Pages

Tuesday, October 15, 2013

KUELEKEA DSM DERBY: 'YANGA WATAITANDIKA SIMBA - JANGWANI WAPO KAMILI, SIMBA BADO WAPO KWENYE KUJENGA TIMU.' ASEMA KOCHA WA AZAM


KOCHA wa Azam FC, Stewart Hall ameipa Yanga asilimia 90 ya kuibuka na ushindi katika pambano la Ligi Kuu Bara dhidi ya hasimu wake Simba litakalopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pambano hilo ambalo kwa kiasi kikubwa limetawala mazungumzo ya mashabiki wa soka nchini, litafanyika wakati ambao, Simba ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 18, wakati Yanga ipo nafasi ya nne na pointi zake 15.

Hall alisema: “Bila kuficha ukiniuliza nani ataibuka na ushindi Jumapili bila wasiwasi nitakwambia asilimia 90 Yanga itashinda, Simba ina asimilia 10 tu.

“Unajua kwanini? Yanga ina wachezaji bora zaidi lakini kubwa ni kwamba wamekaa pamoja kwa muda mrefu tofauti na Simba ambayo ndiyo kwanza inajengwa hivyo inahitaji muda.”

“Nakupa mfano, mabeki wawili wa kati wa Yanga yule Kelvin Yondani na Cannavaro (Nadir Haroub) wana uzoefu mkubwa na wamekaa pamoja kwa muda mrefu, ukija pembeni David Luhende ni kijana mdogo lakini amepevuka, Mbuyu Twite ni mchezaji bora,” alisema Hall.

“Nenda katikati Yanga ina Athumani Iddi, Haruna Niyonzina hawa ni wachezaji mahiri kabisa sidhani kama Simba ina wachezaji wanaoweza kulingana nao. Nataka unielewe kwamba nimezitazama hizi timu msimu huu mara mbili kila moja, hivyo nimebaini uzuri na upungufu wao.

“Ukiwatazama mabeki wawili wa kati wa Simba utagundua bado hawajazoeana sawasawa kama wale wa Yanga, kwa kifupi Simba ya sasa ni kama Azam yangu, kuna vijana wadogo wazuri lakini wanatakiwa kujifunza polepole kabla ya kuwa wachezaji wa kutegemewa,”aliongeza.

Lakini beki wa Simba, Joseph Owino amesikia maoni ya kocha huyo akamjibu kwamba wako vizuri na mechi hiyo haina mwenyewe.

“Kwa upande wetu tupo vizuri, mimi na mwenzangu, Kaze (Gilbert) hakuna shida tumekamilika, lakini mechi yetu na Yanga kulingana na uzoefu wangu wa miaka mingi, hadi sasa haitabiriki, nimewaona Yanga wanavyocheza ukilinganisha na sisi tunavyocheza nashindwa hata kutabiri naona atakayelala vizuri na kuamka na bahati atashinda,”alifafanua.

6 comments:

  1. Naona maoni ya huyu kocha yamebase sana kwenye hisia kwamba iwapo Simba ikishinda na ina kocha mzalendo basi sisi wa... tutakuwa hatu...

    ReplyDelete
  2. Nadhani wewe uliyetoa comment hapo juu ndio kilaza kabisa. Try to understand what do people mean! Sio unatuibulia tope lilojaa kichwani mwako eti sijui wazalendo huo ni ujinga. Sports family haina ujinga wa kubagua kama ni mzungu hau mweusi, the matter here just a vision towards reality.

    ReplyDelete
  3. Kama simba ni kama Azam kwa mujibu wa stiward hall,imekuaje azam wabov wakaifunga yanga??? Basi kwa kuwa simba ni kama azam bas simba itashinda 3-2

    ReplyDelete
    Replies
    1. Frank ndio kabwela kabisa wa mawazo! Ni uchovu wa maisha au ndio uwezo wa kufikiri umefikia mwisho. Kama sentensi chache umeshindwa kusoma na kuelewa sijui acpacity ya kichwa chako ni bites ngapi!
      Msijione wazima mjue kuwa wajinga nao ni ugonjwa

      Delete
  4. Mimi ndiye niliyeandika hiyo comment ya kwanza hapo juu lakini naona kuna mtu humu anajaribu kuchafuwa hali ya hewa. Bado sitaacha kupitia hii blog ya Dauda no matter what! Hayo yalikuwa maoni yangu tu!

    Hii blog naifagilia sana hasa inaporusha ile ishu ya MECHI LIVE

    ReplyDelete
  5. @Frank John ....Hahahahaaaaa ... You made my day! I second you! Amen

    ReplyDelete