Kocha msaidizi wa klabu ya Manchester United Rene Meulensteen amesema mchezaji wa Inter Milan Wesley Sneijder ndiye kiungo anayepaswa kusajiliwa na Red Devils msimu huu.
Rene ambaye ni mholanzi anaamini kuwa Sneijder ndio mtu sahihi anayepaswa kuja kuleta uhai katika dimba la uwanja ndani kikosi cha Man United.
"Hakuna Paul Scholes mpya, kama ambavyo hajawahi kutokea Roy Kean mpya, lakini Sneijder atakuwa mtu sahihi na atafiti vizuri ndani kikosi chetu, " Meulensteen aliuambia mtandao wa Voetbal International.
"Siwezi kuona mchezaji mwingine mzuri zaidi kwa timu yetu.Nasema hivi sio kwa sababu mimi mholanzi.Nimefanya kazi hapa kwa muda sasa, naijua timu ndani na nje na nafahamu kuwa usajili wa Wesley utakuwa mzuri sana.
Anaonekana kama mtu sahihi wa kucheza na wachezaji kama Hernandez, Rooney, Park, Ahley Young, Valencia, Nani na Giggs, na kikubwa zaidi Wesley ana uzoefu wa lazima katika kucheza katika level za juu.
Sijui kuhusu mipango yake ya baadae ndani ya Inter, kama ataondoka au kama bei yake ni nafuu, lakini katika suala ya uwezo wa kucheza soka, Nasema Sneijder ndio mtu sahihi kusajiliwa na United kwa sasa."
BERBATOV + CASH FOR BASTIAN SHWEINSTEIGER
Wakati huo huo gazeti la Daily Star linaripoti kuwa kocha mkuu wa Mabingwa wa England Manchester United anajipanga kumtumia mshambuliaji Dimitar Berbatov katika kufanikisha uhamisho wa Bastian Schweinsteiger kutoka Bayern Munich.
Ferguson ambaye amekuwa akimtamani Schweinsteiger kwa muda mrefu anamuona kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani kama mtu sahihi wa kwenda kuziba mapengo katika safu ya kiungo mkabaji ndani ya kikosi cha Red Devils.
Hivyo katika kujaribu kuwashawishi Bayern SAF anapanga kumtumia Berbatov ambaye amekuwa akizivutia klabu kadhaa barani ulaya ikiwemo Bayern katika deal hilo ambalo pia litahusisha kiasi cha pesa.
HATIMAYE CHARLIE ADAM KUELEKEA ANFIELD
Klabu za Liverpool na Blackpool zimefikia muafaka katika uhamisho wa Nahodha wa Blakcpool Charlie Adam kuelekea Anfield.
Scotland midfielder mwenye umri wa miaka 25, sasa atasafiri kwenda Merseyside kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kukubaliana na Liverpool kuhusu matakwa yake binafsi.
Liverpool walikuwa wakimfuatilia Adam kwa miezi takribani 6, leo jioni hii wamethibitisha kwamba wamekubaliana na "Seasiders" kuhusu bei ya kumsajili Charlie Adam.
No comments:
Post a Comment