Search This Blog

Monday, June 18, 2012

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA MSUMBIJI WALIPOITOA TAIFA STARS

Umati wa mashabiki wa Msumbiji wakiwa uwanjani kuisapoti timu yao

Haruna Moshi Boban , Mrisho Ngassa, Nurdin Bakary na wachezaji wengine wa Tanzania wakiwa kwenye benchi.


Shoamri Kapombe akipambana dimbani kumtoka beki wa Msumbiji

Frank Domayo na Shomari Kapombe wakipata maelekezo kutoka kwa kocha Kim Poulsen


Baadhi ya mashabiki wa kitanzania wakiisapoti timu kwenye mchezo wa jana

Mrisho Khalfan Ngassa akiwapeleka puta mabeki wa Msumbiji

Mbwana Samatta akijaribu kumtoka beki wa Msumbiji


MAXIMO ALONGA KUHUSU YANGA



* Akiri pia kupata ofa nono Ethiopia na Rwanda
* Yanga wasisitiza atawasili badaye mwezi huu



ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Mbrazil Marcio Maximo akiri kuwa ni kweli yupo katika mazungumzo na klabu ya Yanga ila bado hawajakubaliana siku ya kuja na si rahisi kama wanavyodhani.

Maximo kwa sasa anafundisha kwa mafanikio makubwa klabu ya Democrata F.C ya Mjini Rio de Jeneiro Brazil.

Maximo aliondoka nchini baada ya mkataba wake kumalizika Agosti mwaka 2009 ambapo Shirikisho la soka nchini TFF lilishindwa kumuongezea mkataba kwa kutoridhishwa na utendaji wake na nafasi yake kuchukuliwa na Mdenmark Jan Poulsen ambae pia alishindwa kuitoa Tanzania kimasomaso.

Akizungumza na Dimba kwa njia ya mtandao Maximo alisema bado yupo katika mkataba na klabu yake hivyo si rahisi yeye kukurupuka na kuondoka ni lazima afuate mkataba unavyosema.

“Ni kweli nipo katika mawasiliano na Yanga lakini tupo katika mazungumzo kwani nina mkataba na klabu ya Democrata si rahisi mimi kuja huko kwa sasa bila kufuata taratibu, hata hivyo hadi sasa hatujapanga na Yanga tarehe ya kuja huko, nashangaa kusikia kuwa watu wanasubiria kuwasili kwangu.

“Mimi naheshimu sana mkataba na kama kuja ni lazima nifuate taratibu kwanza na si kukurupuka, si rahisi labda wasiwe wanajua nini maana ya mkataba, sijapangiwa na wala tiketi sina kwa kuwa hatujafikia huko,” alisema Maximo.

Maximo alieleza kuwa amefurahishwa na nia ya Yanga kumtaka na kama wataafikiana basi hana budi kuja kujiunga nao kwa ajili ya kuifundisha timu.

Alisema anaifatilia kwa makini ishu ya Yanga kwasababu anaona wakurugenzi wa Yanga wana nia thabiti ya kuendeleza klabu hiyo hivyo hataki kuwaangusha.

Kocha huyo ambae alileta hamasa kwa timu ya Taifa na kuifanya ipendwe na iwe gumzo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, amepata mawasiliano mengine toka kwa timu ya St. George ya Ethiopia na timu za Taifa za Zimbabwe na Rwanda ambayo ipo chini ya kocha Milutin Sredojevic ‘Micho’

Hata hvyo klabu ya Yanga jana ilijulisha umma kuwa Maximo alietarajiwa kufika jana sasa atawasili nchini mwishoni mwa wiki hii kitu ambacho Maximo hakijui.

Katika taarifa ya Yanga jana, ilieleza kuwa Maximo tayari amekwishatumiwa tiketi ya safari ya kuja hapa nchini na ameshindwa kuwasili jana kutokana na Klabu yake anayofundisha ya Democrata kukabiliwa na mchezo mgumu siku ya Jumamosi wiki hii kitu ambacho hakina ukweli.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Marcio mara baada ya kuwasili nchini atafanya mazungumzo na Uongozi wa Klabu ya Yanga ikiwemo kusaini Mkataba na Klabu ya Yanga kabla ya kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho.

Kocha huyo kabla ya kuondoka nchini Brazil amewaahidi Wanachama na Wapenzi wa Klabu ya Yanga kuwa atafanya jitihada za kukiimarisha kikosi cha Mabingwa wa Soka wa Afrika Mashariki na Kati katika kuinua vipaji mbalimbali kupitia soka la Vijana wenye umri mdogo kwa ajili ya kupata wachezaji Bora.
Ilieleza ambo mengine aliyoyapanga Kocha huyo ni pamoja na  kuimarisha nidhamu kwa Wachezaji atakaokuwa akiwafundisha na mara baada ya kuanza kibarua chake cha kukinoa kikosi hicho atakuwa na mtihani wa kwanza kwa kukabiliwa na michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Julai 23 hadi Agosti 7 Mwaka huu.

Stori hii imeandaliwa na Mwani Nyangasa.

SD TV: PENALTI ZILIZOITOA TANZANIA DHIDI YA MSUMBIJI

SD TV: MABAO TAIFA STARS VS MSUMBIJI.

USAHILI WA EPIQ BONGO STAR SEARCH WAMALIZIKA MKOANI DODOMA.

