tag:blogger.com,1999:blog-7666991204659384237.post2296894638991784194..comments2024-03-13T22:55:00.987+03:00Comments on Shaffih Dauda in Sports.: NIONAVYO MIMI: KUNA MUDA TUNAMUONEA BURE JAMAL MALINZIUnknownnoreply@blogger.comBlogger2125tag:blogger.com,1999:blog-7666991204659384237.post-58165951385914017782014-03-06T08:47:10.201+03:002014-03-06T08:47:10.201+03:00Siku moja kabla ya mechi hii nilimsikia Malinzi ak...Siku moja kabla ya mechi hii nilimsikia Malinzi akiongea kwenye kituo kimoja cha redio akiwataka Yanga wawe makini katika mchezo wa marudiano Cairo kutokana na fitna za wamisri wakiwa nyumbani kwao.Malinzi alidai kwamba alikuwepo uwanjani Cairo kwenye mechi ya Super cup baina ya Ahly na Sfaxien ya Tunisia na kwamba washabiki wa Ahly walifanya fujo za kurusha fataki,kuwasha moto na kupiga filimbi pale mchezaji wa timu pinzani alipokuwa anaelekea\ kufunga.Haya yalikuwa maneno ya uchochezi kwa washabiki tulio nao ambao niliwasikia wakiihamasishana kuwarushia chupa za maji benchi la ufundi la Ahly kwa kisingizio kuwa Malinzi amesema Yanga ikienda Cairo itafanyiwa fujo.Kiongozi wa hadhi ya Malinzi hakupaswa kuongea maneno kama hayo hadharani kwani aliangalia zaidi kujijengea umaarufu wake yeye binafsi kwa washabiki wa Yanga bila kuangalia athari za maneno hayo kwa kuzingatia upeo wa asilimia kubwa ya mashabaki wa soka wa Tz. Kama lengo lilikuwa ni kuwatahadharisha Yanga alipaswa kuwasiliana na viongozi wa Yanga kwa njia za kiutawala na sio hii aliyotumia.Pengine suluhisho la vurugu hizi ni Yanga na Simba kujenga viwanja vyao ili wadhibitiane wenyewe kwa wenyewe kwani watakapong'oa viti hasara zitakuwa kwa klabu zaoAnonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7666991204659384237.post-60482577883804461862014-03-05T20:24:04.053+03:002014-03-05T20:24:04.053+03:00Malinzi anahusika moja kwa moja na kushindwa kudhi...Malinzi anahusika moja kwa moja na kushindwa kudhibiti vurugu za mashabiki kwa kushirikiana na jeshila polisi.Polisi wanatakiwa kuangalia wanaofanya fujo jukwaani na sio kuwa watazamaji mpira waliolipa viingilio.Mimi nilifikiri kazi ya polisi ilikuwa ni kwenda jukwaani kuwakamata washabiki waliokuwa wanang'oa viti kwani iljulikana walikuwa wamekaa upande gani lakini badala kwenda upande ambao washabiki walikuwa wanarusha viti wao wakaenda upande wa washabiki waliokuwa wanarushiwa viti ili kuwadhibiti na kuwafukuza.Wakati wa vurugu hizi sikuona hata kiongozi mmoja waTFF akihangaika kutuliza washabiki badala yake ni viongozi wa Yanga na Jeshila polisi ndio waliokuwa wanahangaika kuwatuliza washabiki hao.Malinzi aliahidi kuleta mabadiliko kwenye uendeshaji wa soka lakini hakuna jipya analofanya zaidi ya ubabaishaji.Namshauri aunde Kamati ya Usalama viwanjani na aweke watu makini wa kumshauri badala ya hawa makomandoo wa Simba na Yanga anaowakumbatia bila sababu za waziAnonymousnoreply@blogger.com