![]() |
| Wachezaji wa Simba na Yanga katika moja ya mechi zilizozikutanisha timu hizi. |
KLABU kongwe za Simba ya Yanga za jijini Dar es Salaam, zinaingiza
mamilioni ya pesa kila mwaka kupitia viingilio vya uwanjani, lakini
kutokana na mlolongo wa makato toka taasisi mbalimbali, zimejikuta
zikiambulia kiasi kidogo kulinganisha na kilichovunwa.
Mbali na
makato toka taasisi hizo, likiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
ambalo huzoa mgao mkubwa, jambo lingine linaloziponza klabu hizo ni
kutokuwa na viwanja vyao binafsi ambavyo wangeweza kuvitumia kwa ajili
ya mechi zao mbalimbali na hivyo kupunguza makato.
![]() |
| Huu ni watu umati wa mashabikiwa timu hizi mbili kongwe. Mapato yatokanayo na viingilio vya watazamaji hawa yanaenda sehemu nyingine kwa asilimia nyingi kuliko zile wazipatazo Simba na Yanga. |
Baadhi ya
makato 'yanayonyonya' klabu hizo ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF), Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Chama cha Mpira
wa Miguu Dar es Salaam (DRFA), gharama za uwanja kama ulinzi, usafi,
umeme, tiketi nauli za ndani kwa waamuzi na kamishna, posho za kujikimu
kamishna na gharama za kuwalipwa wajenzi wa uwanja, kampuni ya China
(Beijing Construction).
Yanga pamoja na kumiliki Uwanja wa Kaunda,
lakini haufai na hauna kiwango cha kuchezwa mechi za Ligi Kuu, na Simba
haina kabisa uwanja wake binafsi zaidi ya kumiliki eneo wanalotarajia
kujenga uwanja.![]() |
| Azama FC mfano wa kuigwa kwa Simba na Yanga. |
Klabu ya Azam FC iliyoanzishwa miaka ya karibuni ndiyo pekee nchini yenye uwanja wa kisasa unaokidhi mahitaji ya mechi za Ligi Kuu, hali ambayo imefanya kukwepa baadhi ya makato.
Kwa
mfano, msimu wa 20l0/2011 na 2011/2012, mechi nne za Ligi Kuu
zilizozikutanisha timu hizo, zilipatikana kiasi cha Sh979.5 milioni
lakini baada ya makato kila mmoja akaambulia Sh227.7 milioni tu.
Kiasi hiki walichopata ni kidogo kulinganisha na pesa zilizoingizwa na klabu hizo katika mechi hizo nne baina yao, achilia mbali mechi nyingine za ligi hiyo na michuano mingine ya kimataifa.
Kiasi hiki walichopata ni kidogo kulinganisha na pesa zilizoingizwa na klabu hizo katika mechi hizo nne baina yao, achilia mbali mechi nyingine za ligi hiyo na michuano mingine ya kimataifa.
![]() |
| Hawa ndio viongozi wa Simba na Yanga |
Hii ina maana kwamba,
klabu hizo zimekuwa ziingiza kiasi kikubwa cha pesa, lakini zimejikutaka
zikiambulia kiasi kidogo kutokana na orodha ndefu ya makato.
Katika
misimu miwili, Simba na Yanga zilikutana mara nne, mara tatu kwenye
Taifa, Dar es Salaam na mara moja Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ambapo
Yanga ilishinda michezo miwili, sare moja na Simba kushinda mmoja.
Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, mchezo wa kwanza wa timu hizo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Oktoba 18, 2010, ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, zilipatikana Sh138 milioni.
Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, mchezo wa kwanza wa timu hizo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Oktoba 18, 2010, ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, zilipatikana Sh138 milioni.
Mapato
hayo yalivunja rekodi ya yale ya awali yaliyosomeka Sh105 milioni
katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika kati ya Taifa Stars na Senegal mwaka juzi.
Jumla ya
watazamaji 25,000 waliingia uwanjani kwenye mchezo huo kwa kiingilio cha
juu Sh30,000 na cha chini 5,000, ambapo kila timu uliambulia Sh33.4
milioni.
Machi 5, 2011 katika mzunguko wa pili, ambapo timu hizo
zilitoka sare ya bao 1-1, ziliingiza Sh243 milioni baada ya kuingia
watazamaji 46,539, ambapo kiingilio cha juu kilikuwa Sh30,000 na cha
chini Sh3,000. Katika mgao huo kila timu iliambulia Sh51.1 milioni.
Aidha,
katika mchezo namba 78 uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam, Oktoba 29 mwaka jana, timu hizo zilivuna kiasi cha Sh337.5
milioni.
Pesa hizo zilipatikana baada ya kuingia uwanjani
watazamaji 53,366 kwa kiingilio cha chini Sh5,000 na kila cha juu zaidi
Sh20,000 kwa siti za VIP A. Yanga ilishinda bao 1-0.
Baada ya
makato, kila timu iliweka mfukoni kiasi cha Sh77milioni, na mchezo wa
mwisho ya Ligi Kuu msimu huu ulikuwa Mei 6, ambapo watazamaji 41,733
waliingia uwanjani.
Kiasi cha Sh260.9 zilipatikana na kila timu
ikaweka mfukoni kiasi cha Sh62.6milioni, ambapo Simba iliibuka na
ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Yanga.
Katika misimu hiyo miwili,
msimu wa mwaka 2011/2012 ndiyo uliokuwa na mavuno mengi kwa timu hizo
kulinganisha na msimu uliotangulia kwa tofauti ya Sh61 milioni.
Akiongelea
hali hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwasigwa alisema mfumo wa
makato wa unaziumiza kwa kiasi kikubwa klabu ambazo msingi mkubwa wa
kuziendesha utegemea mapato ya milangoni.
"Kweli makato ni makubwa
sana, kuna mlolongo mrefu wa gharama ambazo zinalipwa toka kwenye
viingilio. Kwa hali hii, klabu zetu haziwezi kusonga mbele," alisema
Mwasigwa.
Mwasigwa alisema wamezungumza mara kwa mara na TFF
kuhusu makato hayo, lakini hakuna ambalo limeweza kufikiwa mpaka sasa.
"Tunahitaji mabadiliko yenye kuzinufaisha klabu na siyo kuzinyonya."
source: www.mwananchi.co.tz





No comments:
Post a Comment