Search This Blog

Monday, June 20, 2011

YANGA KUTANGAZWA RASMI KUCHEZA CECAFA KAGAME CUP KESHO


Klabu ya Yanga inatarajiwa kutangazwa rasmi kurejea katika michuano ya CECAFA Kagame Cup kesho habari kwa mujibu mtu wa ndani wa shirikisho hilo.

Yanga ambayo ilikuwa imefungiwa kwa miaka 3 kushiriki michuano hiyo baada ya kugomea mchezo wao dhidi ya Simba mwaka juzi, iliomba msamaha kwa CECAFA hivi karibuni na wakapewa masharti ambayo walipaswa kuyatimiza ili waweze kukubaliwa msamaha wao na kupewa nafasi ya kushiriki michuano hiyo mwaka huu.

1 comment:

  1. shaffii,mpira wetu hautakua hata siku moja kama tutakosa kujua vipaumbele ni vipi,kucheza na kushinda kagame sio ishu kama kufika nusu fainali ya mabingwa au shirikisho coz kule ndo kwenye exposure kaka,Nani anaangalia kagame?mchezaji gani katoka kiviile kupitia kagame?haya ni maswali ambayo yanakupa picha ya kujua kua hii si michuano ya kuikodolea macho kwa nguvu zote,inabidi hizi timu za tanzania ziwe focus na zitengeneze mikakati ya kujenga vikosi vyao,ukiiangalia Azam utagundua kua baada ya miaka michache itakuja dominate soka la bongo na kufanya vizuri kwenye michuano ya afrika kutokana na Mikakati walionayo hasa ya kuwekeza katika soka la vijana na kufanya usajili wa kiufundi sio wa kishabiki kama wa Simba na yanga.Safari ya mpira wa Mafanikio kwa level ya kimtaifa kwa Tanzania bado ni ndefu sana na tunahitaji Football reform programme ambayo itakua muongozo wa namna ya utawala na uendeshaji wa programm za mpira hapa nchini,Sio siri mimi nilikua mmoja kati ya watu niliekua na muamini sana Tenga but kwasasa nimegundua hana jipya na hana uwezo wa kutuvusha hapa tulipotumbukia,tunahitaji mtu ambae ni creative,commmited na awe supported na hiyo reform programme ambayo kila kiongozi atahitajika kutekeleza mikakati ilioko ndani ya hiyo program na atapimwa uwezo wake kwa kuja na sera ambazo zita elezea ni kwa namna gani atatekeleza program hiyo coz tunachokosea ni kuwaachia watu wachache sana watengeneze program za mpira na matokeo yake ndo tunaishia kwenye ubabaishaji kama huu tunaoendelea nao,tuandae Football reform development programe ya mwaka 2012-2025 then tuandae sera na mikakati ya kutekeleza mikakati hiyo.TFF walivyo kwasasa na watu waliomo mule tusitegemee chochote zaidi ya kupata habari tu za michezo

    ReplyDelete