Pages

Wednesday, December 18, 2013

SHIRIKISHO LA SOKA UGANDA LAANDIKA BARUA FIFA KUULIZIA UHALALI WA USAJILI WA OKWI YANGA.



Shirikisho la soka nchini Uganda limeandika barua kwenda FIFA likisaka ufafanuzi kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Emmanuel Okwi aliyeuzwa kutoka SC Villa kwenda Yanga.

Siku ya jumatatu, Okwi alirirpotiwa kujiunga na mabingwa wa Tanzania bara klabu ya Yanga kwa ada ya uhamisho wa $100,000 kwa mkataba wa miaka miwili, na huku huko nyuma FIFA ilimuidhinisha Okwi kujiunga kwa mkopo na klabu ya SC Villa akitokea klabu ya Tunisia Etoile du Sahel.

Okwi ameichezea SC Villa katika ligi kuu ya Uganda kwa kipindi cha takribani miezi miwili akiifungia timu hiyo mabao matatu.

“Tumeiandikia barua FIFA kwa sababu tunahitaji watueleze kama uhamisho huo ni sahihi," alisema CEO wa FUFA, Edgar Watson.

Lakini mkurugenzi wa SC Villa, Edgar Agaba, aliongea na mtandao wa mntfootball na kusema kwamba mchezaji huyo alijiunga na klabu ya Yanga akiwa mchezaji huru.

Wiki iliyopita shirikisho la soka Afrika kilisema kwamba Okwi na Godfrey Walusimbi hawakuwa na uhalali wa kucheza kwenye michuano ya  2014 Africa Nations Championships (CHAN) kwa sababu walikuwa na matatizo na vilabu vyao vya zamani Etoile du Sahel na Don Bosco (DR Congo).

Itakuwa jambo la kuvutia kuona namna Okwi, ambaye alizuiliwa kucheza CHAN, akiruhusiwa kujiunga na klabu ya Yanga na huku akiripotiwa kuwa na matatizo na klabu ya Etoile du Sahel.hili.” alisema Watson.

14 comments:

  1. Naomba source ya hii Habari Tafadhali

    ReplyDelete
  2. Kwa hili naona kuna upande umeingizwa choo cha kike manake ikiwa sasa fufa wanaandik barua juu ya kutak kujua uhalali wa okwi kusajiliwa na yanga kwani wale walotoa ITC ya kumuidhinisha yanga ni kina nani? Yetu mato cie twaola mwishowe utakuaje

    ReplyDelete
  3. Picha lishafika katikati

    ReplyDelete
  4. Siye yetu macho na masikio mpaka tujue mwisho wq hii movie

    ReplyDelete
  5. Move inaengelea, ngoja tuone nan atakuwa staring

    ReplyDelete
  6. Figisu figisu zimeanza

    ReplyDelete
  7. NAOMBA MNIJIBU SWALI HILI:
    KWANI ITC INATOLEWA NA NANI? MSAADA TAFADHALI

    ReplyDelete
  8. Nyie waandishi wa Habari wa Bongo kuna muda siwaelewi Source za habari mna rely upande mmoja si muulize fifa kama kweli rage kafungua kesi ya madai dhidi ya etoile du sahel ili tujue kama kala hela okwi ili tumwadabishe

    ReplyDelete
    Replies
    1. ITC jamani kwani inatolewa na nani club atokayo,au Shirikisho la nchi atokayo au fifa?

      Delete
  9. mbona kizunguzungu, sc villa wauze mchezaji alie kwa mkopo kwao? ilo aliwezekani,naisi wanasimba wamepigwa changa la macho, watu wamechukua ela kitambo then wanazuga eti oooh ela bado atuja lipwa,naisi villa wanajitambua ndo maana wamemuuza kwenda yanga.viongozi simba wawe wakweli tu wawaeleze ukweli mashabiki wao.

    ReplyDelete
  10. Hata mimi ndhani media hazina uthubutu wa kujua mwisho wa hii Movie coz wangeenda Tunis wakajua ukweli, then FIFA na mwisho FUFA na Vila kisha wabalance taarifa ila wanasubiri habari za wenzao mitandaoni watasiri tu lugha.

    ReplyDelete
  11. Kinachotakiwa ni kuona ukweli uko wapi kati SSC na ESS pamoja na Villa. Kwani nina imani SC Vila hawana ubavu wa kumuuza Okwi kwenda Yanga hizo ni ndoto za mchana.

    ReplyDelete
  12. mm nimeingia kwenye oficial website ya etoile du sahel naona Okwi bado ni mchezaji wao na anamkataba had 2016 sasa hili suala linakuja vp kusajliwa Yanga?jaman Rage sidhan kala hzo pesa coz ww ni mtu gan ule pesa mchana kweupe namna hyo so mm naona pesa hajala bt may b ule mkataba wa mauziano na etoile kuna kipengele ambacho Simba hawakukielewa

    ReplyDelete
  13. Huyu ni mwandishi gani anayeandika habari za upande mmoja tu? Au anatumiwa na Rage ili kumsafisha? Alipashwa kubalance hizo taarifa kwa kuwasiliana na SC Villa na Etoile. Vinginevyo hapa tunamuona kibaraka tu wala haeleweki zaidi ya kurudiarudia taarifa bila kutatua utata wa habari yenyewe.

    ReplyDelete