Search This Blog

Tuesday, February 14, 2012

MECHI ZA LEO NA KESHO ZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE: HENRY KUIAGA VIZURI ARSENAL?








LyonAPOEL
Referee: Paolo Tagliavento (ITA) – Stadium: Stade de Gerland, Lyon (FRA)
LeverkusenBarcelona
Referee: Craig Thomson (SCO) – Stadium: Bay-Arena, Leverkusen (GER)
15 February 2012
ZenitBenfica
Referee: Jonas Eriksson (SWE) – Stadium: Stadion Petrovskiy, St Petersburg (RUS)
MilanArsenal

PAUL SCHOLES YUPO TAYARI KURUDI KUICHEZEA ENGLAND - REDKNAPP AKIWA KOCHA.




Mwezi mmoja baada ya kuhairisha uamuzi wake wa kustaafu na kurudi uwanjani kuitumikia klabu yake ya Manchester United, Paul Scholes sasa yupo tayari kurudi pia katika timu ya taifa ya England katika michuano ya EURO 2012.

Habari hizi zimekuja wakati England ikiwa katika wakati mgumu baada ya sakata la Terry lilopelekea kujiuzulu kwa kocha Fabio Capello.

Lakini pia uamuzi huu Scholes utakuwa mzuri mno kwa kocha atakayepewa jukumu la kuiongoza England in EURO.
Harry Redknapp, kocha anayepewa nafasi kubwa kumbadili Fabio Capello alikiri wiki iliyopita kuwa kama atakuwa kocha wa Three Lions basi atamchagua Scholes katika kikosi chake.

Na kiungo huyo mwenye miaka 37, ambaye alikataa wito wa Capello alipoitwa wakati wa kombe la dunia 2010, anaripotiwa kuwa yupo tayari kurudi dimbani kuisadia England kushinda kikombe cha ulaya kipindi kijacho cha kiangazi.

Scholes alicheza mechi yake ya mwisho ya kimataifa miaka 8 iliyopita wakati England ilipotolewa na Portugal katika michuano ya EURO 2004 kwa mikwaju ya penati.
Inasemekana aliamua kustaafu mapema baada ya kuwa frustrated kwa kuchezeshwa namba ambayo hakuipenda huku akiunda partnership ambayo haikuwa na mafanikio kati yake na Frank Lampard na Steven Gerrard.

Lakini majuto ya kukosa kucheza World Cup 2010 in South Africa ndio inasemekana sababu kubwa ya Scholes kuwa tayari kurudi dimbani kwa ajili ya kuitumikia kwa mara ya mwisho Three Lions.
Ikiwa Redknapp atachaguliwa kuwa kocha wa England, then tutegemee kumuona fundi Scholes ndani ya kikosi cha wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Euro 2012.
Kiongea kuhusu Scholes Harry alisema: “Mwangalie Paul Scholes, na tuwe wakweli, kama kocha ni lazima upende kuwa na mchezaji wa aina yake katika michuano mikubwa kama Euro.”

TEVEZ ARUDI ENGLAND - AGOMA KUOMBA SAMAHANI NA KUWAITA VIONGOZI WA CITY NA MANCINI WAONGO.


Carlitos akiwasili jijini Manchester leo hii.



Muda mchache baada ya kurudi England, Carlos Tevez amemtuhumu Roberto Mancini kwa kumtendea mambo ambayo hata mbwa hafai kutendewa na amembandika kocha huyo wa kiitaliano jina la “Muongo”.

Tevez amerudi leo Manchester baada ya kugoma kwa muda wa miezi 3.
Carlitos alimlipukia Mancini akiwa anakumbuka usiku wa mechi dhidi ya Bayern wakati Mancini alipogombana na Edin Dzeko, then akamfuata Muargentina huyo.
Tev alisema: “ Alikuwa katikati ya majibizano na Dzeko, akaniambia mie niendelee kupasha na kunitendea mambo ya kinyama na kitumwa.
Carlos Tevez akiingia katika mako makuu ya Manchester City.



