MATATIZO YA KIUCHUMI KWENYE MCHEZO WA SOKA HASA KWA UPANDE WA VILABU YAMEKUWA YAKIONGEZEKA SIKU HADI SIKU NA YANATISHIA UHAI WA MCHEZO HUU UNAOPENDWA ULIMWENGUNI KOTE .
SUALA HII LINAHUSIANA NA UPUNGUFU WA MASHINDANO KWENYE LIGI MBALIMBALI AMBAKO LILE 'GAP' BAINA YA VILABU VIKUBWA NA VIDOGO LIMEKUWA LIKIONGEZEKA . KUNA HOJA NYINGI ZA KUJADILI NA MIKUTANO MINGI IMEFANYIKA JUU YA KUTAFUTA USULUHISHO KWENYE HILI , NA LEO HII NIMEKULETEA HOJA ZANGU KUMI ZA MSINGI AMBAZO NADHANI KAMA ZIKIFANYIWA KAZI ZINAWEZA KUPUNGUZA KAMA SI KUONDOA KABISA TATIZO HILI.
1 . VYAMA VYA SOKA KWENYE KILA NCHI LAZIMA VIWE NA JUKUMU LA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA UTAWALA , UCHUMI NA MAJUKUMU YOTE YA KIBIASHARA KWENYE VILABU .
2 . MIFUMO YA KUTOA LESENI KWA KILA CHAMA AU SHIRIKISHO LA SOKA KWA NCHI HUSIKA LAZIMA IHUSISHE SHERIA NA TARATIBU MBALIMBALI ZA BIASHARA , HATUA ZA KUMLINDA NA KUMSHAWISHI MSHANGILIAJI KWENDA UWANJANI PAMOJA NA TARATIBU ZA KUKUZA NA KUENDELEZA SOKA LA VIJANA
3 .KLABU ZOTE LAZIMA ZIHAKIKISHE ZINAPELEKA RIPOTI ZA MWAKA ZA AKAUNTI NA MATUMIZI YA FEDHA PAMOJA NA KUWEKA WAZI AKAUNTI NA RIPOTI NA BAJETI KWA AJILI YA MWAKA UNAOFUATA .
4 .VYAMA VYA SOKA KATIKA KILA NCHI LAZIMA VIHAKIKISHE KUWA VIONGOZI WOTE WANAOHUSIKA NA MCHEZO WA SOKA MATHALANI MAMENEJA , MAWAKALA , MARAIS WA VILABU , WAKURUGENZI , WAMILIKI WA TIMU NAKADHALIKA SI WATU WENYE REKODI AU HISTORIA YA UHALIFU MATHALANI MAKOSA KAMA UKWEPAJI WA KODI NA MENGINEYO .
5 . MARAIS , WAKURUGENZI , NA MAMENEJA WA VILABU LAZIMA WAVIWEKE WAZI VYANZO VYAO VYA MAPATO AMBAYO YANAWEKEZWA KWENYE TIMU .
6 . LAZIMA UWEPO UTARATIBU WA MAWASILIANO YA WAZI BAINA YA MASHIRIKISHO NA VYAMA VYA SOKA NA VILABU NA MAKAMPUNI AMBAYO YANAHUSIKA KATIKA KUSAIDIA MASHINDANO MBAMBALI KWENYE KILA LIGI ILI KUGAWANYA MAPATO TOKA KWENYE MCHEZO KWA USAWA.
7 . LAZIMA IUNDWE MIFUMO YA BIASHARA NA UCHUMI KWENYE SOKA AMBAYO INAELEWEKA ILI KUENDELEZA SOKA KWA VIJANA.
8 . VYAMA VYA SOKA LAZIMA VIWEKE SHERIA ILI VIKOSI KWENYE VILABU VIWE NA ASLIMIA 50 YA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUZWA KWENYE NCHI AMBAYO LIGI HUSIKA INACHEZWA.
9 . LAZIMA VYAMA VYA SOKA VIPIGE MARUFUKU USAJILI WA WACHEZAJI WA KIGENI WALIO KWENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 . WAGENI AMBAO WANASAJILIWA NI LAZIMA WAWE WACHEZAJI WA KIMATAIFA KATIKA TIMU ZA TAIFA WANAKOTOKA.
10 . VYAMA VYA SOKA LAZIMA VIPIGE MARUFUKU MIKOPO YA WACHEZAJI WALIO NA UMRI SAWA WENYE HAKI ZA KIUCHUMI ZA KLABU AU MCHEZAJI BINAFSI .
NAKARIBISHA SANA MITIZAMO YENU WADAU!
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteMlanzi George au The great G.
ReplyDeleteHayo nimapendekezo mazurisana hasa pendekezo number 3 kudhibiti eneo la mapato na matumizi. Eneo hili bado ni changamoto.
pia kwakuongezea lazima kuwe na Website ktk kila club