Siku kadhaa baada ya afisa habari wa klabu Villa Squad, bwana Idd Godi Godi kuhoji juu ya harakati za viongozi wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara kuleta mchakato wa kuunda kampuni itakayoendesha ligi kuu ya msimu ujao. Huku akiwa anahoji ipo wapi ile kasi ya viongozi hao wa vilabu vya ligi kuu waliokuwa wakiongozwa na makamu mwenyekiti wa Simba Geodfrey Nyange Kaburu katika kuhakikisha TFF wanaiachia ligi iendeshwe na kampuni itakayoundwa na vilabu.
Baada ya kuripotiwa kwa hoja zile za bwana Godi godi ambaye nae alikuwa mmoja ya viongozi waliokuwa wakishiriki vikao vya kuhakikisha ligi kuu ya msimu ujao inachezwa ikiwa chini ya uendeshwaji wa kampuni kabla ya Raisi wa shirikisho la soka nchini Leodgar Tenga kuunda kamati ya ligi iliyoundwa na baadhi ya viongozi wa vilabu waliokuwa wakipigania kampuni.
Kuchaguliwa kwa viongozi wale kuingia kwenye kamati ya ligi iliyoundwa na Tenga kulionekana kupunguza kelele na kasi ya harakati za viongozi wale akiwemo Kaburu, Celestine Mwesiga, Meja Charles Mbuge, Said Mohamedi, Seif Ahmed 'Magari', na Henry Kabera, na kwa mujibu wa Idd Godi Godi anasema Leogdar Tenga aliwachagua viongozi hawa ili kuweza kutuliza zile harakati zao wote kwa pamoja na alifanikiwa kwani toka wakati huo ule mchakato umepotea au unafanywa kwa siri bila kutangazwa kwa hatua zilizofikiwa kama ilivyokuwa mwanzo.
Kufuatiwa hoja iliyotolewa na Bwana Idd, nikaona ni vizuri kuweza kuwasiliana na mmoja ya viongozi wakuu wa vilabu, Geodfrey Nyange Kaburu, ambaye alikuwa mstari mbele kutaka mabadiliko kabla ya kuingizwa kwenye kamati ya ligi na Tenga.
Baada ya kumuuliza ni wapi wamefikia kwenye mchakato wa kuunda kampuni itakayoendesha ligi kuu msimu ujao na kwanini wamekuwa kimya muda mrefu bila kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kama ilivyokuwa zamani, hivi ndivyo bwana Kabaru alivyojibu: "Kwanza kabisa nataka niweke vizuri jambo hili kwamba tumekuwa tumeacha kushughulikia mchakato wa kuunda kampuni ya kusimamia ligi kuu msimu ujao, la hasha viongozi wa vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu tumekuwa tukikutana mara kwa mara, na mara ya mwisho tumekutana ni Ijumaa ya wiki iliyopita, kwa bahati mbaya Iddi Godi Godi hana taarifa hizo kwa kuwa klabu yake imeshuka daraja hivyo wamepoteza sifa ya kushiriki kwenye vikao. Lakini so far mipango ipo vizuri sana, tumefika hatua za mwisho mwisho kabla ya kupeleka mpango au mfumo mzima jinsi na namna ligi itakavyoendeshwa na kampuni yetu. Kwa bahati nzuri mkutano mkuu wa TFF chini ya Raisi Tenga ulishatoa maamuzi ya kubariki suala la kampuni huku wakitoa mamalka kwa kamati ya utendaji kutusimamia mpaka tukamilishe mchakato huu wa mabadiliko. Tunategemea wiki ijayo kupitia mwanasheria wetu tutapeleka mfumo rasmi na mpango wote wa jinsi ya kuanzisha kampuni hii na mfumo wa kuendeshwa kwa kamati ya utendaji ya TFF ili kupata baraka zao.
"Pia lingine kubwa ambalo tumelipanga kwa sasa tupo kwenye mazungumzo ja kampuni moja ya kimarekani ambayo kama mambo yakienda sawa ndio itakuwa inayosimamia shughuli zote za kampuni yetu na kuziacha klabu zibaki zikicheza mpira tu. Tumefanya hivi ili vilabu visijihusishe na uendeshwaji wa kampuni moja kwa moja ili kutoa ile hali ya klabu fulani kufanya vitu fulani kwa jili ya kujipendelea(conflict of interest) jambo ambao tumelishuhudia kwenye hii kamati ya ligi ambayo tumeiendesha kwenye nusu ya pili ya msimu."
Alipoulizwa kuhusu mipango ya kutafuta mdhamini mpya baada ya mkataba wa mdhamini wa zamani kuisha, huku ikizingatiwa kwamba ligi ipo karibuni kuanza Nyange alijibu: "Hilo nalo ni moja ya majukumu ya mwanzo tuliyonayo viongozi wa viabu na tunalifanyia kazi, mpaka sasa tupo kwenye mazungumzo na kampuni ya Vodacom ambao wameonyesha nia ya kutaka kutoa mkataba mpya na mungu akijaalia tunaweza tukatoa taarifa rasmi wiki jayo wapi tulipofikia," alimalizia Kaburu.


umefika wakati viongozi wetu wa vilabu wawe serious.suala la kuanzisha ligi ya itakayoendeshwa na kampuni halina mjadala kianchotakiwa kufanywa ni watu kuwa commited.tuache siasa za kwenye media.hatahivyo naunga mkono ligi iendeshe na kampuni ndio mpira wa kileo.
ReplyDeleteH.sato