“Alipoendelea kunisemesha kwa sauti ile kama anaongea na mbwa ndipo nilipomwambia sitofanya warm up.”
“Nilikuwa radhi kucheza lakini kocha alikuwa katika mood ya kijinga kwa sababu alikuwa anagombana na Dzeko. Pia baada ya Dzeko akanifuata mimi huku akitoa maneno machafu dhidi yangu, na muda wote huo nilikuwa mkimya.”

Pia Tevez alizungumzia juu uongo alioutoa Mancini katika kikao cha bodi ya Man City kuhusu kilichotokea usiku ule.


“Niliwaambia Man City, mimi ni mwajiriwa wa City inabidi mnithamini. Mancini amesema uongo kuhusu mimi na wakurugenzi wa Man City wanajua juu ya hili.
“Wanampendelea Mancini. Nataka City wawambie ukweli mashabiki.”

City na Mancini walikuwa na matumaini Carlitos angeitumia interview hii kuomba samahani na kuweka mambo sawa kati yake na klabu pamoja na kocha.

TAARIFA KUTOKA TFF

MANYONI FC YASHUKA DARAJA

Timu ya Manyoni FC ya Singida imeshindwa kutokea kwenye mechi ya Kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Polisi Tabora iliyokuwa ichezwe juzi (Februari 12 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Kwa mujibu wa Kanuni ya 21 ya FDL timu yoyote inayoshindwa kufika kituoni na kusababisha mchezo husika kutochezwa itashushwa daraja hadi Ligi ya Taifa na matokeo ya michezo yake yote itafutwa ili kutoa uwiano sahihi kwa timu zilizobaki kwenye mashindano. Si Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), msimamizi wa ligi hiyo Kituo cha Tabora, Alfred Sitta wala Kamishna wa mechi hiyo Charles Komba waliokuwa na taarifa yoyote ya mapema juu ya Manyoni FC kushindwa kufika kituoni. Manyoni FC ambayo mbali ya kushushwa daraja inatakiwa kulipa faini ya sh. milioni moja kabla ya kucheza Ligi ya Taifa msimu ujao ilikuwa Kundi C pamoja na timu za 94 KJ ya Dar es Salaam, AFC ya Arusha, Polisi Tabora, Polisi Morogoro na Rhino FC ya Tabora.

LIGI KUU YA VODACOM

Ligi Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya 18 kesho (Februari 15 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa viwanja vya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha, Azam Chamazi jijini Dar es Salaam, Mkwakwani jijini Tanga na Kaitaba mjini Bukoba. Mwamuzi Israel Mujuni atazichezesha JKT Oljoro na Ruvu Shooting jijini Arusha, Azam na Villa Squad zitachezeshwa na Judith Gamba jijini Dar es Salaam, Oden Mbaga ndiye atapuliza filimbi kwenye mechi ya Coastal Union na JKT Ruvu jijini Tanga. Mjini Bukoba kutakuwa na mechi kati ya Kagera Sugar na Moro United. Mechi nyingine ya raundi ya 18 itachezwa keshokutwa (Februari 16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Toto Africans itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar.

LIGI DARAJA LA KWANZA

Timu nane zinaingia viwanjani kesho (Februari 15 mwaka huu) kusaka pointi tatu katika mechi za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambayo sasa iko katika mzunguko wa pili hatua ya makundi. Kundi B ni kati ya Majimaji na Small Kids zitakazooneshana kazi Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati Mbeya City itaumana na Polisi Iringa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mechi za Kundi C zitakuwa kati ya Polisi Morogoro na Polisi Tabora kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro huku 94 KJ ikiwa mwenyeji wa AFC katika Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi. Keshokutwa (Februari 16 mwaka huu) Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi ya Kundi A kati ya Mgambo Shooting na Polisi Dar es Salaam jijini Tanga. Februari 17 mwaka huu kwenye uwanja huo huo kutakuwa na mechi kati ya Transit Camp na Morani ya mkoani Manyara. Mechi nyingine ya Kundi B itapigwa keshokutwa (Februari 16 mwaka huu) ikizikutanisha timu za Tanzania Prisons na JKT Mlale kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Amr Zaki avunja mkataba wake na Zamalek


Amr Zaki amekatisha mkataba wake na timu ya Zamalek SC baada ya timu hiyo kushindwa kulipa malimbikizo ya mishahara yake kufuatia ukata unaoikumba siku hiyo.

