Search This Blog

Monday, December 10, 2012

FRANSIC MIYEYUSHO AZIMA NGEBE ZA NASSIBU RAMADHANI


BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO AZIMA NG'EBE ZA NASSIBU RAMADHANI



Bondia Fransic Miyeyusho akionesha ufundi wake kwa kumtupia masumbwi Nassibu Ramadhani wakati wa Mpambano wao wa kugombania ubingwa wa WBF uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Miyeyusho alishinda kwa T.K.O ya raundi ya kumi picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
 
Bondia Mohamed Matumla  kulia  akimuhadhibi Doi Miyeyusho wakati wa mpambano huo usiku wa kuamkia  leo Matumla alishinda kwa K,O raundi ya pili Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Juma Fundi kushoto na Fadhili Majia wakioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki Majia alishinda kwa pointiPicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Miyeyusho kushoto akimwazibu mpinzani wake Nassibu Ramadhani kwa kumtupia makonde mazito wakati wa Mpambano wao wa kugombania ubingwa wa WBF uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Miyeyusho alishinda kwa T.K.O ya raundi ya kumi picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Miyeyusho akionesha ufundi wake kwa kumtupia masumbwi Nassibu Ramadhani wakati wa Mpambano wao wa kugombania ubingwa wa WBF uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Miyeyusho alishinda kwa T.K.O ya raundi ya kumi picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara kulia akimvisha mkanda wa ubingwa wa WBF bondia Fransic Miyeyusho baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani  kwa T.K.O raundi ya kumi kushoto ni promota wa mpambano huo Mohamed Bawaziri www.superdboxingcoach.blogspot.com
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara kulia akimpongeza Bingwa wa ubingwa wa WBF bondia Fransic Miyeyusho baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani  kwa T.K.O raundi ya kumi kushoto ni promota wa mpambano huo Mohamed Bawaziri www.superdboxingcoach.blogspot.com
bondia Fransic Miyeyusho akiwa amebebwa juu akiwa na mikanda miwili alioshinda baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani picha nwww.superdboxingcoach.blogspot.coma
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila  'Super D' kushoto akiwa na wadau waliojitokeza kuangalia mpambano huo

MJUE MESSI TOKA UDOGONI MPAKA LEO ANAPOVUNJA REKODI KIBAO


Lionel Andres Messi anazidi kuishangaza dunia kwa uwezo wake mkubwa karika soka. Lionel Messi aliezaliwa miaka 25 huko Rosario , Argentina. Messi ni mtoto wa Mzee Jorge Horacio Messi ambae alikuwa mfanyakazi wa kiwanda cha Chuma na mama yake  Celia Maria Cuccitti. Kwa upande wa Baba yake Messi anaasili ya Italy tokea mji mmoja unaitwa Ancoma, ambako ilikuwa ni asili ya babu yake aitwae Angelo Messi aliehamia Argentina mwaka 1883. Messi ana kaka wawili na dada mmoja.

Katika umri wa miaka mitano Leo Messi alianza kucheza soka katika club ya Grandoli. Hii ilikuwa klabu ya mtaani kwao iliyokuwa inasimamiwa na Baba ake. Mwaka 1995 Messi alihamia katika klabu ya Newell's Old Boys iliyopo katika mji wake wa Rosario. 
Messi akiwa na miaka 11

Akiwa na miaka 11 Messi aligundulika kukosa hormone za ukuaji. Baada ya kugundulika na tatizo hilo, Klabu ya River Plate moja ya klabu kubwa sana nchini Argentina ilitaka kumchukua ila ikashindwa kutokana na gharama za matibabu yake. Dola $900 ilitakiwa kila mwezi kwa ajili ya gharama za matibabu ya mtoto Messi. Carles Rexach mkurugenzi wa michezo wa Barcelona alikifahamu kipaji cha Messi baada ya kumuona akiwa katika majaribio na Klabu ya Llieda.
Raxach alikubali kumpa Messi mkataba na Barcelona, akiwa hana karatasi yoyote mkononi alimwandikia mkataba wa kwanza Messi katika Leso.
Hatimaye Barcelona walikubali gharama za matibabu ya Messi kwa masharti kuwa ahamie Hispania. Bila kipingamizi Messi na Baba yake wote wakahamia Hispania na Lionel akaanza kuitumikia klabu ya Barcelona akiwa katika katika shule ya vipaji ya  klabu hiyo iliyo maarufu sana kama La Masia. 
Messi na Macarena 

