Search This Blog

Tuesday, June 28, 2011

ON THIS DAY : MAN UTD ALIPIGWA 'WASH' / 'SUPER' kwenye fainali ya UEFA Champions League.

Ni mwezi mmoja umepita sasa tangu Man utd walipofanywa kitu mbaya na Fc Barcelona kwenye mchezo wa Fainali ya UEFA Champions League mnamo may 28 kwenye dimba la Wembley.
katika fainali hiyo Man Utd hawakupata kona hata moja na mashabiki wa soka walikifananisha kitendo hicho kama kufungwa 'woshi' kwenye mchezo wa POOLTABLE au kupigwa 'Super'

kwenye mchezo wa DRAFT.



1 comment:

  1. Kwa ujumla fainali ile imewafanya Manchester wagundue wenyewe kwamba kumbe bado wanahitaji maboresho katika maeneo muhimu uwanjana na ndio maana hadi sasa imeanza usajili kwa fujo sana ikiwa tayari imewanasa ASHLEY YOUNG, JONES na DE GEA akifuata.

    Kwa ujumla kufungwa kwao na Barca kulionyesha wazi kwamba ili waweze kushindana tena kuuwania Ubingwa wa Ulaya mwakani wanahitaji kusajili katika maeneo muhimu ikiwemo yale ya kuziba mapengo ya wachezaji walioamua kutundiga daluga kama vile PAUL SCHOLES pamoja na EDWIN VAN DER SAR. Kwa usajili wa ASHLEY YOUNG na JONES nafikiri ni usajili ambao wameongeza tu nguvu katika yale maeneo ambayo tayari wako vizuri zaidi.

    Ili waweze kukabiliana na changamoto za kuchukua Ubingwa wa Ulaya mwakani wanapaswa waongeze nguvu katika eneo la kiungo cha kati ambapo ndipo hasa udhaifu wao ulipo. Kama Fergie ataweza kupata saini ya mojawapo ya wachezaji kama vile WESLEY SCHNEIDER, LUKA MODRIC, DE ROSSI, NASRI etc basi watakuwa moto mwakani.

    ReplyDelete