Search This Blog

Monday, July 18, 2011

BARCA WAPEWA WIKI 2 KUMALIZANA NA FABREGAS


Mabingwa wa ulaya BARCELONA wamepewa wiki mbili kukamilisha uhamisho wa Cesc Fabregas kwa kulipa pesa inayotakiwa na Arsenal £40million, la sivyo Fabregas ataendelea kubaki Emirates.
Jana usiku mmoja wa kati ya viongozi wa juu wa Barca alisema: "Arsenal wametufahamisha kuwa ikiwa hatukamilisha uhamisho wa Cesc mpaka wa mwisho wa mwezi huu then Fabregas atabaki London."

"Pia walituambia hawakuwa wakipenda kumuuza nahodha wao ingawa wapo tayari kupokea ofa Cesc kurudi nyumbani.Walisisitiza pia kuwa wamekuwa wakilishughulikia suala hili fairly kwa mchezaji na Barcelona.Wamesema hawapo tayari kuendelea kusubiri zaidi, na watafunga mjadala wa uhamisho huu kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

"Tunaelewa kwamba hakuna uwezekano wa Arsenal kumuuza Cesc kwa pesa tuliyoweka mezani lakini uamuzi wa mwisho unabakia kwa raisi wetu Sandro Rossell."

No comments:

Post a Comment