"Naidai Zamaleki LE 3,000,000 kuanzia msimu uliopita hadi msimu huu. Zamaleki pia wameshindwa kulipia gharama za upasuaji kufuatia majeruhi niliyoyapata wakati nikiichezea timu hii" - alisema Zaki.
Hili litakuwa ni pigo kubwa kwa Zamalek kufuatia kiwango kizuri alichokionyesha Zaki mwanzoni mwa msimu huu. Yanga imepangwa kucheza na Zamalek katika kombe la kilabu bingwa Africa mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka huu.

Zamalek ambao wako katika hali mbaya ya kiutawala, wana ukata mkubwa ambao umewalazimisha wachezaji wengi kutishia kuihama timu hiyo.

Rangers njiani kufilisika

Klabu ya soka ya Rangers, imethibitisha kwamba imewasilisha ombi lake kisheria mahakamani ikiwa na nia ya kupata watu watakaosimamia shughuli za klabu huku ikijitayarisha kutangaza kufilisika.
Klabu kimetangaza kwamba kitaendelea na shughuli zake kama kawaida, hadi kitakapotangaza uamuzi wa mwisho kama kitaendelea na hatua hiyo.
Rangers sasa ina siku 10 kufanya uamuzi.
Hayo yakiendelea, klabu kimetangaza kwamba mashabiki wenye tiketi za msimu mzima, na vile vile wenye hisa, wasiwe na wasiwasi wowote.
Hatua hiyo imechukuliwa huku Rangers ikisubiri uamuzi kuhusiana na ubishi juu ya ushuru, pamoja na faini mbalimbali, jumla ya deni ikiwa ni pauni milioni 49.
Kupitia taarifa, klabu kimeelezea kwamba ikiwa uamuzi huo utaamuliwa kwa idara ya forodha kushinda kesi, basi itamaanisha malumbikizo ya deni hilo na faini huenda yakazidi hata pauni milioni 50, na klabu hakitakuwa na uwezo wa kulilipa deni hilo.
Tajiiri anayemiliki klabu, Craig Whyte, alinukuliwa baadaye akisema deni hili huenda likazidi na kufikia pauni milioni 75.
Whyte, ambaye alinunua klabu kutoka kwa Sir David Murray mwaka jana, alisema suala la klabu kupata usimamizi mpya ni jambo la kufikiriwa iwapo klabu kitashindwa katika kesi hiyo kuhusiana na ushuru.

Monday, February 13, 2012

UNADHANI SUAREZ PEKEE NDIO MBAGUZI - ANGALIA HII KATIKA MECHI DHIDI YA ASTON VILLA NA CITY

Aron Ramsay asifunge tena jamani kwa staili hii!

IRENE UWOYA: CHELSEA WAMENIANGUSHA MSIMU HUU - LAKINI NAAMINI YANGA WATANIFARIJI JUMAMOSI



Mwanamaigizo wa kiwango cha juu hapa Bongo ametoa maoni yake juu ya kufanya vibaya kwa klabu ya Chelsea ambayo ndio timu ya nje anayoishabikia.

Uwoya ambaye ni mke wa mwanasoka Hamad Ndikumana anayekipiga katika ligi kuu ya nchini Cyprus amesema msimu huu Chelsea wamemuangusha sana lakini anaamini hiki ni kipindi cha mpito tu ila mambo yatarudi kuwa mazuri darajani


 "Msimu timu yetu imekuwa haipo vizuri kabisa, me napenda soka na Chelsea ndio ninayopenda kwa nje ya Tanzania. Naamini timu yetu inapitia katika mabadiliko ila mambo yataanza kukaa sawa na tutarudi kwenye chati tena. Nashukuru sasa hivi mchezaji wangu kipenzi Micheal Essien amerudi hivyo ataongeza uimara katika kikosi chetu."


Pamoja na kuizungumzia Chelsea pia mwanadada huyo amesema kwa hapa nchini anaipenda sana Yanga na anaamini wanajangwani watamfuta machozi wikiendi hii watakapokutana na Zamalek ya Misri.
"Nina uhakika Zamalek lazima wachezee kichapo wikiendi hii. Timu yetu ipo vizuri na sasa tuna mshawasha na spirit ya kufanya vizuri kwa sababu tupo katika kipindi cha kusherehekea miaka 77 tangu Yanga aianzishwe.





" Rafiki yangu kipenzi Jerry Tegete naamini hatoniangusha na atatupia goli kadhaa kwenye goli la waarabu siku hiyo. Mimi nitaenda uwanjani kama kawaida kwenda kuwasapoti watoto wa Jangwani na naamini tutashinda."

MICK McCARTHY AONGEZA IDADI YA MAKOCHA WALIOPOTEZA AJIRA EPL



Mick McCarthy amefukuzwa kazi kama kocha wa Wolves baada ya kuwa muendelezo wa kupata matokeo mabovu katika English Premier League.
Mwenyekiti Steve Morgan alifikia uamuzi wa kumtimua Mick baada ya Wolves kufungwa 5-1 na mahasimu wao West Brom.

McCarthy amekuwa kiongozi wa benchi la ufundi la ‘The Molineux’ kwa takribani miaka 5 lakini mashabiki walishaanza kukosa imani nae baada ya timu hiyo kushinda mechi 5 kati ya 25 walizocheza katika EPL msimu huu.

Baada ya kufukuzwa Mick McCarthy  sasa Terry Connor atachukua majukumu ya benchi la ufundi mpaka pale atakapopatikana kocha mpya.

BONANZA LA SERENGETI INTER BAR LAFANA JIJINI DAR ES SALAAM.

   NILIKUEPO KUIPA SUPPORT NAMANGA VETERANS

ANAITWA EVANS MANYANYA...HUYU JAMAA HUWA NAMFANANISHA NA DAREN BENT WA ASTON VILLA.



    NAMANGA..
    TEMBONI SOCIAL HALL
    BREAK POINT
    MANGO GARDEN

SIKU YANGA ILIPOSHEREHEKEA MIAKA 77 TANGU ILIPOANZISHWA..

             Mwanamuziki Barnaba akimuimbisha mama Fatma Karume
 Hapa ilikua zamu ya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mh Said Meck Sadiki
   Barnaba pamoja na bendi ya THT walikuepo kutoa burudani...

 Jamal Rwambo mmoja wa mashabiki wakubwa wa SIMBA alikuepo na kivazi chake chekudu.
     Hapa Ditto na THT Wakitoa burudani
 Mzee Ibrahim Akilimali akiitoa historia ya namna Yanga ilivyoanzishwa hapo mnamo 12/02/1935
    Koba Kimanga ( kati) akiwa na wadau wa Yanga..
    sehemu ya wageni waalikwa
  Kocha wa Yanga Kostadin Papic pia alikuepo kwenye mnuso huo..
                Anko Hashim Lundenga ( kulia ) pia alikuepo

    nilipata mwaliko pia kuhudhuria huo Mnuso...

    Sunday Manara ' Computer ' ( kulia ) pia alikuepo...

THIERRY HENRY IS A TRUE LEGEND, KUNA ANAYEBISHA ?

