Search This Blog

Thursday, May 26, 2011

SIMBA SPORTS CLUB YAWASILI CAIRO.







Wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya klabu bingwa ya barani Afrika wekundu wa msimbazi Simba sports club, wamewasili jijini Cairo asubuhi ya leo tayari kwa mchezo wa kuamua timu itakayofuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa wa Afrika.

Simba wataikabili Wydad Cassablanca ya Morocco katika mchezo utakaopigwa kwenye Petrosport stadium huko Cairo Egypt mnamo May 28, hapo siku ya jumamosi.

Msafara wa jumla ya watu 26, umeondoka usiku wa kuamkia hivi leo kuelekea Cairo, lakini mshambuliaji Ahmed Ally Shiboli akisalia nyumbani, baada ya kuumia kwenye mazoezi ya timu hiyo, kule visiwani Zanzibar.



Ndani ya shirikisho la soka la Tanzania TFF, raisi wa shirikisho hilo Leodgar Chilla Tenga anasema kwamba, kwa upande wake ni muumini wa uzalendo, japo anapenda kuona unazi ukiwepo, kwa sababu ya ushindani.

Tenga anasema kwamba, Simba inapaswa kusoma kupitia makosa yaliyofanywa na waliokuwa mabingwa wa Afrika TP Mazembe,lakini kama nchi kila mmoja anapaswa kuwaunga mkoni wawakilishi hao wa Tanzania bara, zaidi ya yote akitoa pongezi kwa uongozi.

Wakati huo huo, Tenga amesema kwamba, kusema kuwa mashindano ya Cecafa ya Kagame yamehamishiwa nchini Tanzania hapana kwani, bado kuna mambo mengi yanatakiwa kufanyika, na zaidi akiwaomba Watanzania walifanyie kazi jambo hilo, ili fedha zipatikane kwa ajili ya kufanyika.

Tenga anasema kwamba ni muhimu sana kwa timu zetu kupata nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa, kwa sababu ya kuwapa uzoefu wachezaji wa Tanzania, ili kuwa bora, hivyo sasa wanachoangalia zaidi ni kupata mtu atakasaidia chakula usafiri na malazi.

No comments:

Post a Comment