| Baada ya kusubiri kwa takribani miaka 44, leo hii Manchester City wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England na kupata haki ya kuongea kwa majigambo ndani ya mji wa Manchester kwa takribani miezi 12 ijayo. Man City wamefanikiwa kuchuku ubingwa huo baada ya kuwafunga QPR 3-2 katika mchezo ambao ulidhihirisha kwamba miujiza inatokea kwenye soka. City walianza kufunga bao kipindi cha kwanza kabla ya Rangers kuswazisha na kuongeza bao la pili liliodumu mpaka dakika ya 92, ambapo Edin Dzeko akasawazisha na baadae dakika 94 na sekunde kadhaa Kun Aguero akafunga bao la ushindi lilomaanisha kwamba City wamewapora ubingwa mahasimu wao Man United ambao nao walikuwa wameshashinda 1-0 dhidi ya Sunderland. |
|
No comments:
Post a Comment