia kati juu ya kukamilisha kwa usajili huo unaotajwa kuwa wenye thamani ya £35.2million.
Kampuni hiyo kubwa ya kimarekani ambayo ndio mdhamini wa jezi za mabingwa wa England inasemekana wapo tayari kulipa kiasi cha pesa kilichopungua katika matakwa ya mshahara anaotaka Sneijder ili kuhakikisha uhamisho huo unafanikiwa.
Nike waliwahi kufanya kitu cha namna hii wakati mbrazili Ronaldo De Lima alipohama kutoka Barcelona kwenda Inter wakati mahasimu wao wa kibiashara Adidas, ambao wanaidhamini Real Madrid, walihusika kwa kiasi kikubwa katika kurahisha mambo kwenye usajili wa Cristiano Ronaldo na David Beckham kwenda Benebeu.
United wamekuwa wakijaribu kukamilisha dili la usajili wa Sneijder ndani ya wiki hii, huku CEO David Gill akikacha safari ya US ili aweze kupata muda wa kuongea na Inter Officials jijini Milan.
Taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa United wapo tayari kulipa £35.2m wanayoitaka Inter lakini mazungumzo yamekwama katika matakwa binafsi ya mchezaji.Kambi ya mchezaji wanataka mshahara wa £200,000 kwa wiki huku Red Devils wakiwa tayari kulipa mshahara wa £170,000 per week.
No comments:
Post a Comment