Zambia mabingwa Afrika 2012


Zambia imechukua ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2012 baada ya kuwafunga Ivory Coast kwa mikwaju ya penati 7-8.
Mchezo huo ulimaliza dakika 90 za kawaida, kabla ya kwenda muda wa ziada, na hadi katika mikwaju ya penati.
Ivory Coast wamekosa penati 2 kati ya walizopiga ambapo Kolo Toure na Gervinho walikosa mikwaju hiyo.
Ivory Coast wataendelea kusubiri kunyakua kombe hilo, licha ya kuwa na wachezaji kadhaa wanaocheza Ulaya hasa katika Ligi Kuu ya England.
Tembo wa Ivory Coast walipoteza katika mchezo wa fainali mwaka 2006 dhidi ya Misri kwa mikwaju ya penati.
Lakini kwa Chipolopolo, ambao wamewahi kushika nafasi ya pili mara mbili, wamemaliza kwa ushindi kwa kuhanikizwa na vifo vya wachezaji wenzao mwaka 1993, baada ya ndege yao kuanguka karibu na uwanja ilipochezewa fainali mjini Libreville.
Mara ya mwisho kwa timu hiyo kutoka Kusini mwa Afrika kufika fainali ilikuwa mwaka 1994, mwaka mmoja tu baada ya wachezaji 18 wa nchi hiyo kupata ajali ya ndege karibu na mji mkuu wa Gabon.
Wakielekea katika mchezo wa fainali, wachezaji hao wa sasa walisema wanahisi nguvu kutokana na kukumbuka janga lililowapata wenzao.
Kwa kushinda mchezo wa fainali, wameonesha dhamira ya kuwashinda wapinzani wao ambao walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kupata

Suarez aomba radhi


Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez na meneja wake Kenny Dalglish wameomba radhi kufuatia Suarez kukataa kumpa mkono Patrice Evra kabla ya mechi siku ya Jumamosi.
"Nimezungumza na meneja baada ya mchezo wa Old Trafford na nimetambua kuwa nilikosea," amesema Suarez katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo.
"Kila mmoja wetu ana jukumu la kuiwakilisha klabu hii katika mtindo unaofaa," alisema siku ya Jumapili.
"Jukumu hilo pia ninalo mimi kama meneja wa Liverpool.
"Nilipozungumza kwenye TV baada ya mchezo sikuwa nafahamu kilichotokea, lakini pia siku fanya kile kinachotarajiwa kufanywa na meneja wa Liverpool katika mahojiano, na ningependa kuomba radhi kwa hilo."
Manchester United ilitoa taarifa ikisema: "Manchester United inawashukuru Liverpool kwa kuomba radhi kufuatia matukio ya siku ya Jumamosi. Kila mmoja Old Trafford anataka kuondokana na jambo hilo.
"Historia ya vilabu vyetu viwili ni ya mafanikio na uhasama katika soka la Uingereza. Hilo ndio liwe lengo letu siku za usoni kwa mashabiki wanaozipenda timu hizi."
Suarez alifungiwa kucheza mechi nane kwa kumbagua na kumtusi Evra wakati wa mchezo wa ligi mwezi Oktoba mwaka jana.
Kukataa kwake kumpa mkono Evra siku ya Jumamosi kulichangia kuufanya mchezo huo kuwa wa vuta nikuvute ambapo United walishinda 2

Sunday, February 12, 2012

ONA KITUKO ALICHOFANYA SUAREZ DHIDI YA PATRICE EVRA.

MAFISANGO APEWA ONYO - HARUNA MOSHI AWAONDOA WAAMUZI KUCHEZESHA VODACOM PREMIER LEAGUE



Kamati ya Ligi imeagiza mchezaji Patrick Mafisango wa Simba aandikiwe barua ya onyo kutokana na kumsukuma mwamuzi Isihaka Shirikisho baada ya kumuonesha kadi nyekundu mchezaji mwenzake Haruna Moshi kwenye mechi kati ya Simba na JKT Oljoro.

Nayo klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya washabiki wake kurusha makopo ya soda na chupa za maji wakipinga uamuzi wa mwamuzi Shirikisho kumtoa kwa kadi nyekundu Haruna Moshi.

Wachezaji waliopigwa faini ya sh. 500,000 kila mmoja baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kutokana na kupiga ambapo pia wanakosa mechi tatu za ligi kwa mujibu wa Kanuni ya 25 ni nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa na Cyprian Lukindo wa Villa Squad............................

WAAMUZI, KAMISHNA WAONDOLEWA VPL
Waamuzi watatu na kamishna mmoja wameondolewa kuchezesha na kusimamia mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na kuonesha upungufu katika uchezeshaji na usimamizi.

Uamuzi huo ulifanywa na Kamati ya Ligi iliyokutana jana (Februari 11 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine ilipitia taarifa za waamuzi na makamishna wa VPL ambayo leo (Februari 12 mwaka huu) inaendelea katika raundi ya 17.

Peter Mujaya wa Mwanza aliyechezesha mechi namba 101 kati ya JKT Ruvu Stars na Yanga amefungiwa kwa miezi 12 kwa mujibu wa Kanuni ya 26(a) ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kushindwa kumudu mchezo huo, hivyo kupata alama za chini.

Naye Isihaka Shirikisho wa Tanga ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa VPL msimu huu kwa kushindwa kumudu mchezo namba 105 kati ya Simba na JKT Oljoro. Moja ya udhaifu alioonesha ni kushindwa kumuadhibu mchezaji Patrick Mafisango ambaye alimsukuma baada ya kumuonesha kadi nyekundu Haruna Moshi wa Simba.

Mwamuzi mwingine aliyefungiwa kwa miezi 12 kwa mujibu wa Kanuni ya 26(a) ni Kennedy Mapunda wa Dar es Salaam aliyechezesha mechi namba 107 kati ya Villa Squad na Simba. Moja ya udhaifu wa Mapunda ni kushindwa kumpa kadi nyekundu Fred Cosmas wa Villa Squad baada ya kumuonesha kadi ya pili ya njano.

Pia waamuzi wasaidizi Michael Mkongwa wa Iringa na Kudura Omary wa Tanga waliochezesha mechi namba 112 kati ya Yanga na Mtibwa Sugar wameondolewa katika mechi zilizobaki za VPL kwa kutokuwa makini. Mwamuzi wa mechi hiyo Ibrahim Kidiwa amepewa onyo.

Waamuzi wengine waliopewa onyo na kutakuwa kujirekebisha ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam aliyechezesha mechi namba 92 kati ya Moro United na Yanga, na mwamuzi msaidizi wa mechi ya Simba na Coastal Union, Issa Malimali wa Ruvuma.

Kamishna wa mechi namba 112 kati ya Yanga na Mtibwa Sugar, Mohamed Nyange ameondolewa katika orodha ya makamishna kwa mechi zilizobaki za VPL kutokana na ripoti yake kuwa na upungufu.

SIMBA NA AZAM ZAINGIZA MIL.67 UWANJA A TAIFA

Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Azam lililochezwa Februari 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 67,548,000.
 
Jumla ya watazamaji 19,257 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 117 kwa kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000 kwa VIP A.
 
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 10,303,932.20 kila timu ilipata sh. 13,182,800.34, uwanja sh. 4,394,266.78.
 
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,757,706.78, TFF sh. 4,394,266.78, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,197,133.39, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 439,426.78 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,394,266.78.
 
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. wamuzi wa akiba sh. 30,000, tiketi sh. 4,350,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
 
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 1,347,990,280 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 1,555,420.

WAPENZI WA YANGA IUNGENI MKONO TIMU YENU KWENYE MCHEZO DHIDI YA ZAMALEK.





Zimebakia siku kadhaa huku nyingi zikiwa zimeshapita kuelekea mchezo wa kihistoria kwa
klabu ya Dar es salaam Young Africans dhidi ya Zamalek Sc toka Misri. Yanga ambao masaa 24 yaliyopita wamesherehekea miaka 77 ya kuzaliwa kwake .


Kwa kawaida klabu za nchi za magharibi kama vile ulaya , Marekani ya kusini na hata za
hapa Afrika kwetu kama afrika kusini na misri wanakotoka za Zamalek zina utaratibu wa
kusherehekea miaka Fulani ya kuzaliwa au kuanzishwa kwa vilabu vya kwa staili ya aina
yake. 


Utakuta maandalizi yanafanywa kwa kutengeneza kumbukumbu za kudumu kwa muda
mrefu na si vitru vya kupita . Mfano mzuri ni Man United ambao misimu michache iliyopita
walitengeneza jezi maalum za kumbukumbu ya ubingwa wake wa kwanza wa ulaya uliopatikana mwaka 1968 kwa kuifunga Benfica ya Ureno. 


Arsenal nao waliwahi kutengeneza jezi maalum za kuadhimisha miaka 100 ya uwanja wa Highbury na nyingine nyingi huwa zina utaratibu kama huo , Yanga nao wangeweza kutengeneza japo jezi ambazo zingekuwa zimeandikwa miaka 77 kwenye nembo yake . 


Hawajachelewa kufanya hivyo na zawadi pekee kwa mashabiki na wapenzi wa Yanga katika kipindi hiki ambcho shamrashamra za maadhimisho ya miaka 77 ya kuanzishwa kwa Yanga bado mbichio itakuwa matokeo mazuri kama si ushindi katika mchezo dhidi ya Zamalek.


Historia haimpi hamasa mwanajangwani yoyote Yule kuwa na matumaini na mchezo wa
mwishoni mwa wiki ijayo lakini historia hizi hizi zimewekwa ili zivunjwe na watu wanaoandika makala kama hii hapa wapo kwa ajili ya kuwakumbusha watu wote kuwa mwaka Fulani historia Fulani iliwekwa na mwaka Fulani historia hii ilivunjwa na mtu Fulani.


Yanga wamekuwa na muda wa kutosha kujiandaa kwa mchezo huu hivyo hakuna anayetegemea kusikia sababu za hakukuwa na muda wa kufanya maandalizi ya kutosha .


Pamoja na hayo Yanga wamekuwa wakionyesha mchezo mzuri kwenye michezo ya ligi ambapo wameweza kupata ushindi katika michezo miwili mfululizo baada ya kuwa wameanza raundi ya pili vibaya kwa sare na Moro United . Kuitumia ‘perfomance’ ya Yanga kwenye ligi ya Vodacom kama kipimo cha jinsi watakavyocheza mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zamalek inaweza kuwa sio sahihi lakini matokeo mazuri yanawajengea wachezaji hali ya kujiamini jambo ambalo ni muhimu kwa mchezaji yoyote kuelekea kwenye mchezo mkubwa na hali hii itakuwa hivi hivi kwa Yanga ambao washambuliaji wao kina Hamis Kiiza na Kenetth Asamoah watakuwa wanajiamini vyema kutokana na hali nzuri waliyo nayo kuelekea kwenye mchezo huo.


Moja ya mambo ambayo yanaweza kuisaidia Yanga kufanya yale yasiyotarajiwa na wengi hasa kwenye mchezo dhidi ya Zamalek ni kuungwa mkono na mashabi na wapenzi wake
watakaojitokeza uwanjani siku ambapo wanajangwani watakuwa wanashuka dimbani kuwavaa waarabu. 


Kwa kawaida mashabiki wa soka la Tanzania wamekuwa na ‘negative mindset’ au kwa lugha rahisi ‘mawazo hasi’ kuzihusu timu za nyumbani kaka timu za taifa na klabu za Simba na Yanga.


 Kiukweli mazingira ya soka la ‘bongo’ hayamfanyi mtu awe na moyo kama alio nao shabiki wa Liverpool kwa timu yake lakini kila mtu anapaswa kuipenda timu yake anayoishabikia na kuwa tayari kuiunga mkono pale inapomhitaji pasipo kujali yale yanayotokea nyuma ya pazia .


Na hii inawahusu mashabiki wote wa Yanga na hata ikiwezekana wa timu pinzani kwao ya Simba kwani ikifanikiwa Yanga hata Simba imefanikiwa kwani wote kwa pamoja wanapeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la soka la kimataifa.


Umuhimu wa mtu ambaye kwa soka amekuwa akifahamika kama mchezaji wa 12 ni wa kipekee na michuano ya kombe la mataifa ya Afrika iliyomalizika huko Gabon na Equatorial Guinea jana imeonyesha hilo. 


Pasipo kutarajiwa na mtu timu kama Equatorial Guinea ambayo iliingia kwenye michuano ikiwa ya mwisho kwenye viwango vya ubora vya CAF na vya FIFA iliweza kufika robo fainali ikitandaza soka safi na kuzifunga timu ngumu kama Senegal na Libya , si wengi wangetarajia haya toka kwa timu hii lakini ukachilia mbali yale yaliyokuwa yanaendelea uwanjani mashabiki walikuwa na mchango mkubwa kuwafanikishia yale waliyoweza kuyatimiza na sioni kwanini hili lisiwe soma kwetu watanzania. 


Mashabiki wa Yanga wakipiga kelele tangu mwanzo hadi mwisho wa mchezo wachezaji uwanjani watapata nguvu ya kuamini kuwa wanaweza kutimiza yale waliyoagizwa na mashabiki maelfu waliofika uwanjani na hata wale ambao wameshindwa kupata nafasi ya kwenda uwanjani .


Kwenye mchezo wa marudiano kati ya Yanga na Zamalek utakaofanyika kule mjini Cairo ndio mashabiki wa Yanga watashuhudia ukweli wa haya yanayozungumzwa hapa kwani waarabu wanaiunga mkono timu yao mwanzo mwisho na mapenzi wanayoyaonyesha kwa mashujaa wao wanaopambana uwanjani ndio yanayowachagiza wachezaji 11 kufanya vizuri hivyo ni vyema mashabiki wa Yanga wakaanza kwa kuipa sapoti timu yao huku wakijua kuwa Yanga watakutana na hali tofauti mjini Cairo.


Kila mtu anaelewa kuwa huu ni mlima mrefu sana kwa Yanga kuupanda lakini penye nia pana njia na wachezaji na viongozi wa Yanga wameonyesha nia kwa kuiweka timu kwenye mazingira mazuri kwa upande wa viongozi na wachezaji wameonyesha matumaini kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakicheza kwenye michezo ya hivi karibuni , Mungu Ibariki Yanga , Mungu ibariki

BAADA YA OSAMA, STEVE JOBS, GADDAFI - AARON RAMSEY APIGA BAO NA WHITNEY AFARIKI


Ni ajabu lakini ndio ukweli, imekuwa ikitokea kila siku ambayo mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey anapofunga bao kwa timu yake ya Gunners basi kuna tukio la kifo cha mtu mashuhuri duniani kitatokea.

Alianza alipofunga goli siku ya May 1 2011dhidi ya Manchester United katika mechi ambayo Arsenal walishinda, masaa machache baada ya mechi dunia ilitangaziwa kuwa Gaidi namba 1 Osama Bin Laden aliuwawa.

Kwa mara nyingine tena Ramsey akafunga bao katika mechi dhidi ya Spurs tarehe 2 mwezi wa 10, 2011 na siku chache baadae mmiliki wa kampuni ya APPLE Steve Jobs akafariki dunia.

Baadae tarehe 19 October 2011 Ramsey akaifungia Arsenal goli dhidi ya Marsaille – masaa machache baadae tukatangaziwa kuuwawa kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.
Na jana tarehe 11/2/2012 Aaron Ramsey alifunga bao la kuongoza kwa Arsenal katika mechi ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Sunderland – na masaa machache baadae mjini Baverly Hills – USA sanaa ya muziki imekumbwa na masikitiko makubwa baada ya kuondokewa na mwanamuziki Whitney Houston.