 
Kundi la akina dada wakitabasamu na kupiga pozi kabla ya kuingia kwa majaji


 Awaichi Mawalla wa Zantel akichangia damu akiwa na mtu wa damu salama
 Kundi la washiriki wa EBSS wakipiga pozi kabla ya kwenda kuonana na majaji
 Mshiriki wa EBSS akiimba na kupiga guitar kwa nguvu zake zote ili majaji wamkubali na apate fursa ya kuwakilisha Dodoma
Mshiriki wa EBSS akiimba kwa nguvu ake zote ili majaji wamkubali

KIFUKWE NA MANJI SI WADHAMINI HALALI WA YANGA!

Mwananchama wa Yanga bwana Abeid.A. Abeid ameibuka na kuwekea pingamizi uchaguzi wa klabu ya Yanga kwa kile anachodai katiba iliyotumiwa na wagombea si halali.
Bwana Abeid amabye aliwahi kuwa mweka hazina wa Yanga siku za nyuma pia amedai ndugu Yusuf Manji na ndugu Francis Kifukwe si wadhamini halali wa Yanga.

RONALDO AWANYAMAZISHA WABAYA WAKE: APIGA MBILI URENO IKIENDELEZA UBABE KWA WAHOLANZI NA KUWATOA EURO


Portugal 2-1 Holland (Euro 2012 - Group B) All... by fasthighlights-2012

UJERUMANI KUWAVAA UGIRIKI WASIOTABIRIKA KWENYE ROBO FAINALI YA EURO


Denmark 1-2 Germany (Euro 2012 - Group B) by fasthighlights-2012

Sunday, June 17, 2012

Taifa Stars yatolewa kwa penalti

Taifa Stars imetolewa kwenye mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa kwa penalti na wenyeji Msumbiji (The Mambas) katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa ulioko Zimpeto pembeni kidogo ya Jiji la Maputo.

Refa Bennett Daniel alipopuliza filimbi ya kumaliza dakika 90 za pambano hilo timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, hivyo kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mikwaju ya penalti ikatumika kupata mshindi.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu timu hizo
zilitoka sare ya bao 1-1.

Msumbiji ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 9 lililofungwa na mshambuliaji Jeremias Sitoe akiungnisha krosi ya Elias Pelembe ambaye mabeki wa Taifa Stars walifikiri ameotea.

Stars ilisawazisha bao hilo dakika ya 89 likifungwa kwa kichwa na
Aggrey Morris kutokana na mpira wa kona uliopigwa Amir Maftah.

Mikwaju ya penalti tano tano walioifungia Stars walikuwa Amir Maftah, Shabani Nditi na Shomari Kapombe wakati Aggrey Morris na Kevin Yondani walikosa.

Kwa vile The Mambas nao walikosa mbili ikabidi iongezwe penalti moja moja. Waliofunga kwa upande wa Stars walikuwa John Bocco, Frank Domayo na Mrisho Ngassa wakati Mbwana Samata alikosa.

Akizungumzia pambano hilo, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen aliwapongeza wachezaji wake kwa kupambana hadi dakika ya mwisho.

"Tulikuja Maputo tukijua kuwa tunatakiwa kufunga bao, tumeweza kufunga bao ingawa katika dakika za mwisho. Unajua linapokuwa suala la penalti chochote kinaweza kutokea, na ndivyo ilivyokuwa," alisema Kim.

Taifa Stars itarejea nyumbani Juni 19 mwaka huu, ambapo itaaondoka hapa saa 4.40 asubuhi kwa kupitia Nairobi, Kenya na kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.50 usiku.

Kikosi kilipngwa hivi; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/John Bocco, Aggrey Morris, Kevin Yondani, Shaabani Nditi, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Thomas Ulimwengu/Haruna Moshi, Mbwana Samata na Mwinyi Kazimoto/Amir Maftah.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MHARIRI GAZETI LA BINGWA AFARIKI DUNIA


Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (kushoto)
akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu Jamhuri ya Uturuki (Idara ya Habari na Maelezo),
Murat Karakaya iliyotolewa kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu
Uturuki, Bulent Arinc aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa nchi
hiyo, Recep Tayyip Erdogan, baada ya kuwasilisha mada katika
mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki
kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita
dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki
iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu,
ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau
wengine kutoka nchi 54 za Afrika.


MHARIRI wa Jamboleo, Willy Edward Ogunde amefariki dunia mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo (saa 6.30) usiku.

Taarifa ya Neville Meena, Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, imesema kwamba Willy aliyewahi kuwa Mhariri wa gazeti la BINGWA, pamoja na wahariri wengine walikuwa mjini Morogoro ambako walikwenda kuhudhuria mkutano wa masuala ya sensa iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Mara baada ya semina hiyo alikwenda kuwaona watoto wake na alikuwa huko hadi saa sita usiku alipomwita dereva wa pikipiki afike kumchukua kwa lengo la kurejea katika hoteli alikokuwa amefikia. Baada ya kutoka nje, na hatua sita hivi kabla ya kufika pikipiki ilipokuwa, alianguka.
Ndugu zake walimkimbiza hosipitali lakini walipofika na daktari kumpima, tayari alikuwa “amenyamaza” yaani amefariki dunia. Taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es Salaam zinafanywa.
Tutamkumbuka daima kwa upole na unyeyekevu wake. Kweli Willy ametuacha, ni pigo kwa taaluma yetu, ni pogo katika Jukwaa la Wahariri. Poleni kwa familia ya Willy Edward Ogunde, pole kwa wahariri wote na pole kwa tasnia nzima ya habari.  Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

MSUMBIJI YAIFUNGA TAIFA STARS KWA MIKWAJU YA PENALTI.

Timu ya taifa ya Msumbiji imefanikiwa kuitoa timu ya taifa ya Tanzania kwa mikwaju ya penalti kwenye kinyang'anyiro cha kusaka tiketi ya kufuzu AFCON 2012.
Mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kufungana bao 1:1.

Habari kamili itafuata....................

HISTORIA INAWAHUKUMU UHOLANZI DHID YA URENO: AKINA VAN PERSIE HAWAJAFUNGA AKINA ONALDO NDANI YA MIAKA 10 ILIYOPITA.

Uholanzi inabidi washinde mechi yao dhidi ya Ureno kwa goli 2-0 au zaidi, na kuombea Ujerumani wawafunge Denmark ili kuweza kuendelea kwenye robo fainali, lakini historia inawahukumu wadachi dhidi ya Wareno.

Matokeo ya nyuma yanaonyesha Ureno wana nafasi kubwa kupata matokeo chanya na kuwafunga vijana wa Bert van Marwijk katika mchezo muhimu wa mwisho wa kundi B leo jumapili.

Tofauti na wanapokutana na wababe wao Wajerumani ambao wamekuwa wakionea sana Ureno katika mechi 16 za mwisho zilizowakutanisha timu hizo, Ureno wamefanikiwa kushinda mechi 3, Ureno nayo imekua ikiionea sana Uholanzi kwenye mechi zao nyingi walizokutana.

Ureno walipata matokeo dhidi ya Uholanzi katika mechi zifuatazo, wakiwafunga kwenye hatua ya 16 bora kwenye kombe la dunia 2006, kwenye nusu fainali ya Euro 2004 wakwafunga tena 2-1, na kwenye kufuzu kombe la dunia 2002 wakawatungua 2-0, na Euro 92 kwa 1-0. Pia hawajawahi kufungwa na Uholanzi kwenye mechi za kirafiki.

Mechi pekee ambayo Wadachi waliwafunga Ureno ilikuwa mwezI wa 10, 1991 mjini Rotterdam kwa 1-0 katika mechi za kufuzu Euro. Robert Witchge aliwafungia The Oranje goli pekee.

Kama wataweza kuwafunga Ureno kwa mara ya pili kwenye historia yao kwa idadi ya magoli mawili au zaidi, basi itabidi wasali na kuomba Denmark wafanye walichofanya miaka 10 iliyopita kwenye Euro 1992 kwa kuwafunga tena Ujerumani.

FERNANDO TORRES NDIO KAISHIKA BAHATI YA SPAIN: HAIJAWAHI KUFUNGWA KILA TORRES ANAPOFUNGA

Spain walipiga hatua muhimu kuelekea kwenye robo fainali ya michuano ya Euro 2012 alhamisi iliyopita kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland. Kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Italia, La Roja waliacha mashaka makubwa kwenye kiwango chao ambacho kilifeli kuwashinda Waitaliano, huku Cesc Fabregas akianza katika mfumo wa kuchezesha timu bila kuwa na mshambuliaji halisi. Lakini kwenye mchezo wao wa pili, Fernando Torres akianza badala ya Fabregas, Spain walirudisha kiwango chao, wakicheza kwa kuelewana zaidi, pasi nzuri na za maana na kikubwa zaidi walipata magoli.

Kwenye mchezo wao ufunguzi, kocha Vicente De Bosque alianzisha kikosi kisichokuwa na mshambuliaji halisi na alitupia lawama nyingi baada ya mchezo, japokuwa Fabregas aliyecheza kama mshambuliaji kivuli, alifunga goli pekee la kusawazisha goli la Antonio Di Natale. Torres aliingia kama sub dakika ya 16 kabla ya mchezo wa kumalizika lakini hakuweza kubadili matokeo ya sare, pamoja na kupata nafasi mbili za wazi mwishoni mwa mchezo huo. Dhidi ya Ireland, magoli yake mawili yalionyesha ni kiasi gani ana umuhimu kwenye kikosi cha kwanza.


Torres alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi na Uefa, pia akafikia rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu kwa kuifungia Spain magoli mengi, akiwa na goli 30. Akimpita Fernando Hierro mwenye magoli 29, huku akiwa nyuma ya Raul mwenye 44, na David Villa mwenye mabao 51.

El Nino, 28, ambaye alifunga goli pekee liloipa ubingwa wa Euro 2008 Spain, wakati walipoifunga Ujerumani na kumaliza ukame wa miaka 44 wa makombe nchini Austria na Switzerland, amekuwa na bahati sna ndani ya timu ya taifa, La Roja haijawahi kupoteza mechi ambayo Fernando Torres anafunga.

Spain wameshinda mechi za 21 za mwisho ambazo Torres anakuwa amefunga. Mechi pekee ambayo Fernando alifunga na Spain wakashindwa kushinda ilikuwa mwaka 2004 mjini Genoa, dhidi Italy. Hili ndilo lilikuwa goli la kwanza la Torres kuifungia La Roja.

Katika magoli yake 30, zimekuwepo hat ticks mbili, moja dhidi ya San Marino na nyingine dhidi ya New Zealand, akifunga ndani ya dakika 17 za mchezo kwenye kombe la mabara, na kuweka rekodi ya kuwa hat tick ya haraka zaidi katika historia ya La Roja.

Italy, San Marino, China, Belgium, Slavakia, Croatia, Ukraine, Tunisia, Liechtenstein, Latvia, Sweden, Germany, Chille, Azerbaijan, New Zealand, Macedonia, Poland, United States, South Korea na sasa Ireland timu hizi zote zimekutana na balaa la Fernando Torres, huku goli muhimu zaidi likiwa lile alilowafunga vijana wa Joachim Low kwenye fainali ya Euro 2008.

So mashabiki wa Spain sasa itabidi waombe kuwepo na ufanano huu kwa mshambulaiji huyu ili kuweza kufanikisha azma yao ya kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuchukua makombe matatu makubwa mfululizo.

IANDIKIE CAPTION HII PICHA!

TASWA tunaomba vigezo vya kumpa Shomari Kapombe tuzo ya uanamichezo bora wa msimu wa 2011/12


HOJA YANGU: TASWA tunaomba vigezo vya kumpa Shomari Kapombe tuzo ya uanamichezo bora wa mwaka 2011/12. Hapa hoja yangu ni kwamba, Kapombe anacheza soka, na katika soka mshindi wa tuzo ni Aggrey Morris. Ina maana Aggrey ndiye mchezaji wa soka bora kuliko wote kwa msimu uliopita. Yes, Kapombe kapata tuzo ya chipukizi bora, kwa maana kuwa kawazidi chipukizi wenzake, lakini kwa soka kwa ujumla amezidi...wa na Aggrey Morris. Sasa hapa ndipo ninaposhindwa kuelewa kirahisi vigezo vilivyotumika. Inakuwaje mtu apewe tuzo ya uanamichezo bora wakati kwenye mchezo anaoucheza wapo watu walio bora kuliko yeye? Ndio kawazidi ubora chipukizi wenzie, lakini kwa soka kwa ujumla aliye bora kuliko wote tuzo kapewa Aggrey Morris. Suala jingine ni je, tuzo za TASWA kwa mwanamichezo bora wa mwaka zinaangalia Watanzania tu? Kwa sababu wengi mtakubaliana nami kuwa hata kwa klabu yake ya simba Kapombe amezidiwa ubora na Emmanuel Okwi kwa vigezo vya kuonesha uwezo mkubwa kuisaidia timu yake ya Taifa kutwaa kombe la Challenge, mchango mkubwa kuisaidia simba kutwaa ligi kuu, na mchango mkubwa kuisaidia simba kung'ara kombe la shirikisho CAF. TASWA naomba vigezo tafadhali.
  • TASWA NI KAMA KAMATI YA HARUSI AKUNA JIPYA KAMA UNABISHA NIONYESHENI OFISI YAKE ALAFU WAACHE WAFANYE VILE WANAVYOTAKA BAADHI YA WAJUMBE NA VIONGOZI HAWANA VISION YA TASWA ILA WANAVISIONI ZAO BINAFSI KAZI IPO KWENYE MICHEZO YA BONGO.
  •  
    Mchezaji bora wa jumla wa taswa 2011/12 shomari kapombe..........vigezo tafadhali wadau...

    KOCHA WA VIJANA JIJINI MWANZA AFARIKI DUNIA

    Mchopa one of the youth coaches in Mwanza, and who was involved in the Tanzania team selecting for the Street Child World Cup 2010 has died. Mchopa will be remember for his time during the preparation of the team and helped with selection of the team during the Mwanza Regional Street Children Tournament.COACH MCHOPA

    EPIQ BONGO STAR SEARCH YAANZA KWA KISHINDO DODOMA

    Zoezi la kutafuta washiriki wa Epiq BSS mkoani Dodoma lilianza kwa baadhi ya watu akiwemo Madam Rita kuchangia damu.

    Mmoja wa washiriki wa Epiq BSS  akiwa anafanya mazoezi kabla ya kuingia kwenye auditions.


    Baadhi ya washiriki ya EBSS mkoani Dodoma wakijiandaa kuingia kwenye auditions

    Majaji Salama Jay, Master Jay and Madam Rita
    Mshiriki kwenye mbele ya majaji

    Winner Lucas mwanafunzi wa UDOMaliwashangaza wengi kwa uwezo mkubwa wa kurap.


    MBWANA SAMATTA NA ULIMWENGU KUONGOZA SAFU YA MSHAMBULIZI YA STARS LEO DHIDI MSUMBIJI

    KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulen ametaja kikosi chake kitakachoanza mechi ya leo dhidi ya Msumbiji (The Mambas) itakayochezwa Uwanja wa Taifa ulioko Zimpeto hapa Maputo. Mechi itaanza saa 9 kamili kwa saa za hapa ambapo nyumbani
    Tanzania itakuwa saa 10 kamili.

    Stars inaundwa na;1. Juma Kaseja, 20. Shomari Kapombe, 22. Erasto Nyoni, 6. Aggrey Morris, 5. Kevin Yondani, 19. Shaabani Nditi, 8. Mrisho Ngasa, 16. Frank Domayo, 11. Thomas Ulimwengu, 10. Mbwana Samata na 15. Mwinyi Kazimoto.


    Wachezaji wa akiba;18. Deogratias Munishi, 17. Amir Maftah, 13. Jonas Mkude, 3. Haruna Moshi, 12. Simon Msuva, 9. Christopher Edward, 14. John Bocco, 7. Ramadhan Singano na 21. Nurdin Bakari.


    Benchi la Ufundi;

    Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk. Juma Mwankemwa (Daktari wa Timu), Dk. Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).

    Refa: Bennett Daniel (Afrika Kusini)

    Refa Msaidizi 1; Molefe Enock (Afrika Kusini)
    Refa Msaidizi 2; Siwela Zakhele Thusi (Afrika Kusini)
    Refa wa Akiba; Hlungwani Tinyiko Victor (Afrika Kusini)
    Kamishna wa Mechi; Mateus Joel Amdhila (Namibia)

    HAPPY BIRTHDAY QUEEN WA BONGO FLEVA LADY JAY DEE

    Usiku wa kuamkia leo, ilifanyika sherehe ya kumpongeza mwanamuziki gwiji wa Bongo Fleva Lady Jay Dee kwa kutimiza miaka 33 tangu aingie kwenye ulimwengu huu, na mie nilikuwa mmoja ya watu tuliodhuria.

     Maggie akiwa ameikamatia keki kuipeleka mbele.
     Lady Jay Dee akipokea keki yake huku Barnaba akimuimbia kwa furaha.
     Ukumbusho.
     Kila mmoja alikuwa akitaka kupiga picha ya ukumbusho.
     ...akikata keki yake kwa taratibu kabisa...
     Wa kwanza kulishwa keki alikuwa ni Barnaba Boy...
     Shabiki wa machozi bendi akiwakilisha...
     ... raha kweli
                        Khadija Mwanamboka hakuwa nyuma kuwalisha...




    Haki Ngowi...

    LEWANDOSKI ASHINDWA KUIOKOA POLAND KUAGA MAPEMA EURO: WAFUNGWA CZECH 1-0


    Czech Republic 1-0 Poland Match highlights... by eurorivals

    WAGIRIKI WAWATOA AKINA ARSHAVIN KWENYE EURO


    GREECE 1-0 RUSSIA Match highlights Euro2012 16... by eurorivals

    TWIGA YATOLEWA NA ETHIOPIA MICHAUANO YA KUWANIA KUFUZU AFCON

    Baada ya jitihada kubwa ya kusaka goli la ugenini katika kipindi cha kwanza timu ya Taifa kwa soka la wanawake ya Ethiopia walifanikiwa kulipata dakika ya 69 na kuiondoa wanawake wenzao Watanzania 'Twiga Stars' kwa jumla ya goli 3-1.

    Katika mchezo huo wa raundi ya mwisho kusaka tiketi ya kufuzu mataifa ya Afrika kwa Soka la Wanawake yatakayo fanyika hapo baadae nchini Gabon, uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ulimalizika kwa Ethiopia kuibuka na ushindi wa goli 1-0.


    Katika mchezo huo, hususani katika kipindi cha kwanza ulibidi Twiga Stars wabaki nyuma wakiokoa hatari lukuki na shukrani zimuendee kipa wa Twiga Stars na safu nzima ya ulinzi kuzuia mashambulizi ya Ethiopia katika kipindi chote cha kwanza.


    Baada ya jitihada za kuzuia mashambulizi ya Waethiopia, katika dakika 69 walinzi wa Twiga Stars walifanya kosa lililo wapa ushindi Ethiopia na kukata tiketi ya kwenda Gabon.


    Katika mchezo wa awali uliochezwa jijini Adis ababa ulimalizika kwa Twiga Stars kufungwa goli 2-1, hivyo kuondolewa kwa jumla ya goli 3-1.

    SHOMARI KAPOMBE: SHABIKI WA MAN UNITED ALIYETOKA KUOKOTA MPIRA MPAKA TEGEMEO SIMBA NA STARS.

    Na Andrew Chale

    MIONGONI mwa majina yanayoanza kuvuma kwa kasi hivi sasa kwenye medani ya soka hapa nchini, hutokosa kusikia jina la Shomari Kapombe.


    Nyota chipukizi wa Klabu ya Simba ‘Wekundu wa Msimbazi’, Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 23 na hivi sasa Taifa Stars.

    Shomari Kapombe baada ya kufanya kweli hivi karibuni U-23 iliyokuwa ikiwania kufuzu michuano ya Olimpiki na Mataifa ya Afrika, na kwenye mechi kadhaa za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu bara iliyomalizika Novemba 3, akiwa na vinara wa ligi hiyo, Simba, Kocha Jan Borge Poulsen, hatimaye kamuona.

    Kapombe, amebahatika kuitwa kwa mara ya kwanza katika historia yake ya soka, baada ya kubahatika kuitwa kikosi cha Stars, chini ya Kocha Mkuu, Jan Poulsen, ambacho kiko kambini kikijiwinda na mechi ya kuwania kupangwa kwenye makundi ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia, dhidi ya Chad, itakayopigwa jijini Nd’jamena, Novemba 11, kabla ya kurejeana siku nne baadaye jijini Dar es Salaam.

    Katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima, Kapombe mwenye historia ndefu katika medani ya soka, licha ya kuwa na umri mdogo, baada ya kutua Simba msimu huu, amefanikiwa kupigana vilivyo na kula sahani moja na nyota kadhaa wakongwe na wa kimataifa na kufanikiwa kucheza mechi karibu zote za mzunguko wa kwanza.

    Kocha wa Stars, Poulsen alimwelezea, Kapombe kama mchezaji wa kipekee ambaye ana uwezo mkubwa, hivyo kumuita katika kikosi chake akiwa ana matumaini kuwa atafanya vema kwa kusaidiana na chipukizi wenzake Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata ambao aliwahi kucheza nao U-23.

    Mbali na Poulsen kukubali uwezo wa chipukizi huyo, mashabiki wengi bila unazi, pia wameonekana kukubaliana na kiwango chake huku wakimtabiria kufanya vema.

    DOGO HUYU KATOKA WAPI?

    Kapombe anasema soka iko katika damu, kwani alianza kuupenda tangu akiwa na miaka mitano mkoani Morogoro, alikokuwa akicheza ‘chandimu’ katika timu yao ya mtaani kwao Mafiga.

    Anasema umri ulivyoongezeka alijiunga na timu ya Santos Fc, ambayo alifanikiwa kuichezea michuano mbalimbali akiwa bado kinda.

    Anaitaja baadhi ya michuano hiyo kuwa ni ‘Serve Access Game’ iliyokuwa ikiandaliwa na taasisi ya kuendeleza vipaji vya soka ya Morogoro Youth Academy.

    KUOKOTA MIPIRA UWANJANI

    Kapombe anabainisha kuwa mbali ya kuchezea Santos, awali aliichezea timu ya watoto wanaookota mipira kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, ‘Jamhuri Ball Boys’.

    “Nilipitia timu mbalimbali wakati nakua, ikiwemo ya Mafiga Kids, Santos Fc, Jamhuri Ball Boys mpaka nilipokuja kuonekana na kituo cha Moro Youth Academy,” anasema Kapombe.

    Wakati akicheza katika timu zote hizo, alikuwa na shauku ya kufika mbali, huku kubwa zaidi ilikuwa ni ndoto ya kuchezea timu bora Tanzania, ama duniani.

    “Nilipokuwa Ball Boys pale uwanja wa Jamhuri, Morogoro, nilikuwa na shauku kubwa na mimi kucheza timu kubwa kama Mtibwa, Simba, Yanga na nyingine nyingi ambazo nilikuwa nikivutiwa nazo wakati zikija kucheza Jamhuri … nilijipa moyo, kwani nilikuwa nikiongeza juhudi zangu katika mazoezi, ili kutimiza ndoto na kweli imetimia,” anasema Kapombe.

    Akiwa na kikosi hicho cha Jamhuri Ball Boys, U-14, aliweza kukiongoza akiwa kama nahodha katika michuano ya WINOME Cup na michuano ya Serve Access Games, alikong’ara, ndipo kituo hicho cha Moro Youth kilivutiwa naye na kumchukua.

    Kapombe anampongeza kocha wake, Yahaya Belin, aliyekuwa akimnoa Jamhuri Ball Boys, kwa kumsaidia mbinu mbalimbali za uchezaji, ikiwemo kujituma kucheza namba mbalimbali uwanjani.

    “Kocha Belin, alikuwa akinisihi kucheza namba tofauti tofauti uwanjani, ili kuweza kuikoa timu pindi inapokuwa imezidiwa kimchezo...kwa hali hiyo, nilikuwa nakumbuka mawazo yake na mimi nilikuwa nikifuata mawazo yake mpaka leo matunda yake nayaona,” anasema Kapombe.

    Akiwa katika kituo hicho cha Moro Youth, baadaye alipanda hadi kikosi cha U-17 cha kituo hicho, ambako aliweza kuchaguliwa kuwa nahodha wa timu ya mkoa wa Morogoro iliyoshiriki michuano ya Copa Coca-Cola 2008, wakati huo akiwa na miaka 16.

    Anasema katika mashindano hayo walitolewa hatua ya robo fainali na Kigoma ambayo ilikuja kuwa mabingwa.

    Kapombe anasema baada ya mashindano hayo ya Copa Coca-Cola 2008, walichaguliwa wachezaji wengi nyota, akiwemo Zahoro Zeiran waliyetoka naye mkoa wa Morogoro ambapo baadaye walikwenda nchini Brazil. “Baada ya michuano ile, nilirudi katika kituo huku nikiendelea na shule na baadaye timu ya Polisi Morogoro walinichukua,” anasema.

    Anaongeza kuwa alichukuliwa yeye na wachezaji wenzake 6, kwenda Polisi Morogoro wakiwa kikosi B ambako walishiriki michuano ya timu za vijana za Ligi Kuu ‘Uhai Cup 2009’, kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza na kucheza Ligi Daraja la Kwanza kituo cha Tanga, akiwa na timu hiyo mwaka jana.

    “Nakumbuka kulikuwa na mechi kati yetu na timu moja ya Arusha ambapo katika mchezo huo, kulikuwapo na kocha Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ambaye aliridhishwa na uwezo wangu na kunieleza kuwa ningekuwemo katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 na kuanzia hapo nilijiunga na kikosi hicho,” anasema.

    Akiwa na U-23, Kapombe anasema aliweza kuonesha uwezo mkubwa, ikiwemo kwenye hatua za kufuzu michuano ya kimataifa kama vile All African Games na Olimpiki ambapo aliweza kucheza mechi zote, nyumbani na ugenini, ikiwemo na timu za Cameroon, Nigeria na Uganda, jambo lililomuongezea uwezo wake kutoka ule wa awali.

    KUIBUKIA SIMBA SC

    Kapombe anasema kuwa ndoto yake ilikuwa ni kuona anasonga mbele, ikiwemo kucheza kwenye klabu kubwa nchini na nje ya nchi.

    “Naikumbuka mechi baina ya U-23 dhidi ya Cameroon, mchezo uliochezwa kwenye dimba la Taifa, siku hiyo viongozi wa Simba walinifuata na kunieleza nia ya kujiunga na Wekundu hao wa Msimbazi.

    Kwangu niliona ni bahati ya pekee, kwani kikosi kizima kilikuwa na wachezaji mahiri, lakini kwa kuwa Simba walinifuata mimi sikuwa na hiyana na nikamshukuru Mungu kuwa ndoto zangu zilikuwa zimeanza kutimia,” anasema Kapombe.

    Anasema, baada ya kujiunga na Wekundu hao, furaha yake ilizidi pale alipokabidhiwa jezi namba 15 na kuwa miongoni mwa wachezaji 18 wa kikosi cha kwanza cha kutumainiwa cha Kocha Mganda, Moses Basena.

    “Baada ya kumaliza sherehe za Simba Day, Arusha, nilijisikia furaha na sikuamini machoni mwangu kama nimechaguliwa kuwa kikosi cha kwanza cha Simba cha wachezaji 18, huku nikikabidhiwa jezi yangu namba 15,” anasema Kapombe.

    Anasema kuwa kwa kuwa Basena alimfundisha kujiamini, aliweza kucheza mechi dhidi ya Yanga kwenye Ngao ya Hisani, ambayo ilikuwa na uangalizi mkubwa ambapo aliingia kipindi cha pili na aliweza kucheza vema bila woga, huku akitumia zaidi uwezo na maarifa ya soka.

    Kapombe anasema, katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu bara, ameweza kucheza mechi zote 13, huku kati ya hizo tisa akicheza dakika zote 90.

    “Ni hakika nimeonyesha uwezo katika mzunguko wa kwanza, hivyo mzunguko wa pili mashabiki wa Simba na wapenda soka wataona vitu vyangu zaidi ya nilivyoonyesha mzunguko wa kwanza...,” anasema.

    KUITWA TAIFA STARS

    Anasema kuwa aliposikia kwenye vyombo vya habari juu ya kuteuliwa jina lake, hakuamini na hata ndugu na jamaa walipomwambia kuchaguliwa kwake huko, bado hakuamini hadi alipohakikisha mwenyewe siku ya pili yake.

    “Sikuamini kwa mara ya kwanza kama nimebahatika kuchaguliwa kikosi cha timu ya taifa, siku ya pili niliposoma magazeti na kupigiwa simu na uongozi juu ya kuchaguliwa kwangu, kwanza nilimshukuru Mungu kwa kuniwezesha kwake,” anasema Kapombe.

    Anasema uwepo wake ndani ya kikosi hicho cha Stars ni kielelezo tosha cha vijana kuisaidia timu ya taifa, ili iweze kufanya vema na kupata mafanikio ya soka hapa nchini.

    “Poulsen ameona mbali, hasa kwa kujaribu kutumia damu changa... uwepo wangu ndani ya kikosi cha Taifa Stars ni changamoto tosha na nawaomba Watanzania wazidi kutuombea, nasi tutajitahidi na tutasonga mbele,” anasema Kapombe.

    HISTORIA KWA UFUPI

    Shomari Kapombe ni kitinda mimba katika familia ya watoto watatu wa Mzee Salum Kapombe wa mjini Morogoro.

    Alizaliwa Januari 28, 1992 katika hospitali ya mkoa wa Morogoro ambapo elimu ya msingi aliipata shule ya Mwale, mwaka 2000 hadi 2006, huku akiwa anajihusisha na soka.

    Aliendelea na soka alipojiunga na Shule ya Sekondari ya Lupanga iliyo jirani na Chuo cha Ualimu Kigurunyembe, mwaka 2007 hadi 2010.

    SIFA ZA ZIADA

    Shomari Kapombe, anasema binafsi amejaliwa kipaji cha kutumia miguu yote miwili na pia awapo uwanjani, hategemei kucheza namba moja.

    “Katika kikosi cha U-23, nacheza pembeni kama beki tatu... hivyo hivyo na kwenye klabu yangu ya Simba, ambayo pia wakati mwingine huwa nabadilisha namba,” anasema.

    Kapombe anasema siku zote amekuwa akitamani sana uchezaji wa Haruna Moshi ‘Boban’ kwani ndiyo unaomvutia kwa hapa nchini na awapo uwanjani hufuata nyayo zake na anaamini iko siku naye atafika mbali ikiwemo kucheza soka la kulipwa Ulaya.

    Kwa upande wa kimataifa, anakunwa na Tom Cleverley wa Mashetani Wekundu na pia ni shabiki mkubwa wa Manchester United ya England.

    SHUKRANI

    Nyota huyo anasema, katika maisha yake hatoweza kuwasahau walimu pamoja na wazazi wake, kwa kumtia moyo hadi hapa alipofikia.

    Anawataja makocha wake hao kuwa ni Yahaya Belin, Allan Sigo pamoja na Rajabu Kindagule wa Moro Youth, John Tamba Polisi Morogoro, Jamhuri Kiwelu ‘Julio’, Moses Basena Simba pamoja na Jan Poulsen wa Taifa Stars.

    ASICHOKISAHAU

    Kapombe anasema kuwa katika maisha yake hatosahu walipokuwa safarini kuelekea mjini Younde, Cameroon, mwanzoni mwa mwaka huu, hali ya hewa ilikuwa mbaya angani, hivyo kusababisha ndege waliyokuwa wamepanda kuyumba sana ikiwa angani.

    “Nilikuwa na hofu kubwa sana, kwani hali ile ilinifanya nibadilike sana kwa hofu, hali ilikuwa mbaya sana na tukio lile sitolisahau kamwe, lakini Mungu alitusaidia na tulifika salama,” anasema.

    DONDOO

    JINA KAMILI: Shomari Salum Kapombe.

    KUZALIWA: Januari 28, 1992.

    MAHALI: Morogoro.

    TIMU YA MTAANI: Santos Fc, Mafiga Kids na Jamhuri Ball Boys.

    KITUO CHA SOKA: Moro Youth Academy
    TIMU YA AWALI: Polisi Morogoro
    TIMU YA SASA: Simba Sports Club
    TIMU ZA TAIFA: Taifa Stars/ U23
    NAFASI UWANJANI: Kiraka/Kiungo
    NAMBA YA JEZI: Klabu 15, U-23 namba 13, Taifa Stars ?

    IDADI MECHI ZA KIMATAIFA: 10.

    LIGI KUU: Mzunguko wa kwanza-13.

    IDADI YA KADI: Njano moja, U-23 vs Nigeria.

    UTAIFA: Tanzania
    ELIMU: Kidato cha nne

    KWANINI WACHEZAJI WAKUBWA WALIOTAMBA BARANI ULAYA WANAKIMBILIA UARABUNI KUCHEZA SOKA?

    Raul Gonzales akitambulishwa kujiunga klabu ya Al Sadd ya Qatar hivi karibuni.
    Katika miaka ya hivi karibuni nchi za kiarabu haswa nchi ya Qatar ndio imekuwa ikionekana kuongoza mbio za kuwasajili makocha na wachezaji wenye makubwa waliotamba kwenye ramani ya dunia ya soka kupitia vilabu vyao tofauti.


    Wachezaji wakubwa kama Gabriel Batistuta, Eric Djemba Djemba, Marcelly Desailly, Christopher Dugarry, Claudio Caniggia, Jay Jay Okocha, Taribo West, Frank and Ronald De Boer, John Utaka, Mario Basler, Hakan Yakin, Paulo Wanchope, Juninho Pernambucano,  Stefan Effenberg, Emile Mpenza, Youseff Chippo, Tony Yeaboah, Victor Ikpeba, Titi Camarra, Abedi Pele, Frank Lebouef, Pep Guardiola, Mauro Zarate(anayecheza Inter Milan) walishawahi kucheza soka nchini Qatar, Huku makocha wakubwa kama Bruno Metsu, Rene Meulesteen wa Man United, Bora Milutinovic, Emerson Leao, wakiwa tayari wameshafundisha soka ndani ya nchi hiyo kwenye miaka kadhaa iliyopita huku wengine wakiwepo na wakiendelea na kazi zao.

    Pia wachezaji kama, Mamadou Niang, Kader Keita, Karim Zian, Mario Melchiot, Aruna Dindane, nahodha wa Korea Kusini Lee Jung-Soo bila kumsahau mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid na klabu bingwa ya ulaya  Raul Gonzales Blanco wamekuwa sura mpya za mastaa walioweka vizuri barani ulaya na Afrika kuwepo ndani ya soka la Qatar.


    Qatar ambayo yenyewe tofauti na nchi zingine za kiarabu yenyewe miaka kadhaa ya nyuma haikuwa ikionekana sana kwenye ramani ya soka, leo hii ndio nchi ya kiarabu yenye mafanikio makubwa kuijumla ya kisoka ndani ya miaka miwili iliyopita, wakifanikiwa kuwashinda Waingereza na wamarekani kwenye mbio za kuandaa faianli ya kombe la dunia mwaka 2022, huku kubwa klabu ya nchi hiyo ikibeba kombe la mabingwa wa Asia mwaka jana.


    Pia makampuni makubwa na matajiri wa nchi hiyo yamekuwa yakiwekeza sana kwenye soka, kwa mfano mwaka jana tulishuhudia klabu ya Barcelona ikivunja mwiko wa kutokuwa na mdhamini wa jezi baada ya kuingia mkataba mnono na Qatr Foundation, huku pia klabu ya Malaga ya Spain ikinunuliwa na tajiri raia wa Qatar, bila kuwasahau matajiri wapya wa ulaya klabu ya PSG inayomilikiwa Qatar Investment Authority.


    Baadhi ya wadau wa soka ulimwenguni nikiwemo mimi nimekuwa nikijiuliza namna nchi hii sasa inavyojaribu kuuteka ulimwengu wa soka, na ndipo nilipokutana na mchezaji wa klabu ya Al Sadd Ally Hassan Afif nikafanikiwa kupata majibu yangu.


    Afif anasema: "Baada ya muda mrefu nchi yetu ya Qatar kupigwa bao na majirani zetu kama Oman, Saudi Arabia na wengineo kwenye soka, ndipo serikali pamoja na wadau(vilabu) wa soka wa Qatar walipoamua kuwekeza kwenye soka na kuweka mipango bora itakayovutiwa wachezajiwa kigeni kuja kucheza hapa.
    Kwanza katika kuifanya soka ya Qatar itambulike kimataifa wakanza kuwasajili wachezaji wenye umaarufu mkubwa huku wakiwa wanawalipa fedha nyingi bila kukatwa kodi, pia wakawa wanasaini makocha wenye ujuzi na majina kwenye ramani ya dunia ya soka.
    Kupitia hili vilabu vilifanikiwa kuwavutia wachezaji wengi maarufu na wenye uwezo kujiunga navyo, kwa kuwa walikuwa wakilipwa fedha nyingi sana kama ilivyo barani ulaya lakini kwa Qatar wakiwa hawalipi kodi, kiukweli hili ndilo limesaidia sana kuitangaza nchi yetu, hivyo hii ndio siri kubwa inayowafanya wachezaji kama akina Raul wamekuja kucheza soka huku.
    Jambo lingine ambalo lilikuwa kwenye mkakati ni kuweza kupata nafasi ya kushinda uenyeji wa kuandaa michuano ya kombe la dunia na alhamdulilah mwaka jana tulifanikiwa kwa hilo na mungu ankipenda mwaka 2022, Qatar tutacheza World Cup tukiwa kwenye ardhi yetu.
    Pia serikali na wafanyabiashara wakubwa kupitia makampuni yao makubwa wakaanzisha mkakati wa kununua vilabu maarufu barani ulaya pamoja na kutoa udhamini, ndio tunavyoona Paris Saint-German na Malaga zote zimenunuliwa na watu wa Qatar, huku Barcelona ambayo ndio klabu ya pili kwa umaarufu duniani baada ya Manchester United, wakiwa wanadhaminiwa na Qatar Foundation. Hii siri ya mafanikio ya nchi ya Qatar katika kuendeleza soka letu pamoja na kufahamika kwenye ulimwengu wa soka."
     

    EXCLUSIVE: PAWASA ALIUKIMBIA UTAJIRI QATAR - WAARABU BADO WANAMKUMBUKA ASEMA AFIF