Search This Blog

Tuesday, March 6, 2012

MPAMBANO WA SIMBA NA KIYOVU WAINGIZA MILIONI 208!

TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
CAF CONFEDERATION CUP 2012
SALES RECORDS SUMMARY
SIMBA VS KIYOVU
 standqntysoldf/passunsoldGt/feeamountexpectation
  1      
1VIP A74028720025330,0008,610,000                              22,200,000.00
2VIP B3,760965922,70320,00019,300,000                              75,200,000.00
3VIP C4,077692503,33515,00010,380,000                              61,155,000.00
4ORANGE ROUND10,8972,581268,2908,00020,648,000                              87,176,000.00
5BLUE/GREEN ROUND36,64629,98106,6655,000149,905,000                             183,230,000.00
          
 TOTAL56,12034,50636821,246          208,843,000.00              428,961,000.00
          
   
      
                 
     
 1              
       1  

ANDRE VILLAS-BOAS KWENYE MAZUNGUMZO YA SIRI KUCHUKUA KIBARUA LUISI ENRIQUE ROMA.

Andre Villas-Boas alikutana kwa siri mjini London na mkurugenzi wa AS Roma Franco Baldini mwezi uliopita kuzungumza juu ya mreno huyo kuwa kocha wa klabu hiyo msimu ujao imefahamika.
AVB, ambaye alitimuliwa na Chelsea juzi Jumapili, amekuwa akiwindwa na seria A club kumbadili kocha wa sasa Luis Enrique kipindi kijacho cha kiangazi.
Mtandao wa Goal.com umeweka wazi kwamba mazungumzo katika ya AVB na Baldini yalifanyika katika mgahawa ambao upo karibu na makazi ya Baldini, ambaye aliacha kazi katika timu ya taifa ya England na kujiunga na Roma in October.
Villas-Boas aliulizwa na Baldini kama angekuwa interested kumrithi Enrique, ambaye inasemekana ndio kocha Anayetajwa kumrithi Pep Guardiola akiwa aamua kuhama kocha ataamua kuondoka Nou Camp mwishoni mwa msimu.
Mreno inasemekana alimjibu msaidizi wa zamani wa Capello kwamba alikuwa akihofia kufukuzwa kazi wakati wowote kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya, hivyo alikuwa tayari kuhamia Roma.
Pia Goal.com imefichua kwamba AVB alishakutana na watu  wa AS Roma kabla ya Enrique hajahamia klabuni pale wakati alipokuwa Porto lakini watoto wa PAPA walishindwa dau la kumtoa Porto paundi millioni13.4 ambayo ilikuja kulipwa na Chelsea.
Enrique anaonekana sio mtu wa kufukuzwa Roma – ambayo ni yasita katika msimamo , lakini kuna vishiaria vyote vinavyoonesha kwamba hatakuwepo Italy msimu ujao.
 Chanzo cha habari kutoka kwa Mhispania huyo kinasema kuna makubaliano yam domo kati ya raisi wa Barcelona Sandro Rossell kuchukua nafasi ya Pep ikiwa kocha huyo wa sasa ataamua kuachana na klabu hiyo kwa sasa.
Akiongea baada ya kufungwa katika derby dhidi ya Lazio wikiendi iliyopita, Enrique alisema: “      Kama mpaka sasa siaminiki kama kocha sahihi wa Roma then nitaondoka bila matatizo yoyote.

CHELSEA YAMSAINI KIPENZI CHA MASHABIKI WA TIMU HIYO KATIKA BENCHI LA UFUNDI.

Newton akisalimiana na Ashley Cole huku John Terry na Di Matteo wakiangalia.
 Chelsea wamejitoa kuwatuliza wachezaji kwa kumleta kipenzi  cha klabu hiyo Eddie Newton kuja kuwa kuchukua nafasi katika benchi la ufundi kwa pamoja na mrithi wa muda wa AVB
Roberto Di Matteo.
Mchezaji huyo wa zamani wa The Blues  - ambaye alicheza mechi zaidi ya 200 kwa klabu hiyo aliungana na kikosi cha sasa leo jumatatu katika uwanja wa mazoezi wa Cobham.
Hii imekuja masaa 24 baada ya Andre Villas-Boas kutimuliwa na Roman Abramovich, ambaye sasa anasaka kocha wa 8 katika miaka 9 tangu alipoinunua timu hiyo.

Marafiki wakweli -tangu wakiwawachezaji mpaka makocha.

Newton aliambia Sky Sports: “Hii kwa ya The Blues. Lengo ni kuisadia timu angalau kupatanafasi ya nne.
“Kila mchezo ni muhimu kutoka sasa mpaka mwisho wa msimu.”
Aliongeza; “Siwezi kuongelea kilichokuwa kinatokea kabla, lakini sasa nipo Chelsea na ninachotaka pamoja na staff wenzangu wote kujitahidi kupata ushindi katika kila mechi na tutaendelea kufanya mpaka iwe tabia tena.”
Staffs wengine waliomfuata Villas-Boas ni Kocha wa fitness Jose Mario Rocha na skauti wa kufuatiliwa wapinzani Daniel Sousa.
Newton alijiunga na Chelsea akiwa na miaka 13 na hatimaye alicheza mechi yake ya kwanza mwaka 1992. Wote wawili Newton na Di Matteo walifunga katika fainali ya kombe la FA Cup dhidi ya Middlesbrough.
Newton na Di Matteo pia walifanya kazi ya ukocha katika za West Brom na MK Dons.

Monday, March 5, 2012

ZLATAN IBRAHIMOVIC: KWANINI NILIKATAA KUJIUNGA NA ARSENAL?



Zlatan Ibrahimovic amefichua kwamba alikataa kuhamia Arsenal kwa sababu Arsene Wenger alitaka mshambuliaji huyo aanzie kwanza kwenye majaribio.
AC Milan player alikuwa mdogo kiumri alipokutana na Wenger in 2000 kuzungumza juu ya uwezekano wa kuhamia London ya kusini.
Ibrahimovic, 30, aliliambia gazeti la The Sun: ‘Arsene alinipa jezi maarufu ya rangi nyekundu na nyeupe – ikiwa imeandikwa jina langu na namba tisa mgongoni, nilifurahi sana hata nikapiga picha na jezi ile.
“Ulikuwa ni wakati mzuri kwangu. Arsenal walikuwa na kikosi kizuri sana lakini wakanifuata mie huku jezi namba 9 ikiwa na jina langu mgongoni.
“Hivyo nikasubiri Wenger anishawishi nijiunge na Arsenal. Lakini hata hakujaribu.
“Hakuwahi kunipa ofa iliyo serious, ilikuwa like “Nataka kuona unajua kucheza vizuri kiasi gani, yaani nifanye majaribio”
“Sikuweza kuamini kwa sababu uwezo wangu alishauona. Zlatan hawezi kufanya majaribio.
“Niliwaza “Aidha hunijui au unanijua na kama hunijui basi huwezi kunitaka mimi”.
“Unaona , hata nilipokuwa mdogo nilikuwa najiamini sana hata kama nilikuwa mdogo.
“Nina hakika kwamba kuna baadhi ya wachezaji wachanga wangeweza kukubali kufanya majaribio kwa sababu ilikuwa ni Arsenal na Yule alikuwa na Arsene Wenger.
“Lakini nilijua haikuwa tu ni Arsenal waliokuwa wakinitaka – Roma na Ajax zote zilikuwa zikipigania saini yangu.
“Hivyo nilisema “Hapana na mwisho wa siku nilisaini kwa Ajax, Lilikuwa chaguo sahihi.
Ibrahimovic badala yake akajiunga na Ajax , ambapo alichukua makombe 8 mfululizo, na baadae akaenda Juventus – ambapo alishinda makombe mawili ambayo baadae walipokonywa kutokana na scandal ya Calciopoli kabla hajaenda Inter, Barcelona na sasa yupo Milan.


Pia alikuwemo katika kikosi cha Milan kilichoshinda goli 4-0 dhidi ya Arsenal katika Champions league, na akafunga hat-trick jana usiku dhidi ya Palermo.
Arsenal wanacheza na Milan jumanne iajyo katika mechi ya pili ya hatua ya 16 bora.

Sunday, March 4, 2012

BREAKING NEWS: VILLAS-BOAS ATIMULIWA CHELSEA - DI MATTEO ARITHI NAFASI YAKE

Kwaheri AVB.
Hatimaye klabu ya Chelsea imemtimua kocha wake Andre Villas-Boas kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya ambayo Chelsea imekua ikiyapata  msimu huu.

Kufuatia kuondoka kwa Andre Villas-Boas klabu hiyo imetangaza kupitia webiste yake, kocha msaidizi Roberto Di Matteo anachukua nafasi ya AVB mpaka mwishoni mwa msimu.
Karibu Di Matteo.


AVB alijiunga na Chelsea miezi nane iliyopita na akimgharimu Abramovich kiasi cha paundi millioni 13 kumnyakua kutoka Porto.

MATCH LIVE CENTRE: SIMBA 2-1 KIYOVU: FULL TIME


19: Felix Sunzu anaipatia Simba goli la kuongoza.

24: Mafisango anakosa bao yeye na kipa.

30: Simba wanaonekana ku-relax na kiyovu wanakuja juu sasa.

32: Simba wanacheza counter attack na Emmanuel anapiga shuti kali linalopiga mwamba na kutoka nje.

35: Goaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaal, Simba wanapata bao la pili hapa, Mafisango anapiga penetration pass kwa Okwi nae anampasia Sunzu anayefunga bao la pili.

40: Kiyovu wanaonekana kutulia huku wakitafuta magoli ya kusawazisha. 

45: Mchezo ni mapumziko Simba 2-0 Kiyovu. Felix Sunzu amefunga magoli yote mawili pasi zote zikitoka kwa Emmanuel Okwi. 

45: Dakika 45 za mchezo kipindi cha pili ndio zinaanza. Kiyovu wamefanya mabadiliko ametoka Shyka ameingia Simon Okwi. 

47: Kiyovu wanapata faulo ndani 18 ya simba, lakini wanashindwa kuitumia vizuri.

50: Haruna Moshi Boban anapoteza mpira akiwa ndani ya 18 ya Kiyovu. 

55: Timu zinashambuliana kwa zamu. Huku Simba wakionekana hatari zaidi wanapoingia katika 18 ya Kiyovu. 

59; Kiyovu wanakosa bao hapa 

62: Patrick Mafisango anatoa pasi ya mwisho kwa Emmanuel okwi ambaye anawatoka mabeki wawili wa Kiyovu na kupiga shuti kali linalogonga mwamba na kutoka nje. 

65: Juma Kaseja anaokoa mchomo wa hatari hapa uliopigwa na Yusuph. 

74: Simba wanakosa bao la wazi kabisa.Patrick mafisango anapiga shuti kali na kipa anaokoa. 

75: Mwinyi Kazimoto anatoka nafasi yake inachukuliwa na Julius Mkude. 

76: Rodrigo anaingia kuchukua nafasi ya Simon Okwi aliyeumia kwa upande wa Kiyovu.

80: Juma Kaseja anaokoa hatari hapa, Kiyovu wanakuja juu sana na wakipata goli 1 lingine then Simba watakuwa wanayaaga mashindano haya.

78:  Kiyovu wanapata bao hapa

85: Haruna moshi anatoka anaingia Singano 'Messi'. 

90: Juma Kasejja anaokoa tena mchomo wa hatari hapa inakua kona 

91: Kaseja anaokoa tena mpira wa kichwa uliokuwa ukielekea golini 

92: Felix Sunzu anatoka anaingia Victor Costa, huku Juma Kaseja analala chini akionekana kuugulia maumivu.