Search This Blog

Monday, May 23, 2011

MICHUANO YA KILI TAIFA CUP YAZIDI KUSHIKA CHATI ARUSHA.




Michuano ya Kili Taifa Cup 2011 hatua ya robo fainali iliyoanza jana huko jijini Arusha imeendelea tena leo kwa michezo miwili iliyopigwa kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid
Katika mchezo wa kwanza ulioanza majira ya saa 8 mchana umeshuhudia mkoa wa Mbeya Mapinduzi Stars ukifuzu hatua ya nusu fainali baada ya kuwafunga mkoa wa Ruvuma (Ruvuma Warriors) mabao 3 kwa 2.
Mabao ya Mapinduzi Stars yamefungwa na Juma Mpola pamoja na Gaudance Mwaikimba aliyepachika mabao mawili huku mabao ya Ruvuma Worrioes yakikwamishwa nyavuni na Alli Bilali huku bao la pili akifunga kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa mbeya Jumanne Elfadhili kumchezea vibaya Alli Bilali katika eneo la hatari katika dakika ya 89 ya mpambano huo.
Na katika mchezo wa pili timu ya Taifa ya vijana ya umri chini ya miaka 23 leo imesukumwa nje kwenye mashindano hayo baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penati dhidi ya mkoa wa Kagera (Lweru Eagles).
Timu hizo zilimaliza dakika 90 zikiwa zimechoshana nguvu baada ya kufungana mabao 2 kwa 2 na ndipo sheria ya mikwaju ya penati ilipotumika ili kumpata mshindi ambapo Rwelu Eagles mkoa wa Kagera wakapata penati 3 wakati timu ya vijana imepata penati moja.

Nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo inatarajiwa kuchukua nafasi kesho ambapo Mwanza Heroes itakipiga na Ilala wakati nusu fainali ya pili itachezwa Mei 25 ambapo Mei 26 itakuwa mapumziko huku mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ukipigwa Mei 27 na fainali itachezwa Mei 28.

No comments:

Post a Comment