Inasemekana Messi amewahi kuwa na uhusiano na mwanadada Macarena ambae naye anatokea katika mji wa Rosario.  Messi alitambulishwa kwa Rosario na baba yake Rosario kipindi aliporudi kuuguza majeraha yake kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia 2006. Messi pia alishawahi kuwa na uhusiano na mwanamitindo wa Argentina mwanadada Luciana Salazaar.
Januari 2009 katika mahojiano ya kipindi "Hat-Trick Barca'" cha Canal 33 Messi alisema anauhusiano na mwanamke mmoja hivi (hakumtaja jina) na anafuraha kuwa nae swali hilo lilikuja baada ya Messi kuonekana katika sehemu mbalimbali na mwanadada Antonella Roccuzzo. Juni mwaka 2012 Messi akicheza mechi dhidi ya Ecuador alifanikiwa kufunga goli, alishangilia Goli hilo kwakuweka mpira ndani ya jezi yake kuashiria kuwa mpenzi wake ni mjamzito. Siku kadhaa baadae ikaripotiwa na vyombo vya habari kuwa mpenzi wake ana ujauzito wa wiki 12 (miezi 3). Mnamo Tarehe 2 Novemba mwaka 2012 mtoto wa kwanza wa Messi alizaliwa na kupewa jina la Thiago.


Messi akishangilia bao dhidi ya Ecuador




Messi ana ndugu wawili ambao waacheza mpira. Maxi anaichezea klabu ya Club Olimpia nchini Paraguay na Emmanuel Biancucchi. Pamoja na kuishi Spain kwa muda mrefu ila Messi hajaacha kupakumbuka Rosario. KIla mara hutembelea mji huu na pia ana mawasiliano na marafiki na ndugu kadhaa wanaoishi katika mji huo. Inasemekana wakati mmoja Argentina ilipokuwa ikifanya mazoezi mjini Buenos Aires. Messi aliendesha mwendo wa masaa matatu baada ya mazoezi kwenda Rosario kula chakula cha jioni na kulala na kesho yake kugeuza mapema kabla ya mazoezi. Messi bado anamiliki nyumba yao ya zamani ambako alikuwa anaishi na familia yake japokuwa hakuna mwanafamilia anayeishi hapo siku hizi.

  

Mwaka 2007, Messi ameanzisha Charity Foundation kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji.
Messi alitangazwa kuwa balozi wakujitolea wa UNICEF katika maswala ya kupigania haki za watoto. Barcelona nao wako nyuma wanamsaidia messi katika hili kwakuwa Barcelona na Messi wana uhusiano mzuri.


Messi alianza kuichezea timu ya wakubwa ya Barcelona tarehe 16 Novemba mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 16 na siku 145 katika mchezo wa kirafiki kati ya Barcelona na F.C Porto ya Ureno.
Miezi michache baadae Frank Rijkaard kocha wa barcelona kipindi hicho alimpatia Messi nafasi ya kucheza ligi ya Spain dhidi ya RCD Espanyol akiwa na Umri wa miaka 17 na siku 114 hivo kumfanya Messi kuwa mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo kuichezea Barcelona na mdogo kabisa kuichezea Barcelona katika ligi. Rekodi ambayo baadae ilikuja kuvunjwa na Bojan Krikic. Goli la kwanza la Messi katika timu ya wakubwa alilifunga dhidi ya Albacete Balompie mwezi Mei mwaka 2005. September mwaka huohuo Messi alipata urai wa Spain.
Baada ya hapo amekuwa akicheza kwa mafanikio makubwa. Messi katika kipindi hichi chote toka alipoanza kuichezea Barcelona amepata mafanikio mengi. Mafanikio Binafsi kama mchezaji na Mafanikio ya timu pia. 

Messi ameweza kuvunja rekodi nyingi ambazo ziliwekwa na magwiji wa soka wa zamani. Tukianzia katika klabu yake Messi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji anaeongoza kwa kufunga mabao mengi katika historia ya klabu hiyo akiwa na magoli 283 na pia ni mchezaji alieifungia Barcelona mabao mengi katika ligi ya Hispania uku akiwa na mabao 192. Messi anashikilia rekodi ya klabu yakufunga Mabao mengi kwenye msimu mmoja akiwa amefunga magoli 73 katika msimu wa 2011-2012. Messi anashikilia rekodi ya Barcelona ya mchezaji aliefunga magoli mengi katika mashindano ya ulaya akiwa na magoli 57 na 56 katika ligi ya mabingwa ulaya. Messi anaongoza listi ya mchezaji aliefunga magoli mengi katika Spanish Super Cup akiwa na magoli 10.
 
Messi ana rekodi ya kuwa mchezaji alieifunga magoli mengi kwa msimu mmoja katika michuano ya mabingwa ulaya akiwa na magoli 14, Messi huyuhuyu ana rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo mmoja wa ligi ya mabingwa ulaya akiwa amefunga 5 katika mechi dhidi ya Bayern Leverkusen msimu wa 2011-2012. Messi ana rekodi pia yakufunga hat-tricks nyingi ndani ya msimu mmoja akiwa amefunga hat-trick mara 8 msimu wa 2011-2012. Na bila kusahau Messi anashikilia rekodi ya Barcelona ya kufunga magoli mengi katika ile michuano ya klabu bingwa ya dunia akiwa na magoli 4.


Kwa ujumla Messi anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliefunga magoli mengi katika msimu mmoja wa ligi ya hispania akiwa amefunga magoli 50 katika msimu mmoja. anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika msimu mmoja wa ligi ya mabingwa huko akiwa a magoli 14 na pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliefunga magoli mengi ndani ya msimu mmoja akiwa na magoli 73 katika mashindano yote. Messi hajaishia hapo, Jana tarehe 09-Dec-2012 Messi amevinja rekodi ya mkongwe Gerd Muller ya mabao 85 katika mwaka mmoja ambayo ilidumu kwa miaka 40. Messi amefunga goli la 85 na 86 jana akiisaidia Barcelona kushinda mchezo wake dhidi Real Betis. Messi ameweka rekodi hiyo mpya uku akiwa na michezo mitatu mpaka mwisho wa mwaka. 


Messi bado ana rekodi zake binafsi. Messi ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka kwa miaka 3 mfululizo (209,2010,2011) na mwaka huu yuko katika ile tatu bora. Messi anashikilia tuzo ya mfungaji bora wa bara la Ulaya ya mwaka 2010 na mwaka 2012. Mshambuliaji bora wa ligi ya Hispania mwaka 2009,2010,2011,2012. Mchezaji bora wa ligi ya hispania mwaka 209,2010,2011,2012.  Mfungaji bora ligi ya Mabingwa ulaya mwaka 2009,2010,2011 na 2012. Man of the match fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 2011.
SOURCE:http://valetyno.blogspot.ca/

Sunday, December 9, 2012

Stars yarejea, macho yote kwa Zambia sasa

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’ Kim Poulsen akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana pamoja na timu wakitokea nchini Uganda kushiriki michuano ya Cecafa Challenge iliyomalizika juzi. Kilimanjaro Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager. (Picha na Mpigapicha wetu).
Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars ‘ wakiwasili  jana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Uganda kushiriki michuano ya Cecafa Challenge iliyomalizika juzi. Kilimanjaro Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager. (Picha na Mpigapicha wetu).
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars ‘ wakiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  jana mara baada ya kuwasili wakitokea nchini Uganda kushiriki michuano ya Cecafa Challenge iliyomalizika juzi. Kilimanjaro Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager. (Picha na Mpigapicha wetu).




Na mwandhishi wetu
Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars iliyoshiriki katika mashindano ya Cecafa Challenge yaliyomalizika Jijini Kampala Jumamosi, imerejea Jijini Dar es Salaam huku sasa ikitizamia kukutana na Chipolopolo ya Zamzbia Disemba 23.
Stars, ambayo inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ilirejea jana jioni kwa ndege ya Precision Air.
Kikosi hicho chenye wachezaji 18, kilifanikiwa kutinga nafasi ya nne katika mashindano hayo baada ya kufungwa za Zanzibar Heros kwa penalty 6-5 na kutinga nafasi ya tatu.
Katika mashindano hayo, The Cranes ya Uganda ilifanikiwa kutetea taji na kubakiza kombe nyumbani. Hii nimara ya 13 kwa Uganda kutwaa taji hilo.
Akizungumza baada ya kurejea, Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen alisema mashindano haya yalikuwa muhimu sana kwa timu yake kwani vijana wamepata uzoefu baada ya kukutana na timu ngumu na zenye uzoefu.
“Mashindano yalikuwa mazuri…tulienda na nia ya kurudi na kombe lakini hatujafanya jivyo ila muhimu ni kwamba mashindano haya yametupa uzoefu mkubwa ili tuweze kujiandaa na mashindano mengine ambayo yako mbele yetu,” alisema.
“Tumefarajika kucheza na timu kubwa kama The Cranes ambayo ndio timu bora katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati,” alisema.
Alisema sasa hivi macho ya wachezaji yote yako katika mchezo ujao wa kirafiki dhidi ya Chipolopolo ya Zambia kwani ni mechi ambayo itakuwa kipimo kikubwa kwa Stars kwa hivyo inahitaji maandalizi makubwa sana.
“Nawaomba watanzania wasikate tama kwa kuwa tunaijenga timu hawa ni vijana na ninaamini siku zijazo watafanya vizuri zaidi,” alisema Poulsen.
Kocha Kim Poulsen anatarajiwa kutangaza kikosi cha Stars kesho Jumatatu na amesema atawaita wachezaji wa Zanzibar pia ambao walicheza vizuri Kampala.
“Niliwaona wakicheza kwa hivyo bila shaka waliofanya vizuri watakuwemo kwenye kikosi hiki,” alisema.

EXCLUSIVE: NIYONZIMA AONGEZA MKATABA WA MIAKA 2 YANGA KWA DOLA 70,000 NA MSHAHARA WA DOLA 3,000

Zikiwa zimepita siku kadhaa za mazungumzo juu ya kuongezwa kwa muda wa mkataba kiungo mshambuliaji wa Dar Young African - Haruna Niyonzima, hatimaye siku ya jana klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati imefanikiwa kukubaliana kimsingi na mchezaji huyo kumuongezea mkataba mpya.

Taarifa rasmi nilizozipata ni kwamba Haruna Niyonzima ambaye amebakiza miezi sita katika mkataba wake na Yanga amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga.

"Niyonzima alikuja Tanzania siku tatu zilizopita kwa ajili ya mazungumzo na uongozi wa Yanga, lakini mwanzoni hawakupata muafaka, ila hatimaye jana alikubaliana na Yanga kuongeza mkataba wa miaka miwili kwa kulipwa dola 70,000 kama fedha ya usajili na mshahara wa dola 3,000 kwa mwezi," kilisema chanzo cha habari kilicho karibu na uongozi wa Yanga.

YEW BERKO AENDA KUJIUNGA NA FC LUPOPO LEO ASUBUHI

Hatimaye leo majira ya saa moja asubuhi golikipa Mghana Yew Berko ameenda nchini Kongo kwenda kujiunga na timu ya FC Lupopo kwa mkopo akitokea Dar Young African.

Berko ambaye alijiunga na Yanga takribani misimu mitatu iliyopita amepelekwa Lupopo baada ya kukosa nafasi ya kudumu ndani ya kikosi cha Yanga mbele ya golikipa Ally Mustapha Barthez. Hivyo ikaamuriwa bora aende kwa mkopo Lupopo ambao walikuwa wakimhitaji kwa muda mrefu na nafasi yake imechukuliwa na Kabange Twite ambaye ni kaka yake na Mbuyu Twite wa Yanga.

"Ni kweli leo asubuhi Yew Berko ameondoka kwenda Congo kujiunga na FC Lupopo, ameondoka hapa kwa ndege ya shirika la Kenya Airways." kilisema chanzo cha habari kutoka Yanga.

MANNY PACQUIAO AGONGWA KWA KNOCKOUT NA MARQUEZ


Knockout blow: Marquez celebrates after stopping Pacquiao in the sixth round


Knockout blow: Marquez celebrates after stopping Pacquiao in the sixth round
Mshindi Marquez

Stunning shot: Marquez lands the bout-winning right hand in the sixth


Knockout blow: Marquez lands the bout-winning right hand in the sixth
Ngumi kali ya kushtukiza iliyompeleka Pacquiao chini
Knockout blow: Marquez lands the bout-winning right hand in the sixth

Knockout blow: Marquez lands the bout-winning right hand in the sixth

Knockout blow: Marquez lands the bout-winning right hand in the sixth


The PacMan: Pacquiao makes his way out to the ring
Pamoja na kupigwa Pacquiao alitoka uwanjani akiwa hana majeraha makubwa

The PacMan: Pacquiao makes his way out to the ring


Sighter: Pacquiao lands a left in the first round


 
 
Smiles better: Former Republican presidential candidate Mitt Romney (right) was in the crowd
Aliyekuwa mgombea wa uraisi wa Marekani Mitt Romney alikuwepo kucheki pambano
On the charge: Marquez takes the attack to Pacquiao
Marquez akimfunza adabu Pacquiao
Floored: Pacquiao hits the canvas after Marquez connects with a right in the third



Floored: Pacquiao hits the canvas after Marquez connects with a right in the third

Floored: Pacquiao hits the canvas after Marquez connects with a right in the third
Mtu mzima Pacquiao Chaliiiiiiiiiiiiiiiiiii
Toe-to-toe: Both fighters were intent on attacking

 
 
Toe-to-toe: Both fighters were intent on attacking
Old acquaintances: The pair were meeting for the fourth time in their careers
Wawili hawa wamekutana mara nne katika maisha yao ya ndondi
Old acquaintances: The pair were meeting for the fourth time in their careers
False dawn: Marquez had a wobble in the fifth after a left jab from Pacquiao


 
Floored: Pacquiao was face down on the canvas for some time
Pacquiao chaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Floored: Pacquiao was face down on the canvas for some time
 
Job done: Marquez celebrates his victory


UGANDA MABINGWA TENA WA CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP 2012!