Search This Blog

Wednesday, May 30, 2012

EDEN HAZARD: MAMBO MATANO MAKUU KUHUSU SOKA LAKE. - FAMILIA YAKE YOTE INACHEZA SOKA

Eden Hazard ndio jina liliopo kwenye kila mdomo wa mpenda soka duniani baada ya mbelgiji huyo kusema kwamba atajiunga na Chelsea kupitia akaunti yake ya Twittter.

Website hii leo inakuletea mambo matano makubwa usiyoyajua kuhusu mwanaume huyu kabla ya hajahamia rasmi darajani.

HAJIAMINI SANA
Inaweza ikawa ngumu kuamini, lakini Hazard amekuwa sio mtu kujiamni muda wote kwa kipaji chake ambacho kimepelekea vita kubwa miongoni mwa giants teams katika soka la England.

Hazard alitemwa katika timu yake ya Lille na kocha Rudi Garcia mwezi September 2010 kutokana na kucheza kwa uwezo mdogo.

Lakini Hazard alirudi kwa nguvu katika raundi ya pili ya msimu na baadae alikiri, "Miezi miwili ya kwanza ya msimu ilikuwa migumu sana. Siwezi kusema kwamba nilianza kuwa na mashaka na uwezo wangu, lakini kiukweli nilikuwa na wakati mgumu sana."

FAMILIA YA SOKA
Kuna vipaji vingi katika familia ya Hazard ambayo unaweza ukaunda timu ya watu watano na bado ukapata nafasi ya substitution.
Wazazi wake wote walicheza semi-proffessional level, mdogo wake mwenye miaka 19 Thorgan anacheza katika klabu ya Lens wakati wadogo zake wengine Ethan(14) na Kylian (6) wapo kwenye academy ya timu ya zamani ya Hazard AFC Tubize.



WAKWANZA KWENYE KILA KITU
Pamoja kuwa mchezaji wa kwanza kutangaza uhamisho wake kwenye Twitter, Hazard pia amevunja rekodi nyingi
Alikuwa ndio mchezaji wa kwanza ambaye sio raia wa Ufaransa kushinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa ligi kuu ya Ufaransa, wakwanza kushinda hiyo kwa mara mbili mfululizo na kuwa mchezaji mdogo zaidi kuifungia Lille goli katika historia ya klabu hiyo - goli lake dhidi ya Auxerre in 2008, akiwa na miaka 17.

BURGERGATE
Hazard mara kadhaa amekuwa hana mahusiano mazuri na timu ya Taifa ya Ubelgiji - huku makocha kadhaa wakimshtumu kwa uzembe na uvivu.

Kuna tukio moja la kukumbukwa wakati Belgium walipocheza dhidi Ututruki June 2010 - tukio ambalo baadae lilipewa jina la 'Burgergate'.
 Hazard alitolewa kwenye mchezo huo baada ya lisaa limoja na kwenda moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kabla ya camera hazijamuonyesha akiwa nje ya uwanja akila burger huku mechi ikiwa inaendelea.

HANA TABIA ZA KUJIRUSHA
Wakati uwezo wake mara kadhaa umekuwa ukiwatia mashaka makocha wake - lakini kitu kimoja ambacho huwezi kumtuhumu ni kuwa mtu anayependa kujirusha - kwa mujibu wa kocha wake wa timu ya vijana pale Lille.

Jean-Michel Vandamme, mkurugenzi wa ufundi wa Lille anasema: "Ni mshindani wa kweli, sio mdanganyifu kwa marefa na katu huwezi kumkuta akilalalmika baaada ya kuchezewa faulo.

No comments:

Post a Comment