MKURUGENZI WA MASOKO WA TBL,DAVID MINJA (KUSHOTO) AKIBADILISHANA NYARAKA NA VIONGOZI WA CECAFAZA M/KITI LEODEGAR TENGA ( KATI) NA KATIBU MKUU NICHOLAS MUSONYE ( KULIA ).
Mashindano ya klabu bingwa katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na kati maarufu kama KAGAME CUP yamezinduliwa rasmi leo hii jijini Dar Es Salaam,
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa CECAFA Leodegar Tenga amesema mashindano ya mwaka huu yataitwa KAGAME CASTLE CUP baada ya kupata udhamini wa Kampuni ya bia nchini Tanzania,TBL kupitia kinywaji chake cha Castle Lager.
Naye mkurugenzi wa masoko wa kampuni hiyo Bwana David Minja amesema TBL imedhamini mashindano hayo kwa kiasi cha pesa ambacho hakitazidi shilingi za kitanzania Milioni 300,
pesa hizo zitatumika kulipia malazi,chakula,usafiri wa ndani na kwa ajili ya kuyatangaza hayo mashindano kupitia vyombo mbali mbali vya habari.
Mlezi wa mashindano hayo,Raisi Paul Kagame wa Rwanda atatoa jumla ya dollar 60,000 za Marekani zikiwa ni kwa ajili ya zawadi mbali mbali za washindi.
Mashindano hayo yanatarajia kuanza hapo siku ya Jumamosi ya tarehe 25/6/2011 na kushirikisha timu bingwa wa nchi wananchama wa CECAFA.
No comments:
Post a Comment