Search This Blog

Monday, July 2, 2012

MANCHESTER UNITED FANS MABINGWA WA SERENGETI FIESTA BONANZA MBEYA

Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Jonathan Maselea akikabidhi zawadi ya kreti la bia kwa nahodha wa timu ya mashabiki wa Manchester United ya Uingereza mara baada ya timu hiyo kuibuka washindi wa shindano la Serengeti Fiesta  Fiesta Soccer Bonanza lililofanyika kwenye viwanja vya chuo cha Uhasibu jijini Mbeya TIA, ambapo washindi hao wameondoka pia na shilingi laki 500.000, huku mshindi wa pili timu ya Barcelona wameibuka na shilingi laki 300,000.
Meneja Msoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Kanda ya Kusini Jonathan Maselle akimsikiliza Mkuu wa mauzo kanda ya kusini na Nchi Jirani Freddy Richard akizungumza mara baada ya timu hizo kukabidhiwa zawadi zao.
Mratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza Shafii Dauda akizungumza mara bada ya kumalizika kwa bonanza hilo kutoka kulia ni Jonathan Maselle Meneja masoko wa Serengeti Kanda ya nyanda za juu Kusini, Mkuu wa Mauzo kanda ya kusini na nchi njirani Freddy Richard na kutoka kulia ni kapteni wa timu ya mashabiki wa Machester United Willy Maisara na Kapteni wa timu ya Barcelona Zefania Bitwale
Mmoja wa wachezaji wa mashabiki wa timu ya Manchester United akiwa amebebwa juujuu na mashabiki wake mara baada ya timu yao kuibuka mabingwa wa tamasha la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza mkoani Mbeya.
Wadau wa mkoani Mbeya wakishoo love mbele ya kamera ya Fullshangwe.
Kutoka kulia ni Mkuu wa mauzo Kanda ya Kusini na nchi Jirani wa kampuni ya bia ya Serengeti Freddy Richaer, Alex Lwambano kutoka Clouds, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi tamasha la Serengeti Fiesta Sebastian Maganga, Mtangazaji wa Clouds Antu Mandoza na Mratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza Bw. Shafii Dauda wakishoo Love/
Wachezaji wa timu ya mashabiki wa Manchester United na Barcelona wakichuana vikali katika mchezo wa fainali ya bonanza hilo.
Mchezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Manchester United akiukokota mpira wakati wa mchezo wa fainali dhidi ya timu ya mashabiki wa Barcelona kwenye viwanja vya TIA jijini Mbeya leo.
Mashabiki wa Manchester United wakishangilia kwa nguvu mara baada ya timu ya kutinga fainali ya bonanza hilo.
kutoka kulia ni Freddy Richard wa SBL Mbeya, Alex Lwambano, Sebastian Maganga na Jonathan Maselle SBL Mbeya wakifuatilia jambo katika tamasha hilo.
Mashabiki wa tamasha la serengeti Fiesta Soccer Bonanza wakifuatilia matukio mbalimbali katika tamasha hilo.
Akiana Meku wanapokutana ni kupanga dili ya hela tu hebu wacheki akina Meku hawa wanapanga dili za hela au wanafurahia maisha.
Mashabiki wa Bonaza hilo wakiwa wamefurika katika viwanja vya TIA jijini Mbeya.
Mtangazaji wa Clouds na mratibu wa tamasha la serengeti Fiesta Soccer Bonanza akimhoji mmoja wa mashabiki wa timu ya Iner Milan ya Italia mabayo mwaka huu haikushiriki katika bonanza hilo.
mashabiki wakifuatilia kwa makini matukio mbali mbali katika tamasha hilo.
Mashabiki wa Manchester United wakishangilia kwa nguvu wakati timu yao ilipotinga katikahatua ya Nusu Fainali ya Bonanza hilo.

PHOTO CREDITS: Fullshangwe.blogspot.com

Sunday, July 1, 2012

SPAIN VS ITALY EURO 2012 FINAL: WATU MILLIONI 250 KUANGALIA, TIKETI MOJA INAUZWA NI HATARI - NI BALOTELLI AU TORRES NANI KUONGEZA TAJI USIKU WA LEO - YAJUE MAMBO MUHIMU KUHUSU FAINALI HII

1: Hii ndio fainali ya kwanza yaEuro ambayo magolikipa wote watakuwa manahodha.

2: Ikiwa Spain wakishinda leo, Vicente Del Bosque atakuwa kocha wa kwanza wa timu ya taifa kushinda kombe la dunia na kombe la ulaya. Helmut Schon aliongoza Ujerumani Magharibi kushinda Euro 1972 na kufuatia na kombe la dunia 1974.

6: Goli la haraka zaidi kufungwa kwenye fainali ya Euro liliwekwa kimiani na mchezaji wa Spain Jesus Pereda dakika ya sita ya mchezo wa fainali.

7: Wachezaji saba tu kutoka nje ya ligi ya Spain na Italy ndio wapo kwenye vikosi vya timu hizi mbili.

7: Kutakuwa na redio saba za kihspaniola zitakazotangaza mchezo wa leo, nyingi kuliko nchi yoyote dunaini.

10: Mreno Pedro Proenca ndio atakuwa mwamuzi wa fainali ya leo jumapili na ameshatoa kadi 10 za njano, huku akiwa hajaigusa kadi nyekundu kwenye michuano hii.

15: Italy wameshapata kadi za njano 15 kwenye Euro 2012, nyingi kuliko timu yoyote kwenye michuano hii.

17: Alvaro Arbeloa ndio mchezaji aliyecheza faulo nyingi kuliko wote kwenye mashindano, akicheza faulo mara 17.

27: Huu ndio wastani wa umri wa kikosi cha Spain.

28: Huu ndio wastani wa umri wa kikosi cha Italia - miaka 28.

31: Kutakuwepo na camera 31 zitakazokuwa zikinasa picha za matukio ya mchezo wa leo kwenye uwanja wa Olympic.

55: Italy wamepiga mashuti 55 kwenye lango - mengi kuliko timu yoyote kwenye Euro 2012.

92.8: Kiwango cha pasi zilizofika cha Xavi ni asilimia 92.8, kiwango kikubwa kuliko mchezaji yoyote kwenye mashindano haya na mchezaji yoyote kwenye fainali ya leo.

120: Gianluigi Buffon atacheza mechi yake ya 120 kwa Italy - ikiwa atapangwa kwenye fainali ya leo.

137: Buffon bado hajamfikia mpinzani wake kwenye fainali ya leo Iker Casillas ambaye amecheza mechi 137 akiwa na La Roja.

164: Mshambuliaji wa Italy Sebastian Giovinco ndio mchezaji mfupi zaidi kwenye Euro 2012 - akiwa na sentimita 164.

180: Huu ndio uwiano wa urefu wa wachezaji wa Spain

181: Huu ndio uwiano wa urefu wa wachezaji wa Italia.

200: Fainali hii itaonyeshwa kwenye zaidi ya nchi 200 duniani.

455: Xavi pekee amepiga pasi zilizofika 455 - nyingi kuliko mchezaji yoyte kwenye Euro 2012.

2000: Adidas wametoa mipira 2000 kwa ajili ya mechi za michuano hii.

3, 568: Gharama ya tiketi ya bei ya katikati kwa ajili ya mchezo wa fainali ni €3468

40,000: Kiungo wa Italia Andrea Pirlo anamiliki kampuni ya kutengeneza wine, Pratum Coller, ambayo inauza zaidi ya chupa 40000 kwa mwaka.

68,055: Kutakuwa na watu 68055 ndani ya uwanja wa Olympic mjini Kiev kwa ajili ya kuangalia fainali ya leo.

582,810: Wachezaji wote wa Spain wamekimbia mita zipatazo 582,810 kwenye Euro 2012.

605,020: Wachezaji wote wa Italy wamekimbia mita zipatazo 582,810 kwenye Euro 2012.

1,000,000: Zaidi ya watu million moja wamenunua jezi ya juu ya Spain zilizotengenezwa na adidas kwa ajili ya Euro 2012.

1, 000,000 - Kampuni ya vinywaji ya Carlsberg inategemea kuuza vikombe millioni moja vya bia kwenye dakika 15 za mapumziko kwenye uwanja wa Olympic na maeneo mengine yaliyotengwa maalum kwa ajili kuangalizia mpira wa mechi ya fainali mjini Kiev.

1, 320,000 - Idadi yote ya mashabiki ambao wameingia viwanjani kuangalia Euro 2012 imefika watu millioni 1.32.

250,000,000 - Watu millioni 250 wanategemewa kuangalia mechi ya fainali ya leo duniani  kote.

IKER 'SAINT' CASILLAS VS GIANLUIGI BUFFON: NANI KIPA BORA ZAIDI KWENYE HISTORIA YA SOKA - MAJIBU LEO USIKU

HIZI NDIO REKODI ZAO KWENYE SOKA MPAKA SASA - NANI KUFUNIKA USIKU WA LEO

IKER CASILLAS
GIANLUIGI BUFFON


20 May 1981 KUZALIWA
28 January 1978
Goalkeeper NAFASI Goalkeeper
622 MECHI ZA KWENYE KLABU 621
136 MECHI ZA KIMATAIFA 119
5 MAKOMBE YA LIGI 5*
1 cup, 3 supercups DOMESTIC CUPS 1 cup, 3 supercups
2 Champions League, 1 Uefa Supercup, 1 Intercontinental Cup MAKOMBE YA BARA LA ULAYA 1 Uefa Cup
1 World Cup,
1 European Championship
MAKOMBE YA KIMATAIFA 1 World Cup
http://u.goal.com/135700/135791.jpg
http://u.goal.com/135700/135791.jpg

SERENGETI FIESTA BONANZA YAANZA KUTIMUA VUMBI HAPA MBEYA

Wachezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Manchester City ya Uingereza wakichuana vikali na mchezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Real Madrid huku wakati wa tamasha la mashabiki wa vilabu vya Ulaya linalojulikana kama Serengeti Fiesta Soccer Bonanza, ambalo linafanyika jijini Mbeya katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu (TIA) na kushirikisha timu za mashabiki wa vilabu vya Manchester United, LiverPool, Bayern Munichen, Asernal, Manchester City Barcelona, Chealsea na Real Madrid, Mshindi katika bonaza hilo atajishindia shilingi 500,000.
Wachezaji wa timu ya mashabiki wa Barcelona wakichuana vikali na wachezaji wa timu ya mashabiki wa Chealsea katika bonanza hili timu hizo ndiyo zilizofungua dimba.
Mratibu wa Serengeti Fiesta Soccer Bonanza Shafii Dauda akitoa maelekeza kwa timu za mashabiki wa Chealsea na Barcelona kabla ya kuanza kwa mtanange wao.
Timu ya mashabiki wa Manchester Unitedi wakishangilia wakati wimbo wao ulipokuwa ukipigwa.
Timu ya Mashabiki wa Chealsea nao wakiimba wimbo wao kabla ya kuanza kwa bonanza hilo.
Timu ya mashabiki wa Arsenal wakiimba wimbo wao huku wakishagilia.
Nao Barcelona hawakuwa nyuma wakirukaruka kwa furaha mara baada ya kupigiwa wimbo wao.
Hawa ni Real Madrid kama unavyowaona katika picha wakishangilia na kucheza wakati wimbo wao ukipigwa.
LiverPoool wakishangilia kwa nguvu wimbo wao.
Mwamuzi wa mchezo huo akitoa maelekezo kwa timu za Chealsea na Barcelona kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Timu zote zikiwa zimejipanga tayari kwa kupigiwa nyimbo zao kabla ya kuanza kwa bonanza hilo kwenye viwanja vya TIA Mbeya.
Peter Kabaisa mmoja wa wafanyakazi akigawa jezi za kuchezea kwa makapteni wa timu hizo.
Mshauri nasaha wa masuala ya ukimwi Flora George  akitoa elimu kwa maadhi ya mashabiki waliofika katika banda la KIHUMBE
Mmoja wa watangazaji wa Clouds mwenye maneno mengi na vituko Mbwiga wa Mbwiguke ambaye ni shabiki wa timu ya Liverpool akitoa tambo zake kwa vituko na kuvuta mashabiki wengi kumsikiliza katika bonanza hilo.
Timu ya Bayern Munichen ikishagilia kwa nguvu kufurahia wimbo wao katika bonanza hilo.
PHOTO CREDITS: fullshangwe.blogspot.com

SERENGETI DANCE LA FIESTA ILIVYOFANA LEO ARUSHA - KESHO SOKA BONANZA MBEYA


Mmoja wa majaji wa shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012 lililofanyika kwenye Club ya Mawingu jioni ya leo,jijini Arusha ,Hamis Mandi a.k.a B Dozen kutoka kipindi cha XXL kinachorushwa na redio ya Clouds FM,akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa kundi shindi la shindano hilo liitwalo Contagious Crew







Mwendesha shindano hilo pichani kati,Nikson akisoma majina ya makundi mawili yaliyoingia fainali na hatimae kulipata kundi moja mahiri kabisa na kundi la Contigious Crew limeibuka mshindi na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja taslim na kreti moja ya bia ya Serengeti,ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2012.



Pichani majaji wa shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012 wakijadiliana jambo wakati wa mchuano mkali wa shindano hilo lililokutanisha makundi manne,ambayo ni Tp Jackson,New Kings,B-Boy Dance pamoja na kundi la Contigious Crew.Kulia ni Jaji Msami kutoka THT na shoto ni Mtangazaji kutoka Clouds TV,Issa Kwisa







Sehemu ya washabiki wa Serengeti Dance la Fiesta 2012 wakivutiwa zaidi na shindano hilo lilipokuwa likiendelea ukumbini humo.


Kila kundi lilionesha umahiri wake wa kucheza,huku kwa aliyeonekana kufanya vyema shangwe na miluzi ilitawala kila kona.

Palikuwa hapatoshi jioni ya leo ndani ya Club ya Mawingu wakati wa shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012 likifanyika,ambapo kila kundi lilionesha umahiri wake wa kuyarudi mangoma kwa staili ya kipekee kabisa.Pichani mcheza shoo wa kundi la B-Boy Dance akionesha umahiri wake wa kucheza.

Vijana mbalimbali waliojitokeza kwa wingi kwenye shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012,ambapo mshindi alifanikiwa kuibuka na kitita cha shilingi milioni moja na kreti moja la bia mshindi wa pili aliibuka na kreti la bia ya serengeti,ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kwa mwaka huu.
 

YANGA WALIVYOISAMBARATISHA EXPRESS YA UGANDA KWENYE PICHA














Mechi kati ya Yanga na Express ya Uganda, imemalizika wenyeji wameshinda 2-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabao yote yakitiwa kimiani na Jerry Tegete dakika ya nne na 20, wakati la mabingwa wa Uganda, beki Ladislaus Mbogo alijifunga katika harakati za kuokoa mpira wa Kiiza Ayoub dakika ya 77. Kipindi cha kwanza Yanga ilitawala mchezo kwa asilimia 60, Express walipiga krosi mbili na shuti moja ambalo halikulenga lango, lakini kipindi cha pili Express walitawala na dakika 20 za mwisho Yanga walikuwa wanaomba mpira usihe. 
Kikosi kilichoanza Yanga, kutoka kulia waliosimama Ally Mustafa 'Barthez', Athumani Iddi 'Chuji', Said Bahanuzi, Oscar Joshua, Jerry Tegete na Nizar Khalfan. Walioinama kutoka kulia ni Kelvin Yondan, Nadir Cannavaro, Juma Abdul, Frank Damayo na Simon Msuva. 
Benchi
Nizar akimpongeza Tegete baada ya kufunga la pili
Vijana wanaingia uwanjani
Wenye timu yao   

PHOTO CREDITS: bongostaz.blogspot.com