Search This Blog

Wednesday, May 30, 2012

EURO 2012: MARIO BALOTELLI ASEMA ATAMUUA MTU YOYOTE ATAKAYEMFANYIA VITENDO VYA KIBAGUZI

"Jaribu kuleta habari za kunibagua kwa rangi then unipeleke jela kwa kukuua. - Mario Balo"
Mario 'Kichaa' Balotelli ametishia atatoka nje ya uwanja ikiwa atatukanwa kibaguzi kwenye michuano ya Euro 2012 na kuhaidi ataweza kumuua mtu yoyote atakayejaribu kumtupia ndizi.

Mshambuliaji huyo wa Manchester City ameongelea suala hilo kufuatiwa kuripotiwa kuwepo kwa tishio kubwa la ubaguzi wa rangi katika nchi ya Ukraine na Poland ambapo michuano ya ulaya inafanyika mwaka huu kuanzia wiki ijayo.

Mpaka sasa familia za wachezaji kama Oxlade Chamberlain na Theo Walcott zimesema hazitoenda kwenye Ukraine kwa sababu ya kuepuka kubaguliwa, lakini Kichaa mwenyewe Balo amesema hatokubalina na suala la kubaguliwa. "Haikubaliki. Ikiwa mtu yoyote atajaribu kufanya kitendo cha kunitupia ndizi uwanjani au mitaani, nitaenda kwa sababu nitamuua."

1 comment:

  1. Dah na huyu jamaa huwa hatanii anaweza kumuua mtu kweli, kwa akili zake zilivyo tu sina shaka na kauli yake.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete