Search This Blog

Tuesday, October 15, 2013

TUJIKUMBUSHE: MASHABIKI WA CHELSEA FC WATWAA KOMBE LA SERENGETI FIESTA SOCCER BONANZA MWANZA.

Meneja Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga (kushoto),akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Chelsea ya Mabatini Mwanza jioni ya leo baada ya kuibuka kidedea kupitia matuta.
TIMU ya mpira wa miguu ya Chelsea FC ya Mabatini Mwanza, leo imefanikiwa kutwaa Kombe la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililokuwa likifanyika jioni ya leo katika uwanja wa Polisi Mabatini,ambapo timu zaidi ya nane zilichuana na hatimaye kumpata mshindi,aliyejinyakulia kikombe na kitita cha shilingi laki 3 kwa mshindi wa kwanza huku mshindi wa pili akipewa kitita cha shilingi laki 2.

Nahodha wa timu hiyo akiwa amenyanyua kombe juu na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo.

Baadhi ya mashabiki wa timu ya Chelsea wakishangilia baada ya kushinda kwa njia ya matuta.

Mwakilishi wa Bia ya Serengeti wa Mwanza Mwanza Joan Semuguruka (kushoto), akimkabidhi zawadi ya mshindi wa pili Nahodha wa timu ya FC Barcelona.

Joan Semuguruka(kushoto) Nahodha wa timu ya Chelsea,huku akishuhudiwa na Meneja wa Vipindi vya Clouds FM, Sebastian Maganga aliyesimama katikati yao.
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo wakishuhudia mpambano huo.

Timu ya Arsenal, ikipambana na Timu ya FC Barcelona ya Mabatini katika moja ya mchezo wa Nusu fainali,ambapo Barcelona iliibuka na ushindi na kutinga hatua ya Fainali.

Mmoja wa wachezaji wa timu ya Real Madrid, akipiga penalty kwenye mpambano wa kuwania kufuzu hatua ya kuingia fainali ya mchezo huo, ambapo Real Madrid ilifukwa kwa mkwaju na timu ya Chelsea.

Mtangazaji wa Clouds FM, Arnold Kayanda aliyesimama katikati ya mashabiki,akitangaza matokeo ya mechi hizo kabla ya kufikiwa kwa hatua ya fainali.

Meneja wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga,akiwamiminia Bia ya Serengeti baadhi ya mashabiki walifika kushuhudia baadhi ya mechi zilizokuwa zikiendelea Kiwanjani hapo.
Kati ya mashabiki waliohudhuria Kiwanjani hapo wakifatilia baadhi ya matukio yaliyokuwa yakijili uwanjani hapo.

SERENGETI FIESTA SOCCER BONANZA SASA ZAMU YA DAR

Tamasha kubwa la Serengerti Fiesta Soccer Bonanza mwaka huu limeingia msimu wa tatu na limefanyika kwa mafanikio makubwa sana katika mikoa ya Kigoma,Singida,Morogoro,Mwanza na sasa ni zamu ya jiji la Dar Es Salaam.
Tamasha hilo linataraji kufanyika siku ya Jumamosi ijayo ya tarehe 19/10/203 kwenye viwanja vya Leaders kuanzia saa nne asubuhi.
Mashabiki wa vilabu vinane vya ulaya ( Manchester Utd,Chelsea,Liverpool,Arsenal,Real Madrid,Fc Barcelona,Ac Milan na Bayern Munich ) watapambana kumpata bingwa wa mkoa wa Dar Es Salaam.

Mashabiki wa Arsenal waliibuka washindi kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya Manchester Utd kwenye uzinduzi wa bonanza la mwaka huu huko mkoani Kigoma, mkoani Singida mashabiki wa Liverpool wakafanikiwa kubeba ndoo baada ya kuwafunga mashabiki wa Bayern Munich mabao 2-0, huku mashabiki wa Chelsea wakiibuka mabingwa kwenye mikoa ya Morogoro na Mwanza.



Monday, October 14, 2013

KUELEKEA DSM DERBY: YANGA WAENDA PEMBA KUWEKA KAMBI


Baada ya kuichapa timu ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika mjini Bukoba mwishoni mwa wiki, jana kikosi cha Young Africans kilirejea jijini Dar es salaam na leo asubuhi kikitua kisiwani Pemba ambapo kitakua kambini kwa muda wa wiki moja.

Young Africans inaweka kambi kisiwani Pemba ikiwa ni mara ya pili mfululizo katika mchezo wake dhidi ya watani wa jadi Simba SC, ambapo kambi ya awali iliwafanya vijana wa jangwani kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza 'Diego'.

Msafara wa watu 38 wakiwemo wachezaji wote 29 waliosajiliwa kwa ajili yakuichezea Yanga msimu huu na viongozi 9, watakua kisiwani pemba katika maandalizi ya mchezo huo ambao ni muhimu kwa Yanga ili kujiweka katika mazuri ya kuongoza Ligi Kuu na baadae kuteteta tena Ubingwa wake.

Mara baada ya kuwasili kisiwani Pemba leo asubuhi kwa ndege tatu za kukodi kikosi kimefanya mazoezi yake ya kwanza katika uwanja wa Gombani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mcezo dhidi ya Simba SC oktoba 20, 2013.

Ikiwa ni takribani siku sita kabla ya kupamba na Simba SC siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kikosi cha mholanzi kimeamua kuweka tena kambi katika visiwa hivyo tulivu kwa lengo la kusaka ushindi.

Kocha Mkuu Brandts amesema anatambua kikosi chake kinakabiliwa na mchezo mgumu, haswa ikizingatiwa wanapokutana watani wa jadi mechi huwa inakua ngumu sana lakini kwa sasa anakindaa kikosi chake ili kiweze kuendeleza wimbi la ushindi.

"Pemba ni sehemu nzuri, tulikuwepo huku mwishoni mwa msimu uliopita kwa ajili ya maandalizi dhdi ya Simba na tuliibuka na ushindi wa mabao 2-0, uwanja wa mazoezi mzuri na hali ya hewa ni nzri vitatutaongeza chachu ya ushindi kufuatia kuwa sehemu tulivu" alisema Brandts

Wachezaji waliondoka kwenda Pemba ni:

Walinda Mlango: Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul.

Walinzi wa Pembeni: Mbuyu Twite, Juma Abdul, Issa Ngao, David Luhende na Oscar Joshua.

Walinzi wa Kati: Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani 'Cotton', Rajab Zahir na Ibrahim Job.

Viungo wa Ulinzi: Athuman Idd 'Chuji', Frank Domayo na Salum Telela na Bakari Masoud.

Viungo Washambuliaji: Haruna Niyonzima, Nizar Khalfani na Hamis Thabit.

Washambuliaji wa Pembeni: Mrisho Ngassa, Saimon Msuva na Abdallah Mguhi 'Messi'

Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerson Tegete, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Reliants Lusajo na Shaban Kondo

SOURCE: YOUNGAFRICANS.CO.TZ

MATOKEO YA NANI MTANI JEMBE KUANZA KUTANGAZWA.

Na Mwandishi Wetu,
Mbeya Bia ya Kilimanjaro Premium Lager itaanza kutangaza matokeo ya kampeni ya Nani Mtani Jembe inayoshirikisha mashabiki wa timu kubwa nchini za Simba na Yanga kupitia vyombo vya habari kila siku. Meneja wa Bia ya hiyo, George Kavishe aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Shindano hilo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika kwenye kiwanda cha bia cha TBL Jijini Mbeya. 

Katika shindano hilo Kilimanjaro inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao. Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu nyingine. Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro ambayo kwenye kizibo chake kuna namba ya kushiriki.

 Alisema baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440. Alisema baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 1,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 1,000 kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza shilingi 1,000 kutoka kwa Simba. 

Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku kuanzia leo Jumatatu hadi siku ya mwisho wa shindano hilo Desemba 14, mwaka huu. Kavishe alisema kuwa mashabiki watakaoshiriki kwenye shindano hilo kila siku pia watanufaika kwa kuchaguliwa watu 400 watakaokuwa wametuma mara nyingi zaidi ambao pia watazawadiwa shilingi 5000 kila mmoja na kufanya kiasi cha fedha zinazokwenda kwa mashabiki kuwa shilingi milioni mbili kila wiki. 

Katika uzinduzi huo wa Nani Mtani Jembe kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Simba iliwakilishwa na Mwenyekiti wake Ismail Aden Rage na Yanga iliwakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Yanga Mohamed Bhinda. Mashabiki wanaweza kufatilia matokeo kila dakika kupitia tovuti maalum ya Nani Mtani Jembe ambayo ni https://cms.rasello.com/kili.
Mwenyekiti wa Simba SC, Aden Rage akiwakabidhi wafanyakazi wa TBL Mbeya wanaoshabikia Simba baada ya kuwashinda wanaoshabikia Yanga katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. Kampeni hiyo inayoendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager inawashindanisha mashabiki wa Simba na Yanga.
 Mwenyekiti wa Simba SC, Aden Rage akimvalisha Richard Kagosi skafu ya Simba baada ya kushiriki shindano la kuvuta kamba
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Mohammed Bhinda akimkabidhi Bahati Msokwa zawadi ya begi baada ya kushiriki mchezo wa kuvuta kamba
Wafanyakazi wa TBL Mbeya Frank Kasege (kushoto) na Bahati Msokwa (kulia) wakishindana kupiga danadana katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Mohammed Bhinda akimkabidhi Mariam Martin zawadi baada ya timu yake kushinda mchezo wa kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya
Wafanyakazi akinamama wa TBL Mbeya wakishindana kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa Simba SC, Aden Rage akishangilia na wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Mbeya wanaoshabikia Simba baada ya kuibuka washindi katika shindano la kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akitambulisha kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa TBL Mbeya mwishoni mwa wiki.

KAMATI YA RUFANI YA MAADILI YAFANYA MAPITIO


Kamati ya Rufani ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana jana (Oktoba 13 mwaka huu) kusikiliza maombi ya mapitio (revision) na mwongozo ya uamuzi wa Kamati ya Maadili.

 
Sekretarieti ya TFF iliwasilisha maombi ya mapitio kwa Kamati hiyo ya juu kabisa ya masuala ya maadili kutokana na ugumu wa utekelezaji wa uamuzi wa Kamati ya Maadili juu ya mashauri nane yaliyowasilishwa mbele yake.

 
Kamati ya Rufani ya Maadili itaendelea na kikao chake kesho (Oktoba 15 mwaka huu), na baadaye itakutana na waandishi wa habari (saa 10 jioni) kwa ajili ya kutangaza uamuzi wake juu ya mwongozo ulioombwa na Sekretarieti ya TFF.

 

KIONGOZI WA MWENGE AFUNGUA KITUO CHA IDYDCC

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Juma Ali Amir amefungua kituo cha kwanza cha Football for Hope kilicho mkoani Iringa kwa kuwataka wananchi kukituia vizuri ili wanufaike na huruma za kijamii zinazotolewa na taasisi ya IDYDC pamoja na kuendeleza mpira wa miguu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho jana (Oktoba 13 mwaka huu), kiongozi huyo amesema taasisi ya IDYDC (Iringa Development of Youth, Disabled and Child Care) wamefanya vizuri kuamua kutumia mpira wa miguu kusaidia jamii kwa kuelimisha juu ya mambo mbalimbali kama ugonjwa wa ukimwi, kusaidia walemavu, haki za watoto na afya ya jamii.


Naye Mwakilishi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Patrick Onyango amesema amefurahishwa na kukamilika kwa kituo ambacho kitasaidia jamii.


Amesema idadi kubwa ya watu waliofika kwenye uzinduzi huo inadhihirisha ni kiasi gani kituo hicho kitakuwa na matokeo mazuri kwa jamii.



Onyango alisema hicho ni kituo cha 14 kukamilika kati ya 20 vinavyojengwa barani Afrika ikiwa ni mpango wa FIFA kurudisha kwa jamii mafanikio iliyopata kwenye fainali za kwanza za Kombe la Dunia barani Afrika.


Kituo hicho kina uwanja mdogo wa mita 20 kwa 40 uliowekwa nyasi bandia, jengo lenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya semina, chumba cha kupimia ukimwi, chumba cha ushauri nasaha, maktaba na ofisi.


Zaidi ya dola 270,000 za Marekani zimetumika kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kilicho eneo la Mtwivila, Iringa mjini.

 

KESSY KUSIMAMIA MECHI YA KOMBE LA DUNIA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Mtanzania Lina Kessy kuwa kamishna wa mechi ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20 kati ya Botswana na Afrika Kusini.

 

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza itachezwa nchini Botswana kati ya Oktoba 25 na 27 mwaka huu. Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi hiyo namba tisa.

 

Waamuzi hao wataongozwa na Pamela Majo atakayepuliza filimbi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Rudo Nhananga, namba mbili ni Stellah Ruvinga na mezani atakuwepo Tambudzi Tavengwa.

 

Boniface Wambura Mgoyo

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

ANGALIA PICHA ZA MASHINDANO YA GOLF YA KUMPONGEZA MISS TANZANIA YALIOFANYI​KA MOROGORO

Bango la kuingia uwanja wa golf wa Gymkan mkoani morogoro ambapo ulichezwa mchezo wa kumpongeza miss tanzania 2013 
Afisa uhusiano wa kamati ya Miss tanzania akiwa na miss tanzania katika  picha ya pamoja  
Mchazaji wa golf Abood akiwa purukushani za mchezo wagolf  katika mchezo ulioandaliwa na chama cha mchezo wa golf mkoa wa Morogoro ulioandaliwa kwa ajili ya kumpongeza Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Redds Miss tanzania.Mshindi huyo ameambatana na mshindi wa pili Latifa Mohamed na Mshindi wa tatu Clara Bayo.
Miss tanzania namba 2 Latifa Mohamed Akiongoza na Mmoja wa wachezaji wa mchezo wa Golf mkoa wa MorogoroWakati wa mashindano ya kumpongeza Miss tanzania 2013.
 Mchezo huo uliondaliwa na chama cha mchezo wa Golf Mkoa wa morogoro na kufanyika katika viwanja vya Gymkana mkanai morogoro ulikuwa na lengo la kumpongeza Miss tanzania Happiness kwa kuwa Hapiness alikuwa ni mkazi wa morogoro na amekulia morogoro japo ameshinda taji hilo akiwakilisha mkoa wa dodoma.
 Miss tanzania 2013 Happiness Watimanywa kulia akiongozana na mshindi wa tatu Clara Bayo wakti wa mashindano hayo yaliendelea katika uwanja wa Gymkana .
Mchazaji huyu wa Golf akifunga Point Muhimu wakati wa Mashindano ya kumpongeza miss tanzania 2013.
Yusufali Akiangalia uelekeo wa gOlf wakati wa Mipigo Mirefu ya watu watatu watatu wakati wa mashindano hayo asubuhi ya leo
Mwenyekiti wa  wa Chama cha Mchezo wa golf Mkoa wa Morogoro akifunga point Muhimu katika mashindano hayo ya kumpongeza miss tanzania 2013
Miss tanzania namba tatu Clara Bayo Akikabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza wa mashindano ya kumpongeza Miss tanzania 2013
Mama Sherida chilipochi akipokea zawadi ya jumla kwa wanawake kutoka kwa miss tanzania namba mbili Latifa Mohamed
Miss tanzania hapiness Akimkabidhi zawadi Mshindi wa jumla Hassan Dendegu mara baada ya kumalizika mashindano ya kumpongeza miss tanzania yaliondaliwa na chama cha golf mkoa wa morogor leo. PICHA NA MATUKIO NA MICHAPO

Sunday, October 13, 2013

MATOKEO VODACOM PREMIER LEAGUE: AZAM FC YAIPIGA 3 - 0 JKT, MTIBWA SUGAR YAUA 5, COASTAL YAPIGWA NA ASHANTI


Mgambo JKT 0 -1 Mbeya City
Azam FC 3 - 0 JKT Ruvu
Mtibwa Sugar 5 - 2 JKT Oljoro
Ruvu Shooting 1 - 0 Rhino Rangers

NIGERIA YAANZA VIZURI SAFARI YA KWENDA BRAZIL: YAIPIGA ETHIOPIA 2-1


Ushindi wa Super Eagles ya Nigeria ugenini dhidi ya Ethiopia umeipa matumaini ya kushiriki kombe lijalo la dunia.

Ethiopia ilipata goli la kuongoza kunako dakika ya 56 kupitia mchezaji Asefa.

Bao hilo halikukaa kwa muda mrefu, kunako dakika ya 67 mkwaju uliopigwa na Emanuel Emenike uliishia langoni na kuwa 1-1.

Ethiopia watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kutumia nafasi kadhaa walizopata na pengine waliponea chupuchupu kunako dakika 77 ambapo mkwaju wa Nigeria uligonga mlingoti wa lango na kurudi ndani.

Goli la ushindi la Nigeria lilipatikana kwenye dakika ya mwisho kwa njia ya penalty iliyofungwa na Emmanuel Emenike na kupalilia njia kwa bingwa hao wa Afrika ya kwenda Brazil.

DIDIER DROGBA, KALOU NA GERVINHO WAIADHIBU SENEGAL: WAIPIGA 3-1 KATIKA MTOANO WA KUELEKEA BRAZIL 2014


Mabao 3 yaliyofungwa na washambuliaji Didier Drogba, Gervinho na Salomon Kalou yametosha kuiongezea matumaini Ivory Coast ya kushiriki fanali za kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.

Goli la kufutia machozi upande wa Senegal lilifungwa kimiani na mshambuliaji wa Newcastle Papiss Demba Cisse.

Mechi ya pili itachezwa mwezi ujao nchini Morocco kwa sababu Senegal inatumikia adhabu ya kutochezea kwenye uwanja wa nyumbani.

Burkinafaso 3 Algeria 2
Penalti ya dakika za mwisho iliyopewa Burkinafaso katika mazingira ya kutatanisha iliiwezesha timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Algeria.
Hadi dakika ya 85 matokeo yalikuwa magoli 2-2 kabla ya Burkinafaso kupata penalti iliyowawezesha kuondoka na ushindi mdogo.

SIMBA YAIFUMUA PRISONS 1 - 0 NA KUENDELEA KUONGOZA LIGI KUU YA VODACOM



YANGA WALIVYOWALAMBISHA SUKARI KAGERA SUGAR - YAITANDIKA 2-1 NYUMBANI KWAO


Kikosi cha Kagera Sugar. Picha na www.bukobasports.com
Kikosi cha Yanga
Waamuzi na Timu Kapteni wakiteta jambo muda mfupi kabla ya mpira kuanza.
Benchi la Yanga.
Benchi la Kagera Sugar.
Raha ya ushindi.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia. Kutoka kushoto ni Mbuyu Twite, Hamis Kiiza na Mrisho Ngasa.
Chukua tano kwanza ....Asante!!
Patashika Uwanjani.
Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza kuangalia pambano la Yanga na kagera